Rais Mama Samia Suluhu asipokuwa makini 2025 CCM itaondolewa madarakani

Rais Mama Samia Suluhu asipokuwa makini 2025 CCM itaondolewa madarakani

Zakamwamoba

Senior Member
Joined
Jul 28, 2016
Posts
177
Reaction score
609
Nimefuatilia sana mijadala inayoendelea nchini kuhusu utendaji kazi wa Mheshimiwa Rais. Mama Samia Hassan nimeona ameungwa mkono sana na watu hasa wale waliojipambanua kuwa ni Wapinzani.

Hii kitu ikanifanya nitenge muda kutafakari why? Tangu lini mtu wa CHADEMA akasifia utendaji kazi wa kiongozi wa CCM na kumuunga mkono wakti hata mwezi hajafikisha akiwa madarakani?

Kitu nimebaini ni kwamba CHADEMA wameona tayari kuna ulaji kwa huyu mama, hivyo wameona waanze kujipendekeza mapema ili wapate nafasi ya kumdefeat na kuguide huko mbele.

Hii kitu mama anatakiwa kukiangalia sana, Sifa za hawa watu siyo bure kuna kitu wanakiandaa. Haijawa tokea nchi hii mtu wa upinzani akafurahia kiongozi wa CCM namna hii.

Kikubwa mama awe makini, akicheza ngoma za hawa jamaa na kuwaacha wana CCM wenzake,CCM itakufa mikononi mwake. CCM haijwahi kuwa na urafiki na CHADEMA hata siku moja . Hizi pongezi kutoka upande wa pili mama aziangalie mara mbili mbili .
 
Sijui upinzani asimame nani ila kwa sasa wapiga kura(wananchi maskini)huwaambii kitu na CCM
 
Mlishazoea kuishi na shetani wenu huku mkimtia ndimu ili aendeleze ushetani wake na nyie mpate kula sasa amekufa mnataka kumpa ushetani mama wa watu Samia ili nae awe shetani. Nawaambia mmeshafeli na kushindwa. Mama Samia ndo Mandela wa Tanzania na Ccm iko salama chini yake.
 
Back
Top Bottom