Rais Mwinyi, tengua Amri haramu ya kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime Zanzibar. Inahatarisha Muungano!

Rais Mwinyi, tengua Amri haramu ya kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime Zanzibar. Inahatarisha Muungano!

Ukimsikiliza ni chuki tu za kibaguzi. Eti kama wanataka kufanya biashara wafungue maduka na wasibebe sime wala marungu. Hiv nchi hii wamasai wamewakosea nini. Maana porin kwao wamefukuzwa na huku mjin wanakojitafuta hawatakiwi. Mnataka wafanye nini waende wapi.
Zanzibar kule ni utalii per se
Na wamasai kujaa sidhan kama mapanga na mafimbo yana umuhimu
Silaha hizo kiasil mazingira ya porin ndio lazima uwe nayo mim mwenyewe hapa endulen natèmbea na sime ingawa sio mmsai.unakuta siku ya mnada una ham na nyama unavaa sime unatembea kule mapori meng
Kwa zanzibar hakuna mapori mapanga mafimbo ya nini?
 
We mwenyewe ndio unajenga hoja ktk msingi wa ubaguzi. Zanzibar nayo ina utamaduni wake, ukifika Roma fanya km waRoma, wakiinama nawe inama. Pili we huwajui vizuri wamasai, hizo sime na fimbo za nini huko mjini Zanzibar? Sime na fimbo zina mantiki kule porini, eti wametumia kujihami. Ni kwamba hizo ndiyo silaha wanazotegemea ukitofautiana nao. Wapigwe marufuku vinginevyo warudi kule porini kwao.
Na nyie wazanzibar mrudi kwenu haraka hatuwataki huku
 
Zanzibar kule ni utalii per se
Na wamasai kujaa sidhan kama mapanga na mafimbo yana umuhimu
Silaha hizo kiasil mazingira ya porin ndio lazima uwe nayo mim mwenyewe hapa endulen natèmbea na sime ingawa sio mmsai.unakuta siku ya mnada una ham na nyama unavaa sime unatembea kule mapori meng
Kwa zanzibar hakuna mapori mapanga mafimbo ya nini?
Ule ni utamaduni wa watu, mbona nyie mnakuja na kanzu zenu huku kwetu na wakati sisi ni wakristo?
 
Zanzibar ina sheria zake, usiingilie !! wamasai wazifuate ama warudi kuchunga mifugo bara.

Bara ni kwajili ya sheria za muungano tu, Zanzibar kuna sheria za Zanzibar na vijisheria vya upande wapili wa muungano.
Ndiyo hatutaki sasa, muungano fake uvunjwe kila upande ubaki kwao
 
Ukimsikiliza ni chuki tu za kibaguzi. Eti kama wanataka kufanya biashara wafungue maduka na wasibebe sime wala marungu. Hiv nchi hii wamasai wamewakosea nini. Maana porin kwao wamefukuzwa na huku mjin wanakojitafuta hawatakiwi. Mnataka wafanye nini waende wapi.
Huyu maza amejificha kwenye dini lakini ni mbaguzi haswa, tukisema huwa mnaona tunawachukia wazanzibar lakini ndiyo tabia zao
 
Serikali ya mapinduzi inapotoshwa kwa hili la wamasai. Kuna chuki kubwa za kidini dhidi ya jamii Za watanganyika
Ila kwa ajili ya siasa watakanusha , wafute tangazo lao kimyakimya dhidi ya wamasai.
Na wazanzibar nao wasije huku bara hatuwataki na kanzu zao
 
Zanzibar kule ni utalii per se
Na wamasai kujaa sidhan kama mapanga na mafimbo yana umuhimu
Silaha hizo kiasil mazingira ya porin ndio lazima uwe nayo mim mwenyewe hapa endulen natèmbea na sime ingawa sio mmsai.unakuta siku ya mnada una ham na nyama unavaa sime unatembea kule mapori meng
Kwa zanzibar hakuna mapori mapanga mafimbo ya nini?
Bro mmasai mwenyewe ni kivutio cha kitalii. The way alivyovyaa tu tembea nchi za watu ndio utajua nachokuambia. Wazungu wanataka kitu unique mzee sio aje aone sawa na kwao
 
Mbona ukeketaji watu wameelimishwa, wakaacha,na ilikuwa utamaduni wa baadhi ya jamii.

