Rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema iwapo Watanzania wangekuwa na ari ya kujituma kama wanavyofanya Wachaga, nchi ingekuwa mbali kimaendeleo

Yuko sahihi kabisa
 
Wivu 🙄 really?
Ukweli mchungu, kuna siku niliwaza kwanini familia nyingine zipo benki kuu, bandarini, mahakamani, taasisi kubwa kubwa

Wazee wao waliotangulia waliweka nafasi kwa watu wa chini yao, sio kwa wepesi kuna gharama zake pia, maisha ya watu, kutapeli, kuumizwa, kufosi

Sasa tujiulize wazee wetu walikuwa wapi miaka hiyo...?
 
JK kwenye hili ninamwelewa,Mimi Mdigo.Yaaani ukitoa Wachaga makabila mengine yanamambo ya ajabu sana ambayo yanazima maendeleo.Mfano unyagoo et unapewaa kipaombele na jamii kuliko kujenga nyumba zaoo,kuoa hovyooo hovyooo,kuchunga ming'ombe 100 halafu nyumba ya nyasi.

NB: Kikawaida popote penye minazi hapaswi kutoka Rais wa nchi.Viva JK watu wanashambulia familia yake wakati yeye ametoa mtazamo wake ambao Hauna biasness,Mimi sio mchaka ila Jamaa wanajitambuaa sana.

Hutakuta kwa mchaga amekusanya ndugu ambaoo Hawana kazii wanamtegemea,mabinamuu mashemeji,.....
 
Huo uwazi angeenda nao mbali zaidi kwa kuwataja hao wavivu wa kutafuta kwa majina ya makabila na maeneo Kama alivyofanya kwa kuwataja wachagga.

Tunasubiri…. Na awe mkweli tupu beyond any reasonable doubt.
 
Amesahau Wasukuma,Wakinga, Waha na makabila mengine ila anakotokea (Kikwete) ukanda wa pwani Mungu aliwanyima maarifa ya kupambania maisha kutwa kucha kijiweni kuteta umbeya sio rahisi kumtofautisha mwanaume na mwanamke wa pwani kwa umbeya wote wapo frontline.
 
Kwahiyo njia zingine za halali wanazotumia watu kujitafutia chochote chao ni upuuzi?!

Material things for a plastic generation!!

Kwamba kumiliki vitu imekua ni muhimu zaidi ya utu to the extent that it doesn’t really matter how you acquire them?!

Kweli kudos kwa waChagga.
 
Material things for a plastic generation!!

Kwamba kumiliki vitu imekua ni muhimu zaidi ya utu to the extent that it doesn’t really matter how you acquire them?!
Ndio ni muhimu, utu haukupi ugali mezani, utu haulipi ada tuache siasa za kiimani, kuna watoto wamesomeshwa kwa hela za wizi ni madaktari wazuri na wanatutibu tunapona
 
Kujituma kivipi sasa,mbona watu wengi wanajituma sana au kujituma kwa kila mwisho wa mwaka kwenda makwao,tumeshawahi kujiuliza kwanini wanatumia nguvu nyingi sana kuhakikisha kuwa mwisho wa mwaka lazima warudi kwao.....
 
Huo uwazi angeenda nao mbali zaidi kwa kuwataja hao wavivu wa kutafuta kwa majina ya makabila na maeneo Kama alivyofanya kwa kuwataja wachagga.

Tunasubiri…. Na awe mkweli tupu beyond any reasonable doubt.
Mimi bila kupepesa macho naanza na Wazaramo, Wandengereko, Wamatumbi,Wangindo.. kidogo kabila lake (Wakwere) wana unafuu kuliko hao niliowataja.
 
Mabilionea Tanzania
1.Mo Dewji
2.Rostam Aziz
3.Bakhresa
4. Ghalib-GSM
Hao wote ni Asian Tanzanian.. wengi wa hawa matajiri wamerithi utajiri toka mababu zao wakati wa ukoloni , walipewa haki ya kununua mazao kutoka kwa makabwela waafrika, mkoloni alitenga madaraja ya raia kama ifuatavyo...Fist class (Europian) Second Class (Asian) na Third Class walikuwa Waafrika..Asian wamefika hapo kwa kupendelewa fursa na mkoloni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…