Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ahudhuria msiba wa Gabriel Ndugulile, Baba wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni

Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ahudhuria msiba wa Gabriel Ndugulile, Baba wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni

ndanda masasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2014
Posts
772
Reaction score
1,177
1.jpg
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete alipowasili eneo la msiba nyumbani kwa marehemu mzee Gabriel Ndugulile Ferry Kigamboni Jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia kwa msiba huo.

2.jpg

Ndugu Dkt. Ndugulile akitoa shukrani kwa watu wote kuhudhuria na kutoa salamu za pole na rambirambi kwa msiba uliowapata kuondokewa na Baba yao kipenzi marehemu Mzee Gabriel Ndugulile.

Pia ametoa shukrani kwa niaba ya familia kwa Mhe.Rais JP.Magufuli kuwapatia ndege moja ya serikali kasafiria kuelekea Mkoani Tabora kwa mazishi.

2.jpg
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe.Sarah Msafiri akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Gabriel Ndugulile kwa niaba ya Serikali nzima ya Manispaa ya Kigamboni.

Mhe. Faustine Ndugulile Mbunge wa Jimbo la Kigamboni alifiwa na Baba Mzazi Gabriel S. Ndugulile Jumamos 18.07.2020 Asubuhi. Msiba upo Nyumbani Kwake Ferry, Kigamboni, Dar Es Salaam
 
Kumbe mzee alichomoka na walinzi wake wale wale tokea akiwa madarakani?

Pole kwa mbunge na wanakigamboni kwa ujumla kwa msiba unaomhusu muwakilishi wao.

Siasa ikae pembeni kidogo mambo mengine yaendelee. Kuna watu watachukia kwanini kaenda kwenye huu msiba.
 
Back
Top Bottom