Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Tayari wanayo, huu mwaka wa 6 au wa 7 wapo Mbeya. Ila wanatumia facilities za hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya.

Ili kujenga majengo yao pqmoja na hospitali, wanahitaji eneo kubwa zaidi. Wamezikataa ekari 50 kwamba hazitoshi.

Graduates wa kwanza wa Udaktari wa UDSM Mbeya College of Health and Allied Sciences wamehitimu mwaka jana, mahafali ya leo walikua ni batch ya pili kuhitimu.
Muhimbili wanatumia balaa
 
Kulipa fidia ili kupisha miradi ya serikali ni kweli na ndiyo utendaji haki, ila siyo uamuzi mzuri wa serikali kutumia raslimali zake kulipa fidia ili kujenga chuo ambacho kinaweza kujengwa sehemu nyingine bila kulipa fidia. Halihii ni tofauti kabisa na ujenzi wa miundo mbinu kama barabara na reli ambayo topographic conditions zinakuwa zinataka ipite eneo fulani ambalo tayari linatumiwa na raia. Ujenzi wa zahanati na vituo vya afya unaweza kusababisha baadhi ya raia wakahamishwa kusudi kuziweka huduma hizo ziwe karibu na wananchi wengi wanaolengwa na huduma hizo. Chuo kikuu hakilengi watu wa Mbeya tu, kinaweza kuwa popote, na hivyo kulipa watu fidia kusudia maeneo yao yatumiwe na chuo kikuu ni matumizi mabaya ya raslimali za serikali.
Chuo kikuu cha mambo ya tiba ni lazima kiwe na hospitali ambayo hiyo hospitali inatoa huduma kwa watu.

Sasa unawezaje kujenga taasisi hizo mbili bila kuzingatia suitability na accessibility ya eneo husika ?

Yaani ujiokotee eneo hata la mabondeni huko kwa sababu haulipi watu fidia, then ukajenge chuo ?
 
Rais wa awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amekataa kupokea ekari 50 ambazo Serikali ya Mkoa wa Mbeya imezitoa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu cha Dar es Saalam kampasi ya Mbeya na kutaka wapewe eneo lenye ukubwa wa ekari 500 au 1,000.

Kikwete amesema kama mkoa huo hautawapa eneo wanalolihitaji watahamishia chuo hicho katika mkoa mwingine ambao utakuwa tayari kuwapa ardhi yenye ukubwa wanaouhitaji.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi, Novemba 27,2021 wakati wa mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Afya na Sayansi Shirikishi kampasi ya Mbeya yaliyofanyika jijini hapa.

Kikwete amesema hawawezi kukubali kupokea ekari 50 walizopewa kwakuwa chuo hicho kina hadhi kubwa hivyo wanahitaji ekari 500 hadi 1000 kwa ajili ya kujenga hosteli, makazi ya wahadhiri, wafanyakazi na hospitali.

Kauli hiyo ameitoa baada ya hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Mwanaidi Mtanda kusema kuwa ukosefu wa eneo kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili licha ya kuwasilisha maombi yao kwa Serikali ya mkoa tangu mwaka jana.

"Ingawa simuoni hapa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (Juma Homera) lakini naamini viongozi wa Mkoa watamfikishia ujumbe, tunaomba kiwanja tujenge chuo cha kisasa na hili lipewe kipaumbele" amesema Mwanaidi.

Mara baada ya hotuba hiyo, Kikwete amesema hawawezi kukubali kupokea ekari 50 walizopewa kwakuwa hazikidhi mahitaji yao

"Hii siyo sekondari kupewa ekari 50, tunataka eneo kubwa la ekari 500 hadi 1000 tenga hata kule Forest, mkishindwa tunahamia mkoa mwingine utakaoweza kutoa eneo kubwa, huu ni ujumbe kwa nyie viongozi" amesema Kikwete.
Hiyo Ardhi Mbeya hawezi kuipata maana wilaya ambazo zina Ardhi kidogo ya akiba ni Chunya na Mbarali lakini 500-1000 too much hata UDSM main campus hawana eneo la hivyo
 
Chuo kikuu cha mambo ya tiba ni lazima kiwe na hospitali ambayo hiyo hospitali inatoa huduma kwa watu.

Sasa unawezaje kujenga taasisi hizo mbili bila kuzingatia suitability na accessibility ya eneo husika ?

Yaani ujiokotee eneo hata la mabondeni huko kwa sababu haulipi watu fidia, then ukajenge chuo ?
University Hospital siyo lazima iwe main campus. Mbeya University wanaweza kuwa University Hospital sehemu moja na main campus sehemu nyingine. Infact vyo vingi vyenye University Hospitals zinazoheshimika huwa hospitali zao ziko off campus kabisa. Hutaki magari ya ambulance yanayopiga ving'ora yawe yanapita kupeleka wagongwa emmergency room na kusababisha makelele madarasani wakati wa lecture.
 
