Rais Mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amuondolea Kinga ya kutoshtakiwa Rais wa zamani, Peter Mutharika

Peter Mutharika akiishangilia Tanzania pamoja na Magufuli

31 Jan 2017
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli akikumbatiana na Rais wa Malawi Prof. Peter Mutharika ambao wote wamekutana katika mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Source : Global TV online

10 Jun 2020
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akizungumza bungeni alipokuwa akichangia muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali (Na 3) wa mwaka 2020, jijini Dodoma.
 
Kama ni MFUMO uliojaa UOZO mwanzo mwisho kwanini AUKUMBATIE? [emoji15][emoji15][emoji15]
Kama aliahidi KUUFUMUA ni lazima ATIMIZE KAULI yake tena BILA KUCHELEWA.
Kwahiyo Malawi kila Rais anayeingia anatunga sheria na kubadili sheria muda wowote anaojisikia. Sasa kesho akitangaza wote waabudu dini yake nani atapinga.
 
Sina neno zaidi ya kusema huyu rais kakurupuka vibaya mno. Huwezi kuja mbiombio ndani ya masaa 24 unafumua mfumo kwa ghafla hivyo, hiyo ni nchi wala sio kama chama cha mpira. Nchi ina systems na hazibadiliki ghafla bali zinabadilika taratibu kuachana na mazoea mabovu yaliyokuwepo.
China alipoingia Deng Xiaoping alikuwa anapinga ujinga uliofanywa na kina Mao Zedong lakini hakufanya haraka hivyo, USSR alipoingia Nikita Kruschev alijipanga kabla ya kuanza kumpinga Stalin ambaye alikuwa ashakufa.
Ni kama vile ana kisirani na kisasi, kama vile kaja kukomoa mtu. Mabadiliko hayaji kama mapinduzi yanatakiwa kuja hatua kwa hatua.
Patrice Lumumba
 
Wapi nilipoandika hivyo? Kama sheria zimekaa UOZO na MADUDU kwanini ZIKUMBATIWE badala ya KUFUTWA!?
Kwahiyo Malawi kila Rais anayeingia anatunga sheria na kubadili sheria muda wowote anaojisikia. Sasa kesho akitangaza wote waabudu dini yake nani atapinga.
 
KIFUNGU cha 91 cha katiba ya malawi ndicho kinazuia raisi kushitakiwa humu ujue unaongea na watu wenye akili zao sio wajinga wajinga

Kifungu hicho hapo cha katiba yao ambacho huyo raisi mpya WA MALAWI anataka kujaribu kukivunja hana ubavu huo anataka kuchezea katiba kifungu hicho hapo

91. Immunity
1. No person holding the office of President or performing the functions of
President may be sued in any civil proceedings but the office of President shall
not be immune to orders of the courts concerning rights and duties under this
Constitution.
2. No person holding the office of President shall be charged with any criminal
offence in any court during his term of office.
3. After a person has vacated the office of President, he or she shall not be
personally liable for acts done in an official capacity during his or her term of
office but shall not otherwise be immune.
Wewe ni mwanasheria wa wapi? Ndio huko mnapopaitaga lumumba sijui?

Ndio wamekuajiri hapo?

Immunity ya Rais wa malawi sio absolute!

Anaweza kushitakiwa katika makosa ambayo aliyatenda nje ya majukumu yake ya urais (official capacity).
 
Tumepokea taarifa kutoka Malawi, kuwa kiongozi mpya aliyechaguliwa kwa kura nyingi katika kura za marejeo, Lazarus Chakwera, katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki, ndani ya saa 24, tokea aapishwe, ameondoa kinga ya kutoshtakiwa, aliyokuwa amejiwekea, kiongozi anayeondoka madarakani, Peter Mutharika.

Tunajifunza nini kwa hatua hiyo iliyochukuliwa na kiongozi huyo mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera?

