Rais Mama Samia Suluhu asipokuwa makini 2025 CCM itaondolewa madarakani

Rais Mama Samia Suluhu asipokuwa makini 2025 CCM itaondolewa madarakani

Nimefuatilia sana mijadala inayoendelea nchini kuhusu utendaji kazi wa Mheshimiwa Rais,Mama Samia Hassan nimeona ameungwa mkono sana na watu hasa wale waliojipambanua kuwa ni wapinzani.

Hii kitu ikanifanya nitenge muda kutafakari why?,.Tangu lini mtu wa CHADEMA akasifia utendaji kazi wa kiongozi wa CCM na kumuunga mkono wakti hata mwezi hajafikisha akiwa madarakani?

Kitu nimebaini ni kwamba CHADEMA wameona tayari kuna ulaji kwa huyu mama,hivyo wameona waanze kujipendekeza mapema ili wapate nafasi ya kumdefeat na kuguide huko mbele.

Hii kitu mama anatakiwa kukiangalia sana,Sifa za hawa watu siyo bure ,kuna kitu wanakiandaa .Haijawa tokea nchi hii mtu wa upinzani akafurahia kiongozi wa CCM namna hii.

Kikubwa mama awe makini,akicheza ngoma za hawa jamaa na kuwaacha wana CCM wenzake,CCM itakufa mikononi mwake. CCM haijwahi kuwa na urafiki na CHADEMA hata siku moja . Hizi pongezi kutoka upande wa pili mama aziangalie mara mbili mbili .
Samia anamalizia miaka zake 4
 
Tuseme imeshakubalika kwamba wanaoikosoa serikali mitandaoni ni sauti rasmi ya CHADEMA? Huo uanachama wao unatambuliwaje? Halafu wananchi haohao wakiona kiongozi wa nchi anafanya vyema wakikubaliana naye wanatiliwa shaka kwa vile walishaikosoa serikali kwa kasoro kabla?

Mawazo ya aina hii ni ya kijinga sana. Huhitaji kuwa mnazi wa CCM kuona kwamba Mama Samia kaanza vyema kwa kusahihisha makosa ya msingi yaliyofanywa na Rais aliyepita. Kila mwananchi mwenye akili timamu amekubali. Kama wote wenye akili ni CHADEMA, so be it!

Kama kuwa CCM ni kuendekeza uozo ili kulinda chama basi hilo ni janga la kitaifa. Kwanza CCM haihitaji kura za wananchi kushinda uchaguzi. Sasa sijui Mama Samia ataiangusha CCM kivipi? Au umeshasahau tahadhari yake kuhusu kuunga kijiko cha sukari baharini?[emoji848]
 
Yule hana huo ubavu kwanza wapiga kura hawako twita wala JF,wapiga kura wapo vijijini,wauza samaki,machinga ndo CCM wanadeal na hao

CCM haihitaji kura kushinda. Ukipigia CHADEMA kura basi ni kama umeunga kijiko cha sukari baharini [emoji15].
 
Acha fitna, Mh. Raisi alisema tufungue ukurasa mpya au huelewi lugha
 
Kwani ikiondoka madarakani kuna shida gani?

Maendeleo hyana chama
 
Wapinzani ndio hawa akina mbowe unategemea nini, hilo labda utokee muujiza na uwe moja kati ya maajabu ya dunia
Ndio hawa hawa wakija CCM tunawapa madaraka huku sisi tukiendelea kusifu na kuabudu! Hapo ndipo uelewe kuwa % kubwa ya sisi wanaccm ni vilazer ndugu yangu! Upinzani ungekuwa dhaifu ccm tusingetumia mbinu chafu kushinda uchaguzi! We unadhani kwa nini hatutaki katiba mpya na tume huru ya uchaguzi? Tunajua fika hapo ndio tunapoponea!
 
Alishawahi kusema hata upinzani ukishinda ccm ndio itaunda serikali, tumuombe tu tufungue ukurasa mpya atuletee tume huru na katiba mpya itakayoleta usawa kwa watu wote wa JMT.
 
Mpaka Khery James anaomba radhi wewe bado uko kwenye giza totoro! Kwa ufupi wanaomsifu mama japo hapendi kutukuzwa, wana matumaini makubwa kuwa ataongoza nchi kama Watanzania wengi wanavyopenda nchi iongozwe isipokuwa wewe na kasuku waabudu sanamu wachache. Maendeleo hayana Chama in capital letter.
 
Hakuna. Hakuna. Hakuna.

Hakuna chama mbadala Tanzania.
Ni kweli kwa kulitumia jeshi na polisi pamoja na Tume ya CCM , hakuna wa kuiondoa CCM , nilisahau na msaada wa jeshi la Burundi pia ulisaidia kuiweka CCM madarakani
 
Nimefuatilia sana mijadala inayoendelea nchini kuhusu utendaji kazi wa Mheshimiwa Rais. Mama Samia Hassan nimeona ameungwa mkono sana na watu hasa wale waliojipambanua kuwa ni Wapinzani.

Hii kitu ikanifanya nitenge muda kutafakari why? Tangu lini mtu wa CHADEMA akasifia utendaji kazi wa kiongozi wa CCM na kumuunga mkono wakti hata mwezi hajafikisha akiwa madarakani?

Kitu nimebaini ni kwamba CHADEMA wameona tayari kuna ulaji kwa huyu mama, hivyo wameona waanze kujipendekeza mapema ili wapate nafasi ya kumdefeat na kuguide huko mbele.

Hii kitu mama anatakiwa kukiangalia sana, Sifa za hawa watu siyo bure kuna kitu wanakiandaa. Haijawa tokea nchi hii mtu wa upinzani akafurahia kiongozi wa CCM namna hii.

Kikubwa mama awe makini, akicheza ngoma za hawa jamaa na kuwaacha wana CCM wenzake,CCM itakufa mikononi mwake. CCM haijwahi kuwa na urafiki na CHADEMA hata siku moja . Hizi pongezi kutoka upande wa pili mama aziangalie mara mbili mbili .

Una maana gani "CHADEMA wameona tayari kuna ulaji kwa huyu mama"
 
Back
Top Bottom