Rais mgonjwa mahututi mpaka mauti, lakini makamu wake hajui, aelezwi na anafichwa!

Yaani kiongozi wa nchi anaumwa muda mrefu, ugonjwa endelevu, anapotelea hospitalini majuma kadhaa, anapambania maisha yake kufa na kupona, hajiwezi. Lakini katika mazingira hayo hayo, taifa zima halijulishwi chochote, makamu wake hajui, aelezwi na anafichwa kimakusudi asijue chochote. Hatimaye Rais anafariki dunia, bado makamu wake hajui chochote, watu wengine wanakaa chini kujadili namna ya kuendesha mambo ya msiba bila makamu wa rais kujua chochote.

Tuseme ukweli, kuna nchi inaongozwa na kikundi cha watu wasiojulikana na kinyume cha katiba kwa 100%. Kuna kila dalili huenda mambo yakawa magumu zaidi huko mbeleni.
Huko ccm raisi na kikosi chake wote wapowapo tu hawajui nchi inaenda wapi
 
Huenda utakuja kujua baadae PENGINE VP alipelekwa Tanga kufichwa siku kadhaa kabla dhidi ya hila mbaya za kusema nae alipata mstuko baada ya Taarifa mbaya

miaka mingi ya baadae Taarifa nyingi zitafichuka

kuna siku pia tutapata jibu ilikuaje Waziri Mkuu alibadilishiwa usafiri kutoka wa Anga hadi wa ardhini na masaa machache baada ya safari kuanza akiwa na Msafara wa magari ya kutosha akatokea Jamaa na Gari akayavuka magari yote ya Msafara akaenda kuligonga la Mheshimiwa kwa mbele na akafariki Mkuu aliekuwa siti ya Nyuma japo alifungwa Mkanda na wengine wote walitoka salama Salmeen na Gari ikakutwa na uharibifu wa kawaida tu kwa mbele kwny Taa na Bampa upande wa kulia wakati Mkuu alikuwa siti ya Nyuma upande wa kushoto
Yes mkuu nimekusoma vema,nakubaliana nawe mengi tu ILA la Dube pale Dumila alikua anaendesha from opposite side,ilitakiwa a slow down au asimame ili msafara upite
 
Tuseme Inshallah, pia tutajua mara ya kwanza na ya mwisho gari zingine kuruhusiwa kutumia barabara sambamba na Msafara wa Waziri Mkuu ni siku hiyo ya ajali na si kabla wala baada yake
 
Kwani Samia amewahi kuthibitisha hivyo? Nashangaa wengi mnatumia kauli ya Mabeyo kama ndio final, au kwasababu alikuwa CDF!

Samia angeweza kupewa taarifa kwa njia nyingine za kimawasiliano, na wakati akipewa hizo taarifa sio lazima Mabeyo awepo, Mabeyo hajui hayo ndio maana hakuyazungumzia.

Mtambue tu, kile alichokizungumza Mabeyo kuhusu afya ya Hayati Magufuli simply alizungumzia part yake, kile alichokiona yeye wakati ule akiwa na mgonjwa hospitalini.

Lakini kama siku nyingine akatokea PM akazungumzia kile alichokiona au kukifanya wakati wa ugonjwa wa Hayati Magufuli, alipokuwa hospitalini nae, inawezekana akaja na majibu ya haya mengine ambayo tunajiuliza kila dakika.

Samia hivyo hivyo nae kama akiulizwa anaweza kusema alikuwa akipewa taarifa za kila kinachoendelea juu ya ugonjwa wa Hayati Magufuli, kumficha taarifa mtu wa karibu jambo zito kama hilo sio rahisi kama wengi mnavyodhani.
Ni miaka mitatu imekwisha tangu mzee akate moto, hakuna mwingine aliyezungumzia scenario nzima ya kifo cha mzee zaidi ya mstaafu wa jeshi. Kwanini tusitumie hiyo kama credible benchmark true story ya tukio zima mpaka sasa?
 
Yaani kiongozi wa nchi anaumwa muda mrefu, ugonjwa endelevu, anapotelea hospitalini majuma kadhaa, anapambania maisha yake kufa na kupona, hajiwezi. Lakini katika mazingira hayo hayo, taifa zima halijulishwi chochote, makamu wake hajui, aelezwi na anafichwa kimakusudi asijue chochote. Hatimaye Rais anafariki dunia, bado makamu wake hajui chochote, watu wengine wanakaa chini kujadili namna ya kuendesha mambo ya msiba bila makamu wa rais kujua chochote.

Tuseme ukweli, kuna nchi inaongozwa na kikundi cha watu wasiojulikana na kinyume cha katiba kwa 100%. Kuna kila dalili huenda mambo yakawa magumu zaidi huko mbeleni.
Nani aliokwambia Rais "hajui"?
 
Kwa hiyo ulaji uko upande wako na saa hii unaogelea kwenye mihela?
Miki siku zote ulaji upo na kukosa kupo pia, so nimeshazoea hali zote ndiyo maana siyo chawa wa mtu yeyote kama ulivyokuwa chawa wa Jiwe. Pole mkuu jaribu kuishi maisha yako bila kutegemea uchawa. Ila kama uchawa uko damuni njoo uwe chawa wangu
 
Yaani kiongozi wa nchi anaumwa muda mrefu, ugonjwa endelevu, anapotelea hospitalini majuma kadhaa, anapambania maisha yake kufa na kupona, hajiwezi. Lakini katika mazingira hayo hayo, taifa zima halijulishwi chochote, makamu wake hajui, aelezwi na anafichwa kimakusudi asijue chochote. Hatimaye Rais anafariki dunia, bado makamu wake hajui chochote, watu wengine wanakaa chini kujadili namna ya kuendesha mambo ya msiba bila makamu wa rais kujua chochote.

Tuseme ukweli, kuna nchi inaongozwa na kikundi cha watu wasiojulikana na kinyume cha katiba kwa 100%. Kuna kila dalili huenda mambo yakawa magumu zaidi huko mbeleni.
You think alikua hajui?

You dudes are soooo blinded
 
Back
Top Bottom