Kama Taifa tunachopaswa kujifunza, ni kuona uongozi ni kama dhamana ambayo tumepewa na wananchi, ambapo tunapaswa tujinyenyekeze kwa wananchi wote na tuwatumikie kwa usawa, hao wananchi waliotupa dhamana hiyo tuliyo nayo na tunapaswa tutekeleze majukumu yetu, kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, bila kuwaonea raia kwa kutumia vyombo vya dola, ambavyo tunaamini kuwa sisi ndiyo tunaovimiliki.

Viongozi wetu pia wanapaswa waache mara moja tabia wanayoiendekeza ya kila kukicha, kupeleka Bungeni miswada mipya ya sheria za ukandamizaji na kujiwekea kinga ya kutoshtakiwa, kama vile wao ndiyo watakaodumu milele madarakani!

Wanapaswa pia kufikiri upya, kama hatua yao ya kupeleka muswada kwa hati ya dharura, kwa viongozi kama vile kuwawekea kinga ya kutoshtakiwa, Spika wa Bunge, Waziri Mkuu na Jaji Mkuu, kama uamuzi huo ulikuwa wa busara.

Ni lazima tujue kuwa ukandamizaji unaozidi kupita kiasi hapa nchini, hautadumu milele, kwa hiyo ni vyema viongozi wetu wakatekeleza majukumu yao kwa haki na kwa mujibu wa Katiba ya nchi, kwani ndiyo kinga pekee ya kudumu, itakayowaacha salama, hata watakapotoka madarakani.
Na yeye baadae atajiwekea hiyo kinga...
 
Mtu aliyestaafu anashtakiwa
Chakwera ametoa tangazo la hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mutharika kwani katiba haitoa kinga kwa makosa binafsi kama rushwa nk
Chakwera amecheza na mind za wamalawi ndiyo maana yeye anakinga kwa masuala ya kiofisi
 
Hapo runajifunza visasi, ambavyo na yeye hatakuwa smart 100% kwahiyo anayefuta atakula kichwa

Mandela alikuwa KIONGOZI
Over
 
Na yeye baadae atajiwekea hiyo kinga...
Hatajiwekea.................

Ikiwa unafanya kazi yako, kwa mujibu wa Katiba na kwa kutumia haki kwa wananchi wako wote, ni kwanini ujiwekee kinga ya kutoshtakiwa?
 
Chiluba alimfanyia zangwe Kaunda lakini kilichompata baadae au mmesahau
Hata huyo akianza kunogewa, si ajabu yeye na genge lake watajiwekea kinga kimya kimya.

Utashangaa tu kasheria kamepenyezwa na kusainiwa.
lu
 
Tumepokea taarifa kutoka Malawi, kuwa kiongozi mpya aliyechaguliwa kwa kura nyingi katika kura za marejeo, Lazarus Chakwera, katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki, ndani ya saa 24, tokea aapishwe, ameondoa kinga ya kutoshtakiwa, aliyokuwa amejiwekea, kiongozi anayeondoka madarakani, Peter Mutharika.

Tunajifunza nini kwa hatua hiyo iliyochukuliwa na kiongozi huyo mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera?

Kama Taifa tunachopaswa kujifunza, ni kuona uongozi ni kama dhamana ambayo tumepewa na wananchi, ambapo tunapaswa tujinyenyekeze kwa wananchi wote na tuwatumikie kwa usawa, hao wananchi waliotupa dhamana hiyo tuliyo nayo na tunapaswa tutekeleze majukumu yetu, kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, bila kuwaonea raia kwa kutumia vyombo vya dola, ambavyo tunaamini kuwa sisi ndiyo tunaovimiliki.

Viongozi wetu pia wanapaswa waache mara moja tabia wanayoiendekeza ya kila kukicha, kupeleka Bungeni miswada mipya ya sheria za ukandamizaji na kujiwekea kinga ya kutoshtakiwa, kama vile wao ndiyo watakaodumu milele madarakani!