Sasa kwa dunia ya artificial intelligence, hayo mafimbo na marungu, na mavisu yana faida gani? Ni sawa na kukomalia kulala porini Ngorongoro, bila nyumba eti utamaduni

Hizo fimbo ni za kuchungia ngombe, wana ngombe huko zanzibar hao wamasai? Kuna simba zanzibar kwamba watakutana naye wapambane naye kwa kutumia hizo silaha?

Utamaduni wa konyo
Wewe chiemba sijui kama huwa zinakitosha kweli,kutoka umezaliwa na kukua,ulishawahi kumwona masai amekata mtu humu mjini?,kwa nn watu wajinga wanazidi kuongezeka hapa nchini?!, tena wajinga wengine unakuta wana shahada.
 
Yaan we jombaa ni kiaz hebu nenda China vijijin huko au hata Japan au hata sehem za Scotland au hata uarabuni hasa jamii za mabedui. Au Namibia. Sio kila mtu anataka kuvaa hayo masuti ni ishu kwake au nyumba za block. Kuna watu kuishi kienyeji ndio furaha yake. Ndio jamii za asili wameamua wao kwanini wewe uwapangie furaha yao hapa dunian. Na ninan kakuambia kuvaa kizungu ndio umeendelea.
Shanghai hata wewe,kuna watu wanaamini kuvaa kizungu ndio maendeleo.
 
Zanzibar ina sheria zake, usiingilie !! wamasai wazifuate ama warudi kuchunga mifugo bara.

Bara ni kwajili ya sheria za muungano tu, Zanzibar kuna sheria za Zanzibar na vijisheria vya upande wapili wa muungano.
Hiyo sheria ya Zanzibar kukataza watu kuishi kulingana na tamaduni zao imeanza lini? Huu muungano ni fix tu, mmewafukuza porini sasa mnaona hata mijini hawatakiwi kuishi?
 
Mbona ukeketaji watu wameelimishwa, wakaacha,na ilikuwa utamaduni wa baadhi ya jamii.

Sasa kwa dunia ya artificial intelligence, hayo mafimbo na marungu, na mavisu yana faida gani? Ni sawa na kukomalia kulala porini Ngorongoro, bila nyumba eti utamaduni

Hizo fimbo ni za kuchungia ngombe, wana ngombe huko zanzibar hao wamasai? Kuna simba zanzibar kwamba watakutana naye wapambane naye kwa kutumia hizo silaha?

Utamaduni wa konyo
Wamasai zanzibar unajua wanafanya kazi gani ? Wao wanatumika kama walinzi wa kitalii ni sehemu ya utalii pia ...mbona vazi la hijabu linatumika sana kufanyia ugaidi na waisiharamu awalipigi marufuku ....wapo watu wamejifunza kung fu je hao siyo hatari kuliko fimbo za wamasai au wamasai wakijifunza kung fu wataambiwa wazivue kunf mwilini .....
 
Zanzibar ina sheria zake, usiingilie !! wamasai wazifuate ama warudi kuchunga mifugo bara.

Bara ni kwajili ya sheria za muungano tu, Zanzibar kuna sheria za Zanzibar na vijisheria vya upande wapili wa muungano.
Huo ubaguzi wenu kuna siku utawarudia,anzishe msingi,wengine watainua boma,na hapo ndipo mtalia na kusaga meno,kwa hizi hizi akili zenu za kipunbavu,ndio maana mlikuwa mnayachoma moto makanisa,na kusema zanzibar ni kwa ajiri ya waislamu tu.
 
Hakuna uhatari wowote kwa muungano wetu adhimu, hakuna Jamii sikivu na yenye umoja na pia isiyotaka Shari kama masai, ukiona umegombana nao basi elewa wewe binafsi ndiye mshari, ufanywe mkutano waitwe wapewe taratibu za kiusalama, case closed!, hutasikia tena tatizo lolote mbeleni. (hayo mavazi na rungu na sime ni Utamaduni wao adhimu).
Mimi ni msukuma,wamasai ni watu wapole,wataratibu na wasiopenda ugomvi,ukiona kuna mgogoro na masai,shida itakuwa sio huyo mmsai,shida itakuwa ni wewe.
 
Wewe Yericho umekosa kazi, hawa wamasai wamekua wasumbufu sana Zanzibar, wamejazana huko bila kazi, wanauza sura beach wakitegemea kupata majimama ya kizungu wapelekwe ulaya. Ukiwakuta beach wanasumbua watalii na vikorokoro vyao, kazi za ulinzi zimewashinda sasa wamekua beach boys. Wanabeba Sime na fimbo wakati znz hakuna simba wala ng'ombe. Hawa bora warudishwe kwao kupunguza kero ZNZ. Na wanao sema Zanzibar wabaguzi basi mbona kuna watanganyika wengi sana wenye shughuli zao na hakuna anaye wabughudhi, wanapiga kazi na wanafata sheria, maisha yanaenda.
 
Nina laani kwa nguvu zote kitendo cha vurugu za mgambo na watu wa jamii ya kimasai kwakupigana hadharani, Nina laani Masai kushambulia Mgambo, Nina laani kwa nguvu kubwa Mgambo wa Zanzibar kushanbulia watu wa jamii ya kimasai! Jambo hili halikubaliki kwa mjibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazokataza kupigana hadharani au kificho.

Lakini naomba nitofautiane na hatua iliyochukuliwa na serikali ya Zanzibar, Amri kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime/visu vyao, Ni Kauli Haramu na ya kibaguzi inayohatarisha muungano wa Tangabyika na Zanzibar.

Ifahamike kuwa Fimbo na Sime kwa Jamii za kimasai ni sehemu ya “vazi lao la asili”, ni Sehemu ya utamaduni wao, Ni Identity yao, na hivyo kujaribu kwa aina yoyote kuondoa kimoja wapo katika hivyo vinavyokuwa ndani ya mwili wa Masai ni kutangaza kuwafukuza Wamasi Zanzibar, Hili ni tangazo la kijinga limekurupukwa na mamlaka za Zanzibar!

Kwamiaka yote tangu kabla ya uhuru hadi leo, Jamii za Wamasai wapo Zanzibar na utamaduni wao wa visu/Sime na Fimbo, hakujawahi kuwa hatari kwa raia yoyote, Kwanini iwe leo baada ya Masai kujihami waliposhambuliwa na mgambo wa mji? Serikali ya Rais @dr.hmwinyi itafute jawabu la kumaliza mzozo huu sio kufunika kwakuwafukuza Wamasai, Tatizo liko kwa mamlaka za jiji, Tatizo liko kwa Wakuu wa Mikoa, na mamlaka zingine za jiji.

Unawazuia Wamasai wasibebe fimbo unataka Wabebe Vikapu vya Nazi na vigemeo vya Litembo? Unataka wabebe Usinga? Unataka wabebe karafuu? Noooo nooo tukatae unyanyasaji huu kwa jamii ya kimasai! Ukamilifu wa Masai ni fimbo na sime. Sasa unaka awe na shuka tu kama dera?

Kesho yataibuka Bara Wapemba watashambuliwa, Je serikali iweke amri wapemba wasizaliane kwa Wingi Bara ambao ni sehemu ya utamaduni wao? Nooo Nooo! Tukatae ubaguzi huu.

Mh Rais @dr.hmwinyi ili kunusuri maafa zaidi na kuoondoa hii taswira mbaya ya ubaguzi iliyotengenezwa na mamlaka za mji hapo Unguja, Ninakuomba na kukusihi Mh Rais, tengua hii kauli ya kibaguzi, Haifai kutolewa na kiongozi wa serikali katika ulimwengu wa leo! Madhara yake ni makubwa zaidi mbeleni.

