Rais Mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amuondolea Kinga ya kutoshtakiwa Rais wa zamani, Peter Mutharika

Hata huyo akianza kunogewa, si ajabu yeye na genge lake watajiwekea kinga kimya kimya.

Utashangaa tu kasheria kamepenyezwa na kusainiwa.
Siyo kweli.....

Ni hulka tu ya baadhi ya watu......

Hebu jaribu ku-imagine, tokea nchi yetu irejee kwenye mfumo wa vyama vingi, ni Rais gani aliiyejitahidi sana kupeleka miswada mingi Bungeni kwa hati ya dharura na mingi ya miswada hiyo ni ya ukandamizaji wa haki za wananchi, kama siyo huyu Rais tuliyenaye hivi sasa?
 
Huyu askofu mstaafu wa Malawi Assemblies of God naona anataka kufukua makaburi_ Wale jamaa zangu wa Kanengo- cash gate products wajiandae
 
Walioenda kubadili katiba ili wasidhtakuee wajue hiyo sio dawa,dawa Ni kutenda haki ,wasipotenda haki,wakabadili sheria wasishtakiwe itafutwa ,itabadilishwa na watashtakiwa tu.
Tatizo si kutenda haki tu mkuu bali pia wanatuibia sana then wanatughiribu na milioni tano sita wanavyogawa barabarani.Ccm inapigana kubaki madarakani kulinda makaburi tu ndo maana mahandaki ya kupita reli mwenyekiti wao anaona nayo ni maendeleo
 
Hiyo sheria aliiweka yeye au ilitungwa na bunge?
Yeye kama yeye anawezaje kubadili katiba ambayo imetungwa na bunge, kwa hiyo yeye yupo juu ya katiba?
Wewe unadhani tunalo Bunge la kupinga matakwa yake Rais anayotaka yapite?

Hebu kuwa mkweli, kwa Spika wa "design" ya Ndugai,ndiyo wa kupinga sheria atakayoileta Rais na atakayotaka ipite?
 
Hiyo sheria aliiweka yeye au ilitungwa na bunge?
Yeye kama yeye anawezaje kubadili katiba ambayo imetungwa na bunge, kwa hiyo yeye yupo juu ya katiba?
Mkuu sheria siyo katiba na pia usikariri kuwa katiba za nchi zote zipo Kama hii ya kwenu msio na akili pia Lakini pia naomba nikukumbushe kwa Tanzania rais ni sehemu ya bunge
 
Cha kujifunza hapa ni kwamba viongozi wetu wa kiafrica wamejaa chuki na visasi... Angepeleka muswada bungeni iwe sheria kwa rais yeyote atakàeingia madarakani siyo kumtarget mpinzan wako tu
Ndicho alichofanya Chakwera......

Yeye kaondoa sheria inayosema Rais anayeondoka madarakani ana "impunity" ya kutoshtakiwa popote katika mahakama za nchi hiyo

Angalau inamfanya Rais ajione ni mtumishi wa Umma, ambaye anatakiwa atekeleze majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi
 
Cha kujifunza ni kuwa ama ana papara ama kuna 'kundi' lenye nguvu lililomuweka hapo na linataka afanye linavyotaka bila yeye kufikiria madhara yatakayompata na wananchi kwa ujumla. Kama na mihemuko aache...na kutulizana kwanza asubiri kimbunga kipite.
 
Hiyo sheria itakuwa retroactive?

Mutharika anaondolewa kinga kwa mambo ya kuanzia lini?
 
Hata huyo akianza kunogewa, si ajabu yeye na genge lake watajiwekea kinga kimya kimya.

Utashangaa tu kasheria kamepenyezwa na kusainiwa.
Malawi mahakama zinanguvu sana kwani wanasheria huko hawatetereki kwa kusimamia sheria, tukumbuke Rais aliyeondoka alikata rufaa kwenye kesi ya uchaguzi lakini mahakama iliitupa rufaa hiyo kwa kukosa hoja.
 
Wewe unadhani tunalo Bunge la kupinga matakwa yake Rais anayotaka yapite?

Hebu kuwa mkweli, kwa Spika wa "design" ya Ndugai,ndiyo wa kupinga sheria atakayoileta Rais na atakayotaka ipite?

Umesoma mada inatokea wapi mr?
Hapa tunazungumzia huko malawi ambako mleta mada anasema raisi kaondoa kinga kwa mtangulizi wake, na kaapishwa jana tu. Sasa je bunge lao lilikaa lini ili liondoe hiyo kinga?
Ila kwa mawazo yako kwa kuwa unajua bunge ni tanzania tu basi umesharukia mambo ya TZ.
 
Mkuu sheria siyo katiba na pia usikariri kuwa katiba za nchi zote zipo Kama hii ya kwenu msio na akili pia Lakini pia naomba nikukumbushe kwa Tanzania rais ni sehemu ya bunge

Wasio na akili ni pamoja na wewe unayetaka tujifunze mambo ya nchi nyingine wakati sisi ni sisi.
 
Malawian preacher Lazarus Chakwera has been sworn in as president after beating the incumbent Peter Mutharika in rerun elections in the southern African nation.
 
31 May 2020
Blantyre, Malawi.

Times Special with Dr Lazarus Chakwera - 31 May 2020


Source : Times Media Group
 
Aisee huyu sasa anatakiwa kuombewa ulinzi wasije muondoa kwenye kiti kabla ya muda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina neno zaidi ya kusema huyu rais kakurupuka vibaya mno. Huwezi kuja mbiombio ndani ya masaa 24 unafumua mfumo kwa ghafla hivyo, hiyo ni nchi wala sio kama chama cha mpira. Nchi ina systems na hazibadiliki ghafla bali zinabadilika taratibu kuachana na mazoea mabovu yaliyokuwepo.
China alipoingia Deng Xiaoping alikuwa anapinga ujinga uliofanywa na kina Mao Zedong lakini hakufanya haraka hivyo, USSR alipoingia Nikita Kruschev alijipanga kabla ya kuanza kumpinga Stalin ambaye alikuwa ashakufa.
Ni kama vile ana kisirani na kisasi, kama vile kaja kukomoa mtu. Mabadiliko hayaji kama mapinduzi yanatakiwa kuja hatua kwa hatua.
 
15 April 2019
Dr Lazarus Chakwera shares his story and the 2019 elections in Malawi
15 April 2019
Dr Lazarus Chakwera is one of the top contesters in the 2019 presidential elections in Malawi. He shares why he wants to be president, and his vision for Malawi and indeed all of Africa.
Source : Chims Talk Africa
 
20 Mar 2019

Part 1 : Saulos Chilima and the Elections in Malawi - Straight Talk Africa

20 Mar 2019
In the episode of Straight Talk Africa host Shaka Ssali talks to Saulos Chilima Vice President of Malawi, who is also a presidential candidate representing the opposition group, the United Transformation Movement, and is challenging incumbent President, Arthur Peter Mutharika. Shaka is joined by political analyst Alex Chanthunya to talk about the elections in Malawi in May.

Source : VOA Africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…