View attachment 365889
View attachment 365890
Museveni mara nyingine anafurahisha sana. Katika msafara wake wiki hii huko Uganda, aliusimamisha ili apokee simu muhimu sana. Akapewa kiti na ili aongee na simu, na kuwaambia askari wake wasiwasumbue watumiaji wengine wa barabara waache wapite tu, huku yeye akiwapa madereva waliopita alama ya "dole tupu!". Aliongea na simu kwa dakika 30 hivi, na wanakijiji wa sehemu hiyo walipopata habari wakaenda sehemu alipo, basi ikabidi awatolee hotuba fupi ili kuwasalimia!
Hapo alipo ni katika barabara inayounganisha Uganda na Tanzania, ambayo Museveni alihakikisha inawekwa rami hivi karibuni. Museveni, ambaye huwa anajiona ana chimbuko toka Tanzania, huwa anasisitiza sana Uganda kuwa na ujirani mwema na eneo la Tanzania mpakani na Uganda, na hata kutoa huduma toka Uganda kwa sehemu hizo. Kuna wakati aliamua umeme toka Uganda upelekwe sehemu za Tanzania zinazopakana na Uganda. Anamchukulia mama Maria Nyerere kama vile mama yake mzazi.
Kihistoria, Museveni alikimbia mauaji ya Idd Amin miaka ya 70 na kuja Tanzania, akiwa na wenzake. Nyerere aliwashauri kwamba badala ya kuingia msituni wakati huo ili kupambana na Idd Amin, waende Chuo Kikuu Dar es Salaam wakasome, wakisubiri wakati muafaka wa kurudi Uganda. Hivyo Museveni alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akiwa chini ya ulezi wa Nyerere.