Rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema iwapo Watanzania wangekuwa na ari ya kujituma kama wanavyofanya Wachaga, nchi ingekuwa mbali kimaendeleo

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
#Repost @mwananchi_official
——
Rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema iwapo Watanzania wangekuwa na ari ya kujituma kama wanavyofanya Wachaga, nchi ingekuwa mbali kwa maendeleo.

Kikwete ametoa sifa hizo kwa Wachaga, huku akiyahusisha baadhi ya makundi ya watu nchini, ambayo hata kulima kwa ajili ya mlo wao wanalazimika kusukumwa.

Kikwete ametoa kauli hiyo jana Jumatatu, Desemba 23, 2024 alipowaongoza maelfu ya wanariadha katika mbio za Rombo Marathon zilizofanyika katika Hifadhi ya Msitu wa Rongai wilayani Rombo, Kilimanjaro.

"Kuna maeneo hapa nchini watu hata kujilimia chakula chao inabidi usukumane nao, lakini hakuna Mchaga utakayemsukuma kwa kujiletea maendeleo, na hiyo ndio siri, uzuri Wachaga hawasahau kwao kila mwaka wanakwenda kuhesabiwa," amesema.

Kwa mujibu wa Kikwete, mtindo wa kwenda nyumbani kila mwisho wa mwaka unajenga ushawishi kwa wengine kuonyesha hatua za maendeleo walizopiga.

"Niwapongeze wananchi wa Rombo kwa moyo wenu wa kujituma na kujiletea maendeleo, mimi nimefanya kazi wilayani, mkoani, wizarani na katika ngazi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi yetu, Watanzania wote wangekuwa na ari ya wachaga nchi yetu ingepiga hatua kubwa, endeleeni na moyo huo," amesema.

(Imeandikwa na Janeth Joseph)
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
 
Hivi huyu mzee anatuonaje Watanzania?

Sisi siyo wapumbavu
 
Kama mikoa ya Manyara, Arusha Kilimanjaro na Tanga kaskazin yangekuwa nchi inayojitegemea, ndio ingekuwa first world country kusini mwa jangwa la Sahara. Kuna wavivu wanakwamisha maendeleo kiu yao ni kuiba na kula jasho la wengine na bado ni masikini. Bravo JK kwa kuwa muwazi.
 
😅😅😅yaani wabondei,wadigo na wa Arusha wavuta bangi hawa ndyo unawaongelea?
 
Wachaga walikuibia nini? kila siku kusema wachaga wezi kana kwamba huko kwenu hakuna wezi waliofungwa magerezani. Acha kuwa na wivu na chugi dhidi ya wachaga kama ule mzoga unaooza kule chattle.
Ukweli unauma sana
 
Back
Top Bottom