mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
Baada ya kuisoma ilani ya chama tawala CCM na kusikiliza hotuba ya rais alipokua anafungua bunge watanzania wengi tuliiona nia ya dhati ya serikali yetu kuboresha uchumi kwa kiasi kikubwa haswa kwa kuhakikisha wawekezaji wanapewa support na serikali kwa kujengewa mazingira mazuri na rafiki ya uwekezajinyumbani
Pamoja na hayo yote niseme tuu bado tatizo lipo tena tatizo kubwa sana, either kwa kutokujua au kwa makusudi binafsi vyombo vya serikali vinavyotakiwa kuwaongoza na kuwapa ushirikiano wawekezaji vimekua vyombo vinavyowahujumu kiasi cha wengi wao kushindwa kabisa kufungua biashara, kushundwa kuendelea kuendesha biashara kwa waliokwisha kufungua, na wengi wao kuishia kufunga biashara kabisa na kurudi nyumbani
Mwanzoni mwa utawala wa Rais Magufuli tuliona vile alivyopambana na wahujumu uchumi; tuliona wakwepa kodi walivyowajibishwa, tuliona waliojitwalia mali za umma walivyozirudisha, tuliona wakwepa kodi walivyoshughulikiwa, tuliona Mabeberu walivyoshindwa kuendelea kuwakandamiza wenye haki na tukaona faida na nafuu kubwa
Kinachoendelea sasa ni kibaya zaidi, inaweza kuwa kwa kujua au kutokujua lakini taasisi nyingi za umma zimekua ndio vinara wa kukwamisha ukuaji wa uchumi nchini. Taasisi hizi hizi zimekua zikuhujumu juhudi za serikali kwa kuwahujumu wananchi na wawekezaji
Kumekua na vikwazo vingi sana BRELA, TRA, ARDHI na TIC na ashukuriwe rais kwa kuanza kumshughulikia TIC.
BRELA, hawa wamekua na urasimu uliovuka mipaka. Kusajili biashara Tanzania hadi ukamilishe imekua shughuli ngumu zaidi ya kununua figo. Brela walipoweka system mpya ya usajili wa online tulijua ingekua suluhu lakini ni yaleyale. Part ya system ipo outomated lakini baadhi ya vitu wanafanya manually ili tuu kuweka ugumu na kutengeneza mazingira ya kusumbua wafanyabiashara ili watoe rushwa. Pia system haionyeshi application imekwama wapi. Usajili wa kampuni Tanzania ni kazi ngumu na ya kuchosha mno. Waziri wa biashara, mkurugenzi wa brela angalieni hili ili kuongeza uwekezaji nchi tunajua liko ndani ya uwezo wenu.
BRELA mngetusaidia sana kama mngeweka wazi kwamba application inachukua muda gani na kama imepita muda bila majibu nani anawajibika.... hili la registration ya miezi nenda rudi linachosha sana
TRA ni kero mno, na hii kero rais amepambana nayo sana. Tatizo la TRA halipo kwa rais, waziri wa fedha wala mkurugenzi mkuu. Tatizo liko kwenye mfumo.
Mfumo wa TRA ulijaa watumishi wala rushwa na pamoja na juhudi zote zinazofanyika rushwa ndani ya TRA bado ni kubwa tuu. Tena sasaivi wanawatesa wawekezaji kwa kisingizio cha kutekeleza maagizo ya rais. Cha kujiuliza ni je, rais anajua mnavyowategeshea wafanyabiashara makosa ili muwacharge tozo zitakazojenga mazingira ya nyie kupata rushwa?
Wafanyabiashara wamechoka wameamua basi biashara hawafanyi tena... je TRA wanajua watu wangapi wanaumia kwa hizi biashara kufungwa? Wanajua serikali inapoteza mapato kiasi gani kwa kufungwa kwa biashara?
Officers wa TRA mnajua kabisa wawekezaji wengi hawana elimu ya kodi na mngeweza sana kuwasaidia wawekezaji kukuza mitaji yao kwa kuwasaidia kuepuka kulipa kodi wasizoweza na penalties lakini bahati mbaya mmegeuka kuwa watesi wao wa kukwamisha mambo ili wawape kitukidogo muweze kuwasaidi. Kwa hili mjue tuu mnamuumiza mkurugenzi wenu, mnamuumiza waziri wa fedha, mnamuumiza rais wetu na mnatuumiza watanzania
ARDHI na TIC walikua kikwazo kikubwa sana kwa wawekezaji. Wawekezaji wanafuatilia mambo wanazungushwa miaka hadi 3.
