Rais Magufulli hawazii tena kuleta maendeleo ya Nchi ya Tanzania


Hivi hii salam munaikumbuka?😎😎
Ilitolewa lini vilee?😡😡😡😡
 
Dhana nzima kwamba maendeleo ya nchi yataletwa na rais ina makosa mengi sana.
kwa maoni yangu, mizizi yake ipo kwenye madaraka ya kifalme aliyopewa raisi, na utaratibu mzima wa mipango ya maendeleo ya nchi.

ilani ya chama, mwenyekiti wa chama, matamanio yake binafsi, madaraka ya kifalme.

Yaani anaweza kuja kwenye mtaa wako, akaamrisha kua wote mjengewe nyumba mpya na barabara kufika magetini, ndani ya miezi 6.. na ikawa hivyo.. wananchi wa hapo mtaani watasema ni nani kawaletea maendeleo? nani mwingine nchii hii ana nguvu hiyo?

nafikiri hivi ndivyo dhana ilivyojengeka.
 
Sikatai kwamba hayo unayoyasema ni kweli.

Ninachosema ni, kumuweka mtu mmoja kama ndiye "mleta maendeleo" ni makosa.

Kwa sababu, maendeleo ya nchi ni jukumu la wananchi wote.

Kwa sababu, watu wengi wanaweza kufanya maamuzi mazuri pamoja kuliko mtu mmoja.

Kwa sababu, rais ni kijakazi aliyewekwa na watu kuwatumikia watu kwa kufuata maagizo ya watu.

Kwa sababu, jamii ya kidemokrasia haitakiwi kuwa na "cult of personality" kama North Korea.

Kwa sababu rais anatakiwa kutekeleza ilani ya chama, si chochote anachotaka yeye tu.

Kwa sababu rais anatumia hela za walipakodi, si zake binafsi.

Kwa sababu maamuzi ya baraza la mawaziri yanapita kwa "collective responsibility", si maamuzi ya rais tu.

Kwa sababu nchi ni Jamhuri, si Ufalme usio na katiba.

Kwa sababu kanuni za ushirikishwaji wa umma zinakataza maamuzi kuhodhiwa na mtu mmoja.

Kwa sababu mtu mmoja kuhodhi mamlaka ya maamuzi yote ni "a single point of failure".
 
on point mkuu..
 
Dhana nzima kwamba maendeleo ya nchi yataletwa na rais ina makosa mengi sana.
Labda sio kweli mku lakini turudi nyuma kidogo tuone tangu zamani tunalipa kodi weeeeeee maendeleo ya haraka hatuoni labda wajumbe wavikao walikuwa wanakaa wengi kujadili hiyo miradi mwisho wa siku wanagawana posho alafu wanashtuka pesa zimebaki kidogo na mradi unaairishwa.
 
Una akili sana wewe mtu..
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…