Rais Mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amuondolea Kinga ya kutoshtakiwa Rais wa zamani, Peter Mutharika

Rais Mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amuondolea Kinga ya kutoshtakiwa Rais wa zamani, Peter Mutharika

Ikiwa ni chini ya saa 24 tangu kuapishwa kwake, Rais mpya wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera amemuondolea kinga ya kutoshtakiwa aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Peter Mutharika ili aweze kushtakiwa.

Vilevile, ili kuhakikisha kuwa mizizi ya utawala katili uliojawa na rushwa uliopita inang’olewa na kuondoka kabisa serikalini, Rais Chakwera amemtimua kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini huko Duncan Mwapasa na kumteua Inspekta Jenerali Dkt. George Kainja kuchukua nafasi hiyo.

Rais Peter Mutharika hakupata muda wa kufuta baraza lake la mawaziri ingawa alitakiwa kufanya hivyo siku chache kabla ya uchaguzi kama ambavyo katiba ya Malawi inamtaka kufanya. Mawaziri waliokuwa katika baraza lake wametakiwa kurudisha mali zote za serikali wanazozishikilia ikiwamo magari waliyopewa na serikali kufikia siku ya kesho kabla ya saa tano asubuhi.

Wakati huohuo, kutakuwapo na mabadiliko makubwa katika Mamlaka ya Mapato ya Malawi yanayotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais Dkt. Chilima ikiwa ni juhudi za kukabiliana na rushwa katika ofisi kubwa za serikali.

**** Watawala wetu wana la kujifunza****

Former president Peter Mutharika has been stripped of his immunity from prosecution and that he can now face charges, a law expert has said.

University of Malawi’s Chancellor College dean of law Sunduzwayo Madise said following legal ritual of new leader Lazarus Chakwera being sworn in as President of Malawi after winning an election rerun, the immunity has been inherited by Chakwera while Mutharika has lost it.

“And just like that by operation of the law the immunity that the former president had against prosecution and suits is gone,” Madise wrote on his Facebook wall.

Saulos Chilima, the vice-president, during Mutharika regime and remains in that position as Chakwera’s deputy, accused Mutharika of high-level graft.

Mutharika’s Democratic Progressive Party (DPP) officials were involved in numerous graft scandals including former minister Ben Phiri and Chief Secretary to government Lloyd Muhara.

With law degrees from the University of London and Yale, Mutharika left Malawi in the 1960s to settle in the United States.

He returned to the country in 1993 to help draft its first democratic constitution after the fall of Hastings Banda’s dictatorship.

Mutharika went back to the US but returned home in 2004 when his brother came to power, serving as his informal advisor.

A widower for 30 years, Mutharika has three children. In 2014 he married his second wife Gertrude Maseko, a former member of parliament.

Mutharika has been defeated by Chakwera who secured the required majority, with 58.57% of the vote, the electoral commission said.
Hivi kinga inaondolewa na bunge au raisi?..
[emoji848]
 
Huyo Raisi mpya wa malawi kachemka,Vifungu vya raisi kutoshitakiwa vinatikiwa vifutwe na bunge tu sio raisi!!! yeye nguvu hizo hana kisheria washauri wake wamempotosha
Hivyo vifungu unataka vifuatwe na rais wa Malawi tu Magufuli hapana.
 

Ikiwa ni chini ya saa 24 tangu kuapishwa kwake, Rais mpya wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera amemuondolea kinga ya kutoshtakiwa aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Peter Mutharika ili aweze kushtakiwa.
Huyu Raisi mpya anataka kuleta machafuko tu Malawi kipengele cha Raisi anayeondoka madarakani kutoshitakiwa kiko kwenye katiba ya nchi kukibadilisha inatakiwa katiba ibadilishwe kwanza na uwezo huo kama Raisi hana ni bunge na kura za maoni za wananchi ndio zaweza kakosea kukifuta hana huo ubavu wa kuvunja katiba wazi wazi!!!

kifungu hicho cha katiba ya malawi namba 91 hiki hapa nanukuu


91. Immunity
1. No person holding the office of President or performing the functions of
President may be sued in any civil proceedings but the office of President shall
not be immune to orders of the courts concerning rights and duties under this
Constitution.
2. No person holding the office of President shall be charged with any criminal
offence in any court during his term of office.
3. After a person has vacated the office of President, he or she shall not be
personally liable for acts done in an official capacity during his or her term of
office but shall not otherwise be immune.
 