Miaka minne iliyopita kidogo pale ardhi kwenye upande wa uwekezaji palibadilika kuna boss mmoja anaitwa Bishanga Mungu atambariki sana kwa kutenda vyema kadri impasavyo. Ila sasa huyu boss sijui kama mambo yanaenda akiwa yeye mezani tuu? Anapokua nje ya office wale subordinates wake huwa wanafanya hujuma kubwa mno na kuwajengea mazingira magumu wateja ili wapewe rushwa. Bishanga ili team yako iangalie vizuri wale ndio wanasababisha mlundikano wa kazi na complain zisizoisha kwa wateja. Na kibaya zaidi sababu ardhi wanafanya kazi na TIC hii connection ya watumishi wahujumu inaenda kufanya ushirikiano mkubwa na wale wa TIC.... basi utasubiri vibali wewe mwezi, mwaka miaka! Wale wa TIC unaweza kuwapigia sim kuhusu request yako wasipokee, ukawatumia msg na kuwaambia unaenda kwa office yao wakakuambia hatupo officin, lakini ndani ya dakika tano unaingia pale unawakuta wamekaa tena kwa kurelax wanachat wassup. Ukiwauliza kuhusu barua zako wanaweza kukupa jibu kwamba, hapa ulikosea kuandika na ukiwauliza ulitakiwa kuandika vipi wanaanza ku-rephrase kile ulichoandika. Sijui hawa watu wanajikutaga werevu sana au ni hizo vyeo vimewalevya!?
Maofficer wanatengeneza tuu mazingira ya rushwa na rushwa yenyewe wanayotaka sasa utasikia dollar elfu5. Walau sasa kuna matumaini baada ya mheshimiwa rais kufanya maamuzi pale TIC.
Ila pamoja na yote wanaleta shida zote hizi ni wale maofficer wa chini kabisa, na hawa wanashirikiana na wa juu yao huku wakurugenzi wakiwa hawana habari
Kwa kweli wawekezaji wengi wanakuatana na vikwazo vikubwa sana na wanakata tamaa kiasi cha wengine kughairi na kuhamishia mitaji yao nchi nyingine ambapo process zao zinaeleweka na hakuna kusumbuana.
Rais, mawaziri na wakurugenzi mnafanya kazi kubwa na mnatumia nguvu mno ila wanaowakwamisha ni subordinates wenu wenye customer care mbaya na wala rushwa.
Kurahisisha kazi yenu mnge automate process zenu zote, tena msiache chochote kile kifanyike nje ya system kwa kisingizio chochote kile.
Kingine wawekeni watendaji wenu kwenye process na mteja anaporequest chochote kiwe channeled kwa mhusika na kuwe na turnaround time kwa kila kitu ili muweze kushughulika na wale ambao wanachelewesha kazi ambao queues zao hazisogei.
Pia tengenezeni mfumo wa kuwapa feedback, hii itawasaidia sana kujua maeneo na watendaji wenye matatizo na kushughulikia kabla ya kuwapoteza wateja
Pamoja kuboresha mfumo wa feedback toka kwa wateja. Kwa TRA commissioner angeongeza kipengele cha kuwapima na kuwawajibisha subordinates wake aliowapa majukumu kwa kila wilaya/kanda, wawe wanatoa reports na sababu za kueleweka pale anapoona wateja wanaongezeko kwenye penalties, kupungua kwa kodi, au kufungwa kwa biashara.
Hii itawafanya watumishi kuwa karibu na wateja kuwapa aina ya maelekezo kama training ambayo yatawafanya kujua sheria za kodi na kufanya vitu sahihi bila kuumizana. Na kwa mfumo waliojiwekea watendaji hili litawezekana tuu kama mfumo utalazimisha mwekezaji na commissioner kuwa na mawasiliano kabla ya kufungwa biashara vinginevyo hawa watu wa chini na wa kati wataendelea kuwatenda wawekezaji kwa kisingizio cha kutekeleza maagizo ya rais
Watanzania tuache maneno ya kila kibaya kinachotokea kusema kinafanywa makusudi na serikali ya CCM. Kwanza tukubali kwa miaka mitano tumeona rais wetu alivyo msikivu na mtendaji makini kwenye mambo yanayogusa maslahi ya watanzania na taifa kwa ujumla. Haiwezekani leo rais asisitize uwekezaji kwenye sekta binafsi halafu huyohuyo rais akwamishe wawekezaji.
Watanzania tuache kumtuhumu rais, watendaji husika tuache kumhujumu rais kwa kutowajibika.
Uwekezaji ni maendeleo ya mtanzania mmoja mmoja kupitia ajira, uwekezaji ni uboreshwaji wa huduma, uwekezaji ndio kichocheo cha kuongeza pato la taifa