Rais Mwinyi achukizwa na tabia ya viongozi kujiuzulu kimya kimya

Rais Mwinyi achukizwa na tabia ya viongozi kujiuzulu kimya kimya

Swala la wamasai kubaguliwa na wamatumbi wenzao kalizungumziaje otherwise hayo mengine awaambie hao wateule wake wakati anawateua sisi hayatuhusu.

Tunataka kujua hatma ya watanganyika wenzetu huko Zanzibar ache unafiki wake.
Ingia kwenye instagram ya azam Tv, uone tunavyofanywa wajinga. Kumbe lile tukio lilitokea miaka kadhaa iliyopita, kuna mkora kalitupia kwenye Jf kupima uwezo wetu wa kukumbuka na kufuatilia mambo! Polisi wamekanusha kuwepo kwa tukio la namna hiyo. Yericko nyerere inabidi atuombe radhi, na ikibidi akaisaidie polisi huyu!
 
Kumbe yule Waziri aliyejiuzulu kule Zenji alikurupuka bila hata wakubwa zake kujua kwamba anataka Kujiuzulu.

Sasa Dr.Mwinyi amewataka Viongozi kutoa taarifa Kwa mamlaka ya Uteuzi kabla ya kukirupukia kutangaza Kujiuzulu.

My Take
Naunga mkono hoja Kwa sababu next time hakuna mtu atakuamini tena.

====

Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Kiongozi akitaka kujiuzulu anapaswa kumpa taarifa Boss wake kwanza badala ya kukurupuka kwenda kutangaza kwenye Vyombo vya Habari huku akitoboa siri kuwa hata yeye akiwa Waziri wa Ulinzi aliwahi kumwandikia barua ya kujiuzulu Rais Mstaafu Kikwete baada ya mabomu ya Gongolamboto lakini alimwambia ile ni ajali na hana sababu ya kijiuzulu.

Akiongea leo February 1, 2024 wakati akiwaapisha Mawaziri wapya wateule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar Rais Mwinyi amesema “Suala la kujiuzulu Waziri ni suala ambalo si geni ni moja katika njia ya kuwajibika, katika Wizara kunaweza kukawa na mazingira mawili ya Waziri kujiuzulu, mazingira ya kwanza yanaweza kuwa katika Sekta yako inayoisimamia kumetokea tatizo au changamoto na wewe kama Waziri unawajibika kwa changamoto ile, si lazima uwe umeifanya wewe lakini unawajibika kwasababu wewe ndio Msimamizi wa Sekta”

“Nimekuwa nasikia kwenye mitandao kuwa Zanzibar hajawahi kujiuzulu Mtu, si kweli, wakati wa ajali ya meli kuna Waziri alijiuzulu na alijiuzulu si kwasababu alisababisha
yeye ile ajali kawajibika kwasababu ni Sekta anayoisimamia na kilichotokea ilikuwa ni uzembe na si ajali”

“Ilipotokea ajali ya mabomu kule gongo la mboto, Mimi nikiwa Waziri wa ulinzi nilipeleka ujumbe kwa Rais wangu wakati huo Mhe.Kikwete nikimtaka aliridhie nijiuzulu lakini sikukurupuka kwenda kwenye Vyombo vya Habari nikatangaza kwamba nimejiuzulu sio utaratibu, utaratibu unataka umwambie aliyekuteua akubali ndio ukatangaze kujiuzulu, Mhe.Kikwete akasema hii ni ajali huna sababu ya kujiuzulu, hakuna Mtu aliyesikia kama nilitaka kujiuzulu leo nasema hili hadharani lakini sikuwahi kulisema”

Kauli ya Rais Mwinyi inakuja siku chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohammed Said, kujitokeza kwenye Vyombo vya Habari na kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri akisema mazingira ya kutekeleza jukumu hilo yamekuwa magumu. #MillardAyoUPDATES

Kuna jambo la msingi halijatolewa ufafanuzi hapa ; mazingira gani magumu yaliyo fanya waziri ajiuzulu? Kuna maneno mengi yanasemwa kuhusu Rais Mwinyi kuhusishwa na biashara ya pombe/vilevi akishirikiana na mtoto wa marehemu Babu Ladwa!! Sasa wanasema huko Zenj toka zamanı kuna utaratibu wa kufanya biashara hiyo unaozingatia utamaduni wao.! Hussein Mwinyi na huyo mbia wake wanakiuka mazoea hayo ikiwemo dini ya kiislam!
Wanakwenda mbali zaidi na kusema Rais Mwinyi na huyu mtoto wa Ladwa ( Kumbuka baba zao walikuwa marafiki) walifanya ufisadi mkubwa walipoagiza magari ya jeshi kutoka India aina ya Ashok Leyland; wakati huo Hussein Mwinyi akiwa waziri wa ulinzi
Hawa wawili wameanza siku nyingi kufanya biashara ya vilevi na magendo yao kupitia duty free shops zilizokuwa jeshini na kupelekea Magufuli kuzifunga.
Rais Mwinyi ni mfanya biashara zaidi kuliko mwanasiasa!
 
Rais Mwinyi? Huyu wa kila Ijumaa msikiti mwengine. Na biashara ya pombe. Maajabu hayaishi.
 
Back
Top Bottom