Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Hawa waliokuja juzi kutoka aliko Lissu, Ubelgiji na EU, nao wamo kwenye hilo kundi au hawakukutana na UONGO wa Lissu!? Nenda Ulaya, nenda Asia, nenda UK, nenda Urusi au popote kule duniani, mifumo ya usimamizi na ya kisheria pamoja na vyombo na Taasisi husika vipo kote.Hakuna mwekezaji mwenye akili timamu anayeweza kuja kuwekeza nchini. Tatizo la kwanza nchi hii haiheshimu utawala wa sheria. Maofisa wa serikali wanaweza tu kujiamulia kushikilia au kufunga biashara binafsi kwa sababu ya kijinga kabisa. (Tumeona juzi Mkuranga RC anakataza mwenye kiwanda cha Rhino asihamishe mitambo kama kwamba na yeye ni mmiliki wa hiyo mitambo)
Nchi ina utitiri wa taasisi zinazowaandama wawekezaji kama mbu. Kuna TBS, BRELLA, Fire, NEMC, OSHA, Leseni, TRA, manispaa, jiji na kila ghasia. Katika mazingira kama haya hamna mtu atakuja kuwekeza.
Usilalamike, waambie wafuate taratibu za kuhamisha kampuni kama inavyoelekezwa kwenye makubaliano waliyoingia(Tumeona juzi Mkuranga RC anakataza mwenye kiwanda cha Rhino asihamishe mitambo kama kwamba na yeye ni mmiliki wa hiyo mitambo)
Hao walinunua. Unampangiaje mnunuzi pa kupeleka mali yake aliyonunua kihalali?Usilalamike, waambie wafuate taratibu za kuhamisha kampuni kama inavyoelekezwa kwenye makubaliano waliyoingia
Sawa endeleeni kusubiri wawekezaji. Dangote mwenyewe anaangalia exit strategy....Unaujua mkataba alioingia na serikali? Unawezaje kuzalisha bila kuwa na vitendea kazi?
Uwii uwii uwiii, kuna uwekezaji mkubwa mno unafanyika sehemu, umeme wamefuatilia from April of 2020 hadi sasa hivi!Sheria nyingi mno! Vibali vingi mno! Kodi nyingi mno! Rushwa nyingi mno!
Sawa. Je hii itakuwa tofauti na the so called ONE STOP CENTRE" au ni majina tu? Napita tu sijui!NI VYEMA SUALA LA UWEKEZAJI LIKAWA NA "ONE STOP DESK" YAANI OFISI AMBAYO ITAKUWA NA WATU WA VITENGO VYOTE MUHIMU BAADA YA WAZO LA MWEKEZAJI KUPITIA KWENYE DESK MOJA MAALUMU TU LITAKALOKUWA LINAUTATHIMINI MRADI HUSIKA KWA KINA TENA KWA WIKI MOJA TU THEN KAZI INATUPWA KWENYE ONE STOP DESK KWA UTEKELEZAJI WA HARAKA
Halafu ni lazima kuwe na utaratibu, vinginevyo, leo mwekezaji atajenga kiwandan say Arusha, baada ya muda, kwa sababu zake binafsi, atataka akihamishie say Mwanza! Hii siyo sawa na nini kitatokea kwa staff wa kwanza hapo Arusha, atawalipa au basi! Utaratibu lazima ufuatwe kwenye mambo muhimu kama haya.Usilalamike, waambie wafuate taratibu za kuhamisha kampuni kama inavyoelekezwa kwenye makubaliano waliyoingia
Brela na TRA wanasimamia hilo kwa karibu sanaHalafu ni lazima kuwe na utaratibu, vinginevyo, leo mwekezaji atajenga kiwandan say Arusha, baada ya muda, kwa sababu zake binafsi, atataka akihamishie say Mwanza! Hii siyo sawa na nini kitatokea kwa staff wa kwanza hapo Arusha, atawalipa au basi! Utaratibu lazima ufuatwe kwenye mambo muhimu kama haya.
Mama d tunapewa lengo na lazima ulifikieKuna watu walizoea kujichotea pesa za serikali sasa serikali imebana wanaumiza wawekezaji. Inasikitisha sana hii
Issue siyo kuondoa chama A kuweka chama B suluhisho ni strong taasisi zenye uwezo wa kusimamiana.Utakuja kushangaa hata CCM ikiondoka madarakani mambo yakawa ni yale yale. Kumbuka kuwa hata hao viongozi watakaokuja nao ni zao la mifumo na falsafa zile zile. Viongozi hao hawatatoka mbinguni.
Hebu angalia nchi za Kiafrika walikoweza kuondoa chama tawala na wapinzani kuingia. Ni wapi walikoweza kuleta mabadiliko ya kweli na kufumua mifumo na kuanza upya? Zambia? Malawi? Kenya (japo KANU ilikufa jina tu lakini tabaka tawala ni lile lile)?
Ila naungana nawe. Kuna haja ya kuwaachia na wengine wajaribu jamani. Liwalo na liwe japo wahenga waliwahi kutudanganya eti zimwi likujualo kamwe haliwezi kukula likakumaliza!