Hivi kinga inaondolewa na bunge au raisi?..
[emoji848]
Inaondolewa na bunge baada ya process zote kukamilika ikiwemo kura za maoni za kubadilisha katiba kuondoa hicho kipengele cha immunity ya raisi

Huyo RAISI Kauanza uraisi kwa kuvunja katiba
 
Huyu Raisi mpya anataka kuleta machafuko tu Malawi kipengele cha Raisi anayeondoka madarakani kutoshitakiwa kiko kwenye katiba ya nchi kukibadilisha inatakiwa katiba ibadilishwe kwanza na uwezo huo kama Raisi hana ni bunge na kura za maoni za wananchi ndio zaweza kakosea kukifuta hana huo ubavu wa kuvunja katiba wazi wazi!!!

kifungu hicho cha katiba ya malawi namba 91 hiki hapa nanukuu


91. Immunity
1. No person holding the office of President or performing the functions of
President may be sued in any civil proceedings but the office of President shall
not be immune to orders of the courts concerning rights and duties under this
Constitution.
2. No person holding the office of President shall be charged with any criminal
offence in any court during his term of office.
3. After a person has vacated the office of President, he or she shall not be
personally liable for acts done in an official capacity during his or her term of
office but shall not otherwise be immune.
Beba hicho kifungu ukamsaidie utetezi mahakamani...
 
Wala hajawaahidi watu maziwa na asali, hao watu walikuwa vikwazo vya demokrasia kwa kuchakachua Kira na mhimili wa wizi,. Raisi mpya na yeye alaumiwe kama atafanya makosa ya namna hiyo.
Samahani. Demokrasia ni nini??
 
Kuna wale nzi wa kijani huwezi kuwaona wakichangia kwa uhuru kwenye suala kama hili
 
Tumepokea taarifa kutoka Malawi, kuwa kiongozi mpya aliyechaguliwa kwa kura nyingi katika kura za marejeo, Lazarus Chakwera, katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki, ndani ya saa 24, tokea aapishwe, ameondoa kinga ya kutoshtakiwa, aliyokuwa amejiwekea, kiongozi anayeondoka madarakani, Peter Mutharika.

Tunajifunza nini kwa hatua hiyo iliyochukuliwa na kiongozi huyo mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera?

Kama Taifa tunachopaswa kujifunza, ni kuona uongozi ni kama dhamana ambayo tumepewa na wananchi, ambapo tunapaswa tujinyenyekeze kwa wananchi wote na tuwatumikie kwa usawa, hao wananchi waliotupa dhamana hiyo tuliyo nayo na tunapaswa tutekeleze majukumu yetu, kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, bila kuwaonea raia kwa kutumia vyombo vya dola, ambavyo tunaamini kuwa sisi ndiyo tunaovimiliki.

Viongozi wetu pia wanapaswa waache mara moja tabia wanayoiendekeza ya kila kukicha, kupeleka Bungeni miswada mipya ya sheria za ukandamizaji na kujiwekea kinga ya kutoshtakiwa, kama vile wao ndiyo watakaodumu milele madarakani!

Wanapaswa pia kufikiri upya, kama hatua yao ya kupeleka muswada kwa hati ya dharura, kwa viongozi kama vile kuwawekea kinga ya kutoshtakiwa, Spika wa Bunge, Waziri Mkuu na Jaji Mkuu, kama uamuzi huo ulikuwa wa busara.

Ni lazima tujue kuwa ukandamizaji unaozidi kupita kiasi hapa nchini, hautadumu milele, kwa hiyo ni vyema viongozi wetu wakatekeleza majukumu yao kwa haki na kwa mujibu wa Katiba ya nchi, kwani ndiyo kinga pekee ya kudumu, itakayowaacha salama, hata watakapotoka madarakani.
 
Naona angeacha tu aweke mifumo bora kuanzia alipoingia, unajua hizi siasa za chuki mara nyingi huwa hazijengi kwenye hizi nchi zetu za Africa.
Kwa hiyo mtu akifanya uhalifu akiwa mamlakani akitoka akachukuliwa hatua inakuwa ni siasa za chuki.!!

Je,ni haki mtu au watu fulani wawe juu ya sheria lkn wengine wawe chini ya sheria. Hiyo nchi itakuwa ni nchi ya misukule au watu. Acheni Mutharika apate stahiki yake. He deserves the gallows.
 
Wote wanaojiwekea ujinga kama huo, wakija wengine watavifuta/suspend katiba and one gets accountable!
Viongozi wetu wanapaswa watekeleze majukumu yao kwa usawa na wasiwaonee wananchi wao, kwa kutumia Jeshi la Polisi, ambalo wao viongozi wanaamini kuwa ndiyo wanaolimiliki Jeshi hilo la Polisi
 
Hiyo ni haki kabisa, kuna wajinga wengine hapa Tz eti wanajifanya wako juu ya sheria eti hawawezi kushitakiwa mahakamani lkn nawaona nawahurumia wanavyojidanganya.

Ni swala la muda tu wataburuzwa mahakamani kujibu tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo utekaji nyara watu, mauaji, ufisadi na utumiaji mbaya wa madaraka.

It's just a matter of time before these people start to bite the dust. No one can defeat justice.
 
Back
Top Bottom