Rais Mwinyi wa Zanzibar naye atakuwa anamuachia Mama awe anaenda Safari zake kama Mama afanyavyo Kwake?

Rais Mwinyi wa Zanzibar naye atakuwa anamuachia Mama awe anaenda Safari zake kama Mama afanyavyo Kwake?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Sasa ni mara ya Pili au ya Tatu hivi naona Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ' Safari ' zake nyingi ( hasa za Ziara za Mikutano na hata nyinginezo ) anapenda mno ' Kuwakilishwa ' na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Hivyo basi nami GENTAMYCINE nauliza je, na Yeye Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Yeye pia akiwa na Safari za ' Mialiko ' au za ' Uwakilishi ' atakuwa anamuomba ( anamuachia ) Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan awe anaenda?

Nimeupenda sana huu Utaratibu alioubuni Rais Samia Suluhu Hassan hasa wa Kupenda ' Kuwakilishwa ' Safari zake za nje ( za Kimataifa ) na Rais wa Zanzibar tu Dkt. Hussein Ali Mwinyi hivyo kuwafanya Makamu wa Rais JMT Dkt. Philip Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wawe ni ' Wabobezi ' tu wa Safari za ndani ya nchi kama vile Tandahimba - Ibirizi na Biharamuro - Nachingwea za Kukagua Madaraja na Kuhesabu tu Kuku ' waliototolewa ' Kitaalamu SUA Mkoani Morogoro.
 
Mtaalamu, inawezekana umeupenda huo utaratibu ila ukasahau muundo wa serikali ya JMT.

Hussein Mwinyi ni nani katika serikali ya JMT?

WaZNZ wameshaona fursa ya kushika hatamu, SMZ haina kiti popote isipokuwa EAC, raisi wa SMZ hawezi kumuwakilisha raisi wa JMT.

Anamuwakilisha kwenye yale mambo 22 ya Muungano?

Raisi wa SMZ hawezi kuendesha Baraza la mawaziri mbele ya VP kama raisi wa JMT hayupo, iweje awakilishwe na naye nje? Protokali hapa imekaaje?

Nafasi ya raisi wa SMZ kuwa VP kwenye JMT ilishaondolewa kwa kuzingatia mkanganyiko wake, viongozi wakubwa 3 wa JMT wanapaswa kuwa juu ya raisi wa SMZ, sasa inawezekana vipi? Msaidizi wa raisi wa JMT ni VP, kwanini amtume raisi wa SMZ?

Kazi iendelee.
 
Inafikirisha sana.
Na ukiona nimeanzisha Uzi jua kuna ' nilichokibaini ' na nakiona ama hakija kaa sawa au kina ' Ulakini ' hivyo ' nawachokozeni ' tu Great Thinkers ninaowapendeni ( JF Members ) ili tujadili na kwa marefu na mapana yake. Ubunifu huu ' Mama ' nahisi utaanza ( au umeshaanza ) kuzaa ' Visununu ' kwa upande wa Tanzania Bara na najua akina Mpango ( VP ) na Majaliwa ( PM ) linawauma mno ila ' wanajikausha ' tu.
 
Itakuwaje sasa ikiwa wameomba tugawane mbao
Kuna ' insider ' kanitonya ' Kishkaji ' kuwa Daktari wa Falsafa kutokea kwa Watani zangu Mkoani Kigoma huu ' Utaratibu ' wa Mama ' unamchukiza ' kwani nae alijua kama ilivyozoeleka Mtu wa Cheo chake ( Makamu ) ndiyo mara nyingi humuwakilisha Mkuu ( Namba Moja ) Matokeo yake ' pande ' la Safari anapewa mwingine na Yeye kutumwa tu kwenda Kuangalia ' Mazalia ' ya Panya wapya na Mende wa Kufuga SUA Mkoani Morogoro.
 
Mtaalamu, inawezekana umeupenda huo utaratibu ila ukasahau muundo wa serikali ya JMT.

Hussein Mwinyi ni nani katika serikali ya JMT?....
Ninapoanzisha ' Mada ' hapa Jamvini ( JamiiForums ) kisha nikiona ninaanza Kueleweka vyema na JF Intelligent Members ( kama Wewe hivi ) huwa nafurahi sana. Ulichokiandika ndiyo sahihi 100% na ' Mama ' awe makini mno na ' Utaratibu ' huu kwani utazalisha ( unazalisha ) Visununu na ataanza ' Kuhisiwa ' kuwa ana ' Uzanzibari ' mwingi kuliko ' Katiba ' ya JMT inavyotaka.
 
Na ukiona nimeanzisha Uzi jua kuna ' nilichokibaini ' na nakiona ama hakija kaa sawa au kina ' Ulakini ' hivyo ' nawachokozeni ' tu Great Thinkers ninaowapendeni ( JF Members ) ili tujadili na kwa marefu na mapana yake. Ubunifu huu ' Mama ' nahisi utaanza ( au umeshaanza ) kuzaa ' Visununu ' kwa upande wa Tanzania Bara na najua akina Mpango ( VP ) na Majaliwa ( PM ) linawauma mno ila ' wanajikausha ' tu.
Waanakausha vipi, wamuambie ukweli tyuuh kwani protokali inasemaje?
 
Na ukiona nimeanzisha Uzi jua kuna ' nilichokibaini ' na nakiona ama hakija kaa sawa au kina ' Ulakini ' hivyo ' nawachokozeni ' tu Great Thinkers ninaowapendeni ( JF Members ) ili tujadili na kwa marefu na mapana yake. Ubunifu huu ' Mama ' nahisi utaanza ( au umeshaanza ) kuzaa ' Visununu ' kwa upande wa Tanzania Bara na najua akina Mpango ( VP ) na Majaliwa ( PM ) linawauma mno ila ' wanajikausha ' tu.
Rais Mwinyi ndiye Rais Mtarajiwa wa JMT mwaka 2025 kimsingi mama anakamilisha tu kipindi cha mpito kuja kumkabidhi kijiti mwinyi 2025 hili litasimamiwa kwa ukaribu sana na vyombo vya dola kuhakikisha the chosen anakuwa Rais wa JMT hili liko wazi
 
Back
Top Bottom