Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Unayajua majukumu ya Rais?? isome katiba vyema hapo ndipo kuna msingi wa malalamiko, wananchi hawakurupuki.
Afya yako ni wajibu wako. Anza kwanza wewe kutelekeza wajibu wako..unataka rais aje akuvalishe barakoa na unaijua corona vizuri. Acha visingizio
 
Tiyari ameanza kukubali taratibu, nilivyokuwa nasikia namna anavyozungumza Majaliwa kwenye Msiba wa Balozi kijazi nikajua kabisa anasafisha njia kwa Jiwe kukubali Corona ipo nchini na watu wanapaswa kuchukua taadhari

Mimi nashauri angehutubia Taifa moja kwa moja kuhusu hili suala linalogharimu maisha ya watu na siyo kujificha makanisani kutoa matamko ya chini kwa chini kwa Jambo serious kama hili
Kwahiyo mkuu wewe kuanza kuchukua tahadhari mpaka Rais aongee?

Au kuamini kuwa Corona ipo mpaka Rais aseme?

Kwa Hali kweli ni halali elimu iendelee kutolewa bure.
 
Ni mungu yupi unaemkusudia?
Wewe ni mjinga wa kiwango cha kumzidi shetani kabisa. Serikali kama serikali ule ni ufalme uliosimikwa na Mungu, mambo yote unayoyaona usije dhani yapo kwa bahati mbaya, ni calculated. Uzuri rais wetu anahofu ya Mungu na anamuamni Mungu ndiye mponyaji wa taifa, so ujinga wenu wala si kitu kwake.
 
Kwahiyo mkuu wewe kuanza kuchukua tahadhari mpaka Rais aongee?

Au kuamini kuwa Corona ipo mpaka Rais aseme?

Kwa Hali kweli ni halali elimu iendelee kutolewa bure.
Kila mmoja awajibike kwa upande wake, Kiongozi ana nafasi yake, Raia pia ana wahibu wake
 
Mbona ameishia tu kukejeli waliovaa barakoa kwamba eti hawana imani? Tena akamsifu babba paroko kwa kutovaa barakoa, huku akizikandia na kudai zimeletwa na na mabeberu kutuangamiza watanzania eti kwa sababu ya vita vya uchumi! Mimi nadhani kuna mtu anamdanganya na kumpotosha rais! Sio kwa maboko haya! Au nyie mmepata taarifa wapi?
 
Uko nyuma Sana mkuu, Mimi Naamini pia kuwa Corona ni vita ya kiuchumi hasa Kwa mataifa makubwa,
Uchumi gani ambao Tanzania iko nao hadi mataifa makubwa yafanye nayo vita? South Afrika, Misri, Nigeria wao watasemaje kama Tanzania itasema ni vita? Tumia hata ka akili kadogo uliko nako kufikiri.
 
Ameyasema hayo baada ya kuona corona imepiga hodi malango ya ikulu. Rejea post yangu niliyoitoa hivi karibuni kuhusu wagonjwa wa corona kiwandani kwangu hapa urafiki. Nilisema nikiwa kama naibu meneja mkuu ni lazima niwe mkweli maana mficha maradhi kifo humuumbua. Hii ni aibu kwa magufuli na serikali yake.
Aibu kubwa sana!! Tena sana! Tunaishi maisha ya sayansi,kama ni hivo afunge hata mahospitali na dawa wasitumie! Kama hataki cha mzungu arundi porini kuwinda na kuishi maisha ya kale.
 
Hivi huko kanisani ndio sehemu rasmi ya ku address janga kubwa na la kitaifa kama hili.

Alishindwa nini kufanya hotuba kama zile walizokua wanafanya watangulizi wake

Kipindi kile ukisikia rais anahutubia taifa basi station almost zote alikua anasikika live .
anatafuta uungwaji mkono na kanisa, kanisa hasa katoliki wamegoma.

Lakini pia mimi najiuliza, Rais yuko mis informed au ameamua tu kutudanganya kwa makusudi, Hivi Msd wanatengeneza barakoa au sanitizer? msd wana manufacturing plant wapi? sio wao wanaomba makampuni fulani fulani watengeneze hizo mask na sanitizer kwa jina lao. kama sivyo naomba kusahihishwa na kama ndivyo basi hata hayo makampuni yakiamua kusambaza maambukizi kwa njia hiyo kama anavyodai Rais mbona bado inawezekana. Mi sioni Rais anakataa nini na anakubali nini.
 
Uchumi gani ambao Tanzania iko nao hadi mataifa makubwa yafanye nayo vita? South Afrika, Misri, Nigeria wao watasemaje kama Tanzania itasema ni vita? Tumia hata ka akili kadogo uliko nako kufikiri.
Vita ya tembo nyasi ndio huumia
 
hesabu za wapi tena hizi jamani kubadili barakoa kila baada ya saa 8 utabadili mara 12 ndani ya saa 48?
 
Hii hotuba Rais ameitoa makusudi kumjibu Askofu mkuu yuda Thadeus ruwaichi. Hii siyo sawa kabisaa kufanywa na mkuu wa nchi. Halafu Rais magufuli huwa anatuonaje!?? Kwenye hotuba yake anasema; Barakoa kitaalam inatakiwa kuvaliwa kwa masaa 4, kisha uitupe na kuvaa nyingine. Rais anasema siku ina masaa 48, kwa hiyo utalazimika kuvaa barakoa 12 kwa siku..!!

Hivi Rais wetu mbona anatudharau Sana sisi wapiga kura wake!?? Yaani kweli siku moja ina masaa 48?? Halafu kwani barakoa unavaa hata ukiwa umelala??

Rais usitufanyie hivyo bhaana!
 
Hii speech ya leo imeonyesha ni jinsi gani amelishwa conspiracy theories....
i thought usomi wake ungemsaidia lakin 0.

yaan amejenga maadui wake kichwani ambao hawaonekani.

na mbaya zaidi analazimisha wananchi waamini the same.

na mtu yoyote aliekaribu nae asipoamini hivyo basi lazima afukuzwe ateuliwe mwingine.
 
Hii hotuba Rais ameitoa makusudi kumjibu Askofu mkuu yuda Thadeus ruwaichi. Hii siyo sawa kabisaa kufanywa na mkuu wa nchi. Halafu Rais magufuli huwa anatuonaje!?
Ameshajua wabongo ni fuata upepo. halad si watu wakuingia deep na kufanya research.
anaona powa tu akiongea lolote watu wataendea na huo upepo.
 
Hii paragraph imehitimisha nia ya serekali katika kupambana na janga la corona ni ipi.

Imagine social distancing pamoja na kuvaa barakoa vimepondwa na kuonekana kuwa havina maana na maombi yamewekewa msisitizo!View attachment 1708025
Kwani wapi amesema havina maana?

Mbona unataka kumlisha maneno?

Amesisitiza maombi kwa sababu Bwana asipoulinda mji waulindao wanafanya kazi bure!

Maombi ndiyo msingi wa yote..tukifanya hayo mengine yote tukasahau maombi itakuwa kazi bure.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom