RAIS MWINYI: Jina lako linapolomoka umaarufu kwa mradi usionatija wa MABASI

RAIS MWINYI: Jina lako linapolomoka umaarufu kwa mradi usionatija wa MABASI

The only

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
11,197
Reaction score
14,771
Baba! Baba! Baba!

Nimekuita mara tatu,hakuna mtu kajijengea jina zuri kwa marais ukiondoa Muasisi wetu karume kama wewe ,yaani Mheshimiwa umempiku mpaka Mzazi wako .Nia yako imethibitishwa hadharani wewe unaitakia mema Zanzibar ,toka ukanyage ikulu sijawahi kuona kasoro yako makuu ulofanya hata kuwaza hatukuwahi.

Umejua kubadili utamaduni wa uvivu nanuzembe vyema umesimamia mapato na matumizi kwa mkono wa chuma ninasema haya MBELE ZA MUNGU na sina haja ya uchawa maana hunijui na hutakaa unijue hivo ningeamua hata kukukosea adabu hutonipata ,ila nakiri NINAPENDA UONGOZI WAKO 100% .ILA HILI LITAKUCHAFUA

Ewe rais mwema,zanzibar hakukuwa na shida yeyote ya foleni nje ya zanzibar penyewe mjini kati huku kisongo na njia ya za jirani ambazo dawa ushaiweka mezani ikiwemo flyover na umepanua barabara nyingi za kuingia mjini na ujenzi unaendelea nakupa HEKO.

Zanzibar kabla ya uamuzi mbovu na mchafu wa haya mabasi kulikuwa na usafiri wa uhakika bei tsh 500 kwenda almost kokote .ulikuwa nanuwezo wa kutoka buyu hadi fuoni kwa dakika 25 .Mheshimiwa mm sitaki UONGO fanya utafiti huru .leo kutoka buyu wala sitaji fuoni hadi kijangwani tu si chini ya saa moja na nusu hadi masaa matatu.

Kimsingi ukianza safari kutokea kijanjwani kuelekea buyu mda mmoja na mtu anaeanza safari dar kuelekea morogoro atawahi mapema wa morogoro .

Ni dhahili mradi una muonekano wa kisasa ila umeirudisha zanzibar mwaka 1987 kiusafiri ,wapiga kura wako wanatembea kwa miguu sasa hivi kuliko nyakati yeyote tangu utawala wa salmini .sababu walioleta huu mradi ni watu wasio na fikra wenye kukopi dareslamu bila kuijua zanzibar.kifedha wananufaika ila kinachotolewa sadaka JINA LAKO JEMA ULILOJIJENGEA .Watu wanaamini una 10% kwenye hilo wakati mm nauhakika huhusiki ni ulijua itaboresha zanzibar.

NINI KIFANYIKE !
1.Rejesha daladala kwanza watu waheme kwanza uwatue mzigo ,nawajua vijana wengi walioamua kutembea kwa miguu kuepuka kero za hiyo mibasi .
2 .Weka usimamizi mpya toa wote walioleta mazoea ya nyuma ukibidi toa watu wakali bara.unda team smart na strong .
3 .Team hiyo ije na namna ya kusimamia yafuatayo
a) Daladala zijiendeshe kwa kupewa kibali cha miezi mitatu mitatu tu .
b) ili kupata kibali kondakta na dereva watavaa yuniform itayoshonwa na mzabuni wa team hiyo tu ,shati jeupe suluali bluu na tai juu.
C) hakuna gari itapewa kibali bila kuthibitishwa ina air condition inayofanya kazi
D) Gari zote ili zipewe kibari kitachoanza kutolewa baada ya miezi 2 toka sasa ,ikarabati interior condition kwa gereji zilizopitishwa na team hiyo ambazo zimepewa vigezo vinavyopaswa .matengenezo mengine wanaruhusiwa yafanya popote kulinda riziki ya gereji ndogondogo ila quality ya interior ikiwemo floor carpet ,seat sofa,paa carpet dashbord safi itasimamiwa na gereji tambuliwa tuu

Ewe mkuu natumaini yupo raia mwema wa karibu ataejua namna ya kukupenyezea huu ujumbe ,najua ni ngumu maana washanunua mabasi ila kila usiku mmoja usioamua kuwatoa kuna wazanzibari si chini ya 10000 wanabidi aidha wachelewe kazini ,wafukuzwe kazi,au watembee kwa miguu juzi nimeona mbibi wa miaka kama 70 nae anatembea kwa miguu pale matrector mbwen
 
Back
Top Bottom