Wanapaswa pia kufikiri upya, kama hatua yao ya kupeleka muswada kwa hati ya dharura, kwa viongozi kama vile kuwawekea kinga ya kutoshtakiwa, Spika wa Bunge, Waziri Mkuu na Jaji Mkuu, kama uamuzi huo ulikuwa wa busara.

Ni lazima tujue kuwa ukandamizaji unaozidi kupita kiasi hapa nchini, hautadumu milele, kwa hiyo ni vyema viongozi wetu wakatekeleza majukumu yao kwa haki na kwa mujibu wa Katiba ya nchi, kwani ndiyo kinga pekee ya kudumu, itakayowaacha salama, hata watakapotoka madarakani.

Kama mbwai na iwe mbwai.
 
Tumejifunza kuwa wananchi wa mataifa yote ya Afarika wanatamani kumpata Rais kama Mh .Magufuli kama Vile Kwa miaka kumia iliyopita tangu 2010 Tanzania ilivyohangaika kumpata Rais atakaye wadhibiti wahujumu uchumi na wezi wa Mali za umma na wanasiasa wanaotumia siasa kwa Manufaa yao kama Mpigaji Mkuu na dikteta kivuli Mbowe aliyebadili katiba ya Chama Chake na kuondoa Ukomo wa nafasi ya Uenyekiti na sasa ameingia kwenye rikodi ya akina Lipumba ,Mrema ,Cheyo n.k.

Haina Ubishi ,Afrika na Dunia Nzima chaguzi nyingi waliopo madarakani wataangushwa vibaya kwa sababu ya kushindwa kuwatetea Wanyonge na kuendekeza ulafi na wizi na ubinafsi na kupuuza maslahi ya umma. Kila nchi inatamani kuwa na Rais kama Magufuli. Na Tanzania ndio tulitangulia kumpata mana watu waliomba sana kumpata hasa wapinzani. Magufuli ni zawadi kwa wanyonge duniani. Marais wote wezi na vibaraka wa Mabeberu Afrika wajiandae na vyama vyao.

Leo hii watanzania hawaoni umuhimu wa kuandamana mana wanaona uzalendo. Ndio maana hata Mungu ameondo roho ya maandamano kwenye nchi yetu mana hakuna haja ya kuwepo .
Siku Magufuli atakapoacha kuwakemea wezi,wahujumu uchumi ,wazinzi kama DAS yule, Walevi kama waziri yule aliyelewa bungeni wakati wa bajeti na Msemaji yule wa kambi Rasmi, Waporaji wa Mali za wajane, uuzwaji wa ardhi Mara mbili mbili kwa magobachori, uvuvi haramu,uwindaji haramu,kusafirisha twiga na tembo ,kuwaacha wenye vyeti feki na wanaotumia Ofisi za umma kujilimbikizia Mali huku wakizuia haki za wengine hapo ndipo ile roho ya maandamano itakaporudi Tanzania na kuwaingia watu bila kupanga wala kulazimishwa.

Kwa sasa Kwa Kweli hatuoni cha kujifunza Malawi zaidi ya kuchagua viongozi wazalendo.

Kwenye uchaguzi ujao Tanzania Magufuli atashinda japo panaweza kutokea Washindani wake wenye uzalendo na wasio na makandokando. Kwa sasa hatuoni kwa nini tusimchague Magufuli akaendelea tena mpaka 2035.
Mpaka wabunge wa Upinzani watakapokuwa na idadi ya kutosha kuweza kutupa Katiba Bora na sheria bora zaidi. Kwa sasa Kwa wingi wa wabunge wa CCM pakitokea Rais mpigaji nchi itayumba sana. Anayeweza kupambana na wezi kwa sasa ni Magufuli (wezi ambao wengi wao wapo CCM japo pia kuna akina Mbowe na Genge lake ndani ya Chadema na vyama vingine )
 
Back
Top Bottom