Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Nina laani kwa nguvu zote kitendo cha vurugu za mgambo na watu wa jamii ya kimasai kwakupigana hadharani, Nina laani Masai kushambulia Mgambo, Nina laani kwa nguvu kubwa Mgambo wa Zanzibar kushanbulia watu wa jamii ya kimasai! Jambo hili halikubaliki kwa mjibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazokataza kupigana hadharani au kificho.
Lakini naomba nitofautiane na hatua iliyochukuliwa na serikali ya Zanzibar, Amri kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime/visu vyao, Ni Kauli Haramu na ya kibaguzi inayohatarisha muungano wa Tangabyika na Zanzibar.
Ifahamike kuwa Fimbo na Sime kwa Jamii za kimasai ni sehemu ya “vazi lao la asili”, ni Sehemu ya utamaduni wao, Ni Identity yao, na hivyo kujaribu kwa aina yoyote kuondoa kimoja wapo katika hivyo vinavyokuwa ndani ya mwili wa Masai ni kutangaza kuwafukuza Wamasi Zanzibar, Hili ni tangazo la kijinga limekurupukwa na mamlaka za Zanzibar!
Kwamiaka yote tangu kabla ya uhuru hadi leo, Jamii za Wamasai wapo Zanzibar na utamaduni wao wa visu/Sime na Fimbo, hakujawahi kuwa hatari kwa raia yoyote, Kwanini iwe leo baada ya Masai kujihami waliposhambuliwa na mgambo wa mji? Serikali ya Rais @dr.hmwinyi itafute jawabu la kumaliza mzozo huu sio kufunika kwakuwafukuza Wamasai, Tatizo liko kwa mamlaka za jiji, Tatizo liko kwa Wakuu wa Mikoa, na mamlaka zingine za jiji.
Unawazuia Wamasai wasibebe fimbo unataka Wabebe Vikapu vya Nazi na vigemeo vya Litembo? Unataka wabebe Usinga? Unataka wabebe karafuu? Noooo nooo tukatae unyanyasaji huu kwa jamii ya kimasai! Ukamilifu wa Masai ni fimbo na sime. Sasa unaka awe na shuka tu kama dera?
Kesho yataibuka Bara Wapemba watashambuliwa, Je serikali iweke amri wapemba wasizaliane kwa Wingi Bara ambao ni sehemu ya utamaduni wao? Nooo Nooo! Tukatae ubaguzi huu.
Mh Rais @dr.hmwinyi ili kunusuri maafa zaidi na kuoondoa hii taswira mbaya ya ubaguzi iliyotengenezwa na mamlaka za mji hapo Unguja, Ninakuomba na kukusihi Mh Rais, tengua hii kauli ya kibaguzi, Haifai kutolewa na kiongozi wa serikali katika ulimwengu wa leo! Madhara yake ni makubwa zaidi mbeleni.
Serikali ijifunze kutatua migogo kwa hekima na busara, Majibu ya hasira ya kiserikali yanaweza kuleta maafa zaidi kuliko kutatua, Nimeisikiliza kauli ikitolewa na yule kiongozi wa mjinibZanzibar (Unguja) ni wazi alitawaliwa na ghadhabu zaidi kuliko hekima ya kiuongozi, Amewahukumu Wamasai bila kujaribu kujua undani na kutafuta jawabu, Badala yake ametafuta jibu ambalo ni la hovyo zaidi!,
Nimesikitika sana kwa kauli hii ya serikali ya Zanzibar katika zama hizi za utandawazi na utandaridhi! Utengamano wa taifa letu ni muhimu kuliko hizi chuki zinazokolezwa na namlaka za nchi!
Na Yericko Nyerere