Rais Magufuli: Wengine wanasema nipo Chato, kwani waliambiwa Chato sitakiwi kuwepo? Hapa si ndio nilipozaliwa na hata nikifa nitazikwa?

Rais Magufuli: Wengine wanasema nipo Chato, kwani waliambiwa Chato sitakiwi kuwepo? Hapa si ndio nilipozaliwa na hata nikifa nitazikwa?

Hapo kasema maneno murua Kabisa, "Mtu kwao".

Nashangaa kuna ''misukule'' kila kukicha inawazia ulaya, wakati hao ulaya wenyewe wanawadharau zaidi kuliko takataka za jalalani. Tatizo wengi hawawafahamu wazungu wamekuwa malimbukeni. ''charity begins at home.''
 
Mkuu almost nina all bidhaa muhimu za kula for two to three months ninazo home na pale ninapolazimika kutoka mask na sanitizer lazima iwemo kwenye mkweche wangu,,so bidhaa ninayonunua Kama IPO kwenye kivungashio lazima niipige sanitizer,Jumamosi nilikuwa naenda Moro, traffic police akanikamata kwa speed,kabla ya kugusa leseni yangu ilibidi nimpige sanitizer kwanza
Hongera kwa kuchukua tahadhari hizo. Waelimushe na waoendwa wako wengine wasio na uwezo kama wa kwako. Kwa pamoja tutavuka salama.
 
Brainwashing tu hakuna la maana hapo Eni wei tumuache afanye kwa utashi alio jaaliwa na Muumba
 
Heshima kwenu wakuu, binafsi naunga mkono msimamo wa Mh Rais Magufuli kuwepo Chato kwa sababu zifuatazo:

1. Chato ni sehemu ya Tanzania na ina haki zote za kutembelewa na viongozi kama ilivyo mini mingine.

2. Hakuna mtu ama RAIA yoyote nchi hii mwenye taarifa nyeti na mhimu kama Rais kwa hiyo Mimi na wewe hatiwezi jua washauri wa Rais wameshauri kitu gani. mpaka kupelekea Rais aendeshe shughuri zake Chato.

3. Rais ni Nembo ya taifa, kwa hiyo anapaswa alindwe na ajilinde dhidi ya maadui wa nje na ndani korona ikiwemo..hivyo ni mhimu zaidi Rais kubaki chato kuliko kuwa Dar es salaam ama Dodoma ambako maambukizi yanatajwa kuwa yapo juu na wizara ya afya.
 
Ukifuatilia Hotuba za rais Magufuri toka achukue nchi ,ameonekana kujua kila fani kumbuka sakata la makanikia, korosho , kuokota vichwa vya treni, vyeti feki,na Sasa Corona hivi haya yote Ana utaalam nayo ? Vipi Uchumi,siasa,uhusiano wa kimataifa,mambo ya ulinzi na usalama hivi ukiwa rais wa nchi unakuwa unajua kila kitu ,maana hata magenius huwa ni magenius wa fani husika sio kila fani ,hii imekaaje?Sasa naona na masuala ya dini.
 
IMG_20200506_154310.jpg
 
Poo Malendi, kama mmemsikia leo, amesema hivi! Wabunge ambao si Wa dar, watakamatwa Kwa uzurulaji ni Bora warudi kwao ama Bungeni

Wabunge nao bila kujua ilikuwa ni mtego kwamba watasemaje!!!

Mmoja alisema! Sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano Tanzania naweza kukaaa na nisiulizwe, jaribu kunishika uone, ni ukwli kabisa, mtu yeyote ktk nji hii anaruhusiwa kukaa mahali popote bila bighudha yoyote ile

Swali Kwa wabunge!! Raisi Yuko Chatto, Kwa nini Wao wanauliza maswali mengi Sana kumtaka atoke huko na ilihali hata yeye hajatoka nje ya Jamhuri hiii?
 
Kwa mujibu wa nyarakamakazi/ofisi ya raisi ni ikulu au ikulu ndogo kwenye mikoa au wilaya.
 
Kwa Tanzania yetu hii mpya, Rais yupo sio juu tu ya Sheria na Katiba, yupo juu hata ya "MBINGU".

Haina haja ya kua na Sheria wala Katiba nchi hii, kama "SPIKA WA BUNGE" anampitisha na kumtambua mbunge bila "UCHAGUZI WA WANANCHI KUMCHAGUA", basi pengine ana "KATIBA YAKE" anayoitumia alioitunga yeye na "MKE WAKE CHUMBANI WAKIWA FARAGHA".

Kila kiongozi, kuanzia wakuu wa mikoa/wilaya/vijiji/vitongoji nchi hii wana "SHERIA & KATIBA" zao wanazotunga na "WAKE/WAUME/VIMADA" zao vyumbani.
 
Back
Top Bottom