Serikali ijifunze kutatua migogo kwa hekima na busara, Majibu ya hasira ya kiserikali yanaweza kuleta maafa zaidi kuliko kutatua, Nimeisikiliza kauli ikitolewa na yule kiongozi wa mjinibZanzibar (Unguja) ni wazi alitawaliwa na ghadhabu zaidi kuliko hekima ya kiuongozi, Amewahukumu Wamasai bila kujaribu kujua undani na kutafuta jawabu, Badala yake ametafuta jibu ambalo ni la hovyo zaidi!,

Nimesikitika sana kwa kauli hii ya serikali ya Zanzibar katika zama hizi za utandawazi na utandaridhi! Utengamano wa taifa letu ni muhimu kuliko hizi chuki zinazokolezwa na namlaka za nchi!

Na Yericko Nyerere
View attachment 2890368
Watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa wamasai,sio wabantu,wamasai wametokea pembe ya Afrika,walikotokea waarabu,wasomali,waethiopia,na ndio ukaona mila zao,mavazi,ufugaji,kutembea na fimbo,bakora,sime,visu,majambia ,wanafanana.Lakini waarabu na wasomali,wameacha mila za kutembea na fimbo,bakora,visu,sime,majambia,hata huko kwao,kutokana na dunia kubadilika.Kwa mfano waarabu,mila ya majambia na fimbo na bakora,wanaifanya wakati wa ndoa tu,tena ni bwana harusi,ndio anakuwa navyo kama mapambo tu.
Hata wapemba,walikuwa na mila hizo,za kutembea na visu na bakora,lakini walipokuja Tanzania bara,taratibu waliacha mila hizo,kwa kufuata jinsi wenyeji wa Pwani ya Tanzania wanavyoishi.
Kwa hiyo mila hatarishi,,na utamaduni hatarishi ni kuwacha.
 
Wamasai wapo ZNZ kwa miongo kadhaa sasa, kwanini hiyo chuki ianze leo? Acheni kujizima data. Hivi ni mara ngapi nchi hii Wakulima wamekuwa wakishambuliwa na hata kuuawa na jamii ya wafugaji hususani Wamasai? Ni kipi kinawawezesha Wamasai kufanya mashambulizi yao kirahisi hivyo kama sio hiyo the so-called utamaduni wv kutembea na silaha? Acheni ku-justify ujinga kwa kigezo eti cha utamaduni kwa sababu hata huo utamaduni lazima uendane na mazingira. Kwenye yale mazingira yao ya asili ni sawa tu hata kutembea na bunduki kwa sababu you never know ni wakati gani wanyama wakali watatokea mbele yao, sasa Zanzibar unatembea na silaha kwa sababu zipi? Halafu kwanini mnaona ni Wamasai ni exceptional community ambapo sheria zingine ziwaguse wengine tu lakini sio Wamasai? Hii nchi kila kabila lina maeneo yake ya asili, na baadhi yao wamekuwa wakihamishwa vile vile lakini hatujawahi kusikia haya madai ya "mnatuhamisha maeneo yetu ya asili". Wamasai ni jamii ya kwanza kuhamishwa kwenye maeneo tengefu au kwenye hifadhi za taifa?
Wewe unasumbuliwa na chuki za kijinga,au hujawahi kuitembelea dunia na kuona jinsi tamaduni za makabura zinavyolindwa.
 
Huo ubaguzi wenu kuna siku utawarudia,anzishe msingi,wengine watainua boma,na hapo ndipo mtalia na kusaga meno,kwa hizi hizi akili zenu za kipunbavu,ndio maana mlikuwa mnayachoma moto makanisa,na kusema zanzibar ni kwa ajiri ya waislamu tu.
Hivi wewe unajua kuna wabara wangapi wanaishi Zanzibar? Mbona hawana shida yeyote na serikali?Takriban waajiriwa 60% wa mahoteli yote ZNZ wabara, umesikia wamebaguliwa na Wazanzibari?
 
Back
Top Bottom