Huko watani zangu Mna majanga mengi, mafuriko,ma ukimwi, matetemeko, mavita ya Kagera n.k

Mtakitia Nuksi Chuo chetu pendwa kilichofanikiwa kutoa Ma Rais wawili wa Jamhuri ya Tz, Rais mmoja wa Uganda, Rais wa Sudan kusini n.k hadi sasa!
Waje Kagera eneo lipo tutawapa.
 
Hiyo Ardhi Mbeya hawezi kuipata maana wilaya ambazo zina Ardhi kidogo ya akiba ni Chunya na Mbarali lakini 500-1000 too much hata UDSM main campus hawana eneo la hivyo
Mmmh, ya kweli hayo mkuu... ?
Yaani Mbeya ikose ekari 500 hadi iende huko wilayani ?
Au wewe unazungumzia HEKTA 500 ?
 
Mmmh, ya kweli hayo mkuu... ?
Yaani Mbeya ikose ekari 500 hadi iende huko wilayani ?
Au wewe unazungumzia HEKTA 500 ?
Heka 500-1000 Mbeya mjini atazipata wapi? Wilaya ya Mbeya imezungukwa na milima maeneo ya tambarare ni machache sana na mengi yanamashamba au majumba ya watu
 
University Hospital siyo lazima iwe main campus. Mbeya University wanaweza kuwa University Hospital sehemu moja na main campus sehemu nyingine. Infact vyo vingi vyenye University Hospitals zinazoheshimika huwa hospitali zao ziko off campus kabisa. Hutaki magari ya ambulance yanayopiga ving'ora yawe yanapita kupeleka wagongwa emmergency room na kusababisha makelele madarasani wakati wa lecture.
What is the essence then ?
Yaani unafanya new project, halafu unajenga chuo sehemu moja na hospitali unaijenga sehemu nyingine ya mbali ?
Hii umewahi kuiona wapi mkuu ?

Halafu ambulance inapiga kelele inapopita barabarani huko, ambulance kamwe haipigi king'ora ikiwa kwenye mazingira ya hospitali. Never.
 
Huko watani zangu Mna majanga mengi, mafuriko,ma ukimwi, matetemeko, mavita ya Kagera n.k

Mtakitia Nuksi Chuo chetu pendwa kilichofanikiwa kutoa Ma Rais wawili wa Jamhuri ya Tz, Rais mmoja wa Uganda, Rais wa Sudan kusini n.k hadi sasa!
Majanga yapo ili kukujenga ukomae na ujue kupambana, chuo chenyewe kimeshakuwa na nuksi hadi sasa.
 
Tayari wanayo, huu mwaka wa 6 au wa 7 wapo Mbeya. Ila wanatumia facilities za hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya.

Ili kujenga majengo yao pqmoja na hospitali, wanahitaji eneo kubwa zaidi. Wamezikataa ekari 50 kwamba hazitoshi.

Graduates wa kwanza wa Udaktari wa UDSM Mbeya College of Health and Allied Sciences wamehitimu mwaka jana, mahafali ya leo walikua ni batch ya pili kuhitimu.
Toeni eneo sasa mjenge tawi la mbeya mnangoja nini?
 
Toeni eneo sasa mjenge tawi la mbeya mnangoja nini?
Tutatoa mkuu. Chuo ni jambo jema sana. Tutatoa, hatuwezi kuruhusu hii fursa ipotee kwenda kwenye mkoa mwingine (ambayo nayo ni ngumu sana, sema ni vile Mkwere kaamua tu kupiga mkwara)
 
Tutatoa mkuu. Chuo ni jambo jema sana. Tutatoa, hatuwezi kuruhusu hii fursa ipotee kwenda kwenye mkoa mwingine (ambayo nayo ni ngumu sana, sema ni vile Mkwere kaamua tu kupiga mkwara)
Hakuna mkwara hapo mkizingua tunahamisha hii nchi ina maeneo mengi tuu yanahitaji kujengewa chuo kikuu.
 
Then tell me where in Mbeya District you can get
222+ to 444+ Hectares of Land?
Mimi na wewe ni lazima kwanza tukubaliane tunajadili nini hapa.

1. Ekari (Acres) au Hekta (Hectares)
2. Ni lazima eneo hilo liwe tambarare and unoccupied ?
 
Waende wakajenge Dodoma huko ndo Kuna miekari ,mbeya ni jiji la viwanda na ni mkoa wa kilimo,unalisha takribani 75% ya mikoa yote tz,tuwape miekari 1000,halafu tulime wapi ,kwanza hiyo UDSM kwetu si kipaumbele labda wangekuwa SUA at least tungeweza kufikilia ,UDSM ni chuo Cha mashalobaro na sistaduuz ,ekari 50 hamtaki Basi,nendeni kwingine,
 
Mimi na wewe ni lazima kwanza tukubaliane tunajadili nini hapa.

1. Ekari (Acres) au Hekta (Hectares)
2. Ni lazima eneo hilo liwe tambarare and unoccupied ?
Nimezibadilisha tu kubwa hekta aya ngoja nianzike heka 500-1000 niambie katika wilaya ya Mbeya ni eneo gani anaweza kupata? Lisiwe ni la misitu ya TFS nk
 
Back
Top Bottom