Nadhani hili linapotosha maana nzima ya uongozi, ikifika kipindi kila mtu aamue basi hakuna umuhimu tena wa kuwa na kiongozi ambaye ni jukumu lake kulinda wananchi kwa sera bora na kulinda taifa, ukiachia kila mtu kivyake basi isiwe katika hili hata na mengine ya kuamua kuandamana au kutoandamana kila mtu shauri yake, ukaimua kukimbia speed 100 au 50 juu yako utaona lipi bora kwako. Hakuna uongozi wa namna hiyo kuna mawili tu black and white, mambo ya shaurieni yenu kesho kitakuja kipindupindu tutasema shauri yako ukitaka kufanya usafi au hutaki juu yako japo usafi ni bora. Kiongozi ni dira kauli yako ndio mwelekeo...Ni haki yako kuwa na mawazo kama hayo.
Rais katika hotuba yake, kwa lugha rahisi, ameeleza matumizi ya barakoa na madhara yake. Akatoa mifano ya nchi ambazo kuvaa barakoa ni sheria bado maambukizi yapo na wanakufa kwa wingi. Wataalam wa afya pia wanatoa angalizo la matumizi ya barakoa.
Hata vile amemwachia kila mtu kufanya uamuzi. Nawe rukhusa kufanya unaloona litakupitisha salama kwenye janga hili mradi huwi mmoja wa watakao ambukizwa au kuambukiza kwa sababu ya ujuaji na/au ujeuri