Rais, Makamu wake na Waziri Mkuu wote wapo nje ya nchi?

DENG XIAOPING

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2022
Posts
2,396
Reaction score
2,598
Habari za sasa wanajamii , natumai ni nzuri.

Nilikuwa na maswali kadhaa kuhusu ziara za viongozi wetu wakuu wa nchi wa tatu (Rais, Makamu wa Rais, na Waziri mkuu)

1. Je ziara za viongozi wetu hawa kwa mataifa waliyo enda kuzuru zitatamatika lini kwa kila mmoja?

2. Kulikuwa na umuhimu gani kwa viongozi wote wakuu wa tatu wa nchi kwenda nje ya mipaka ya nchi yetu kwa wakati mmoja?

3. Kwa sasa kiongozi wa juu wa kiserikali ndani ya mipaka yetu ni nani (Cheo na jina lake)

4. Hatari ni ipi kwa nchi endapo viongozi wote watatu wa juu wa serikali wasipokuwepo ndani ya mipaka ya nchi yetu ?

5. Ni faida zipi taifa ina zipata kwa ziara za viongozi hawa watatu kwa mataifa waliyo zuru?
 
Zitatamatika soon baada ya shughuli iliyowapeleka kumalizika.
2. Kulikuwa na umuhimu gani kwa viongozi wote wakuu wa tatu wa nchi kwenda nje ya mipaka ya nchi yetu kwa wakati mmoja ?
Kila mmoja amekwenda kwa tukio muhimu, ila imetokea tuu matukio yamegongana.
3. Kwa sasa kiongozi wa juu wa kiserikali ndani ya mipaka yetu ni nani [ Cheo na jina lake ] ?
Tuna kitu kinachoitwa hierarchy anaanza Rais, VP, Rais wa ZnZ, PM, Spika, JM,
Wale VP wawili wa Zanzibar, katiba ya JMT haiwatambui!. Ikitokea wote sita hawapo, anateuliwa most senior cabinet minister mmoja kukaimu urais.
4. Hatari ni ipi kwa nchi endapo viongozi wote watatu wa juu wa serikali wasipokuwepo ndani ya mipaka ya nchi yetu ?
Hakuna hatari yoyote!. Ulinzi wa nchi ni chini ya CinC, ambayo haikaimishwi, CinC asipokuwepo nchini, ulinzi wa nchi uko chini ya CDF.
5. Ni faida zipi taifa ina zipata kwa ziara za viongozi hawa watatu kwa mataifa waliyo zuru?
Faida ni nyingi!.
P
 
hiyo hierarchy hujaiandika sawa kwa mujibu wa katiba

katiba inasema

raisi
makamu wa raisi
spika wa bunge
jaji mkuu

pm hayupo kabisa,anaangukia kwenye hilo group la anayeweza kuteuliwa na raisi kushika hiyo nafasi.

Sent from my BLA-L09 using JamiiForums mobile app
 
Umeelezea vizuri sana. Niongezee mchoro wa hayo maelezo yako...
 

achaga kupuyanga ngosha, CnC na ulinzi wapi na wapi??
 
Tuweke ivo vifungu vya katiba tuwaone hao sita
 
Mkuu Sam Wellson
Naomba uweke ibara na vifungu vinavyoelezea hilo (hayo mabadiliko) uyasemayo.

Kama ukiweza pia weka na huo waraka na sisi tuupitie ili kujiongezea maarifa.

It's document against document here.

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…