Kama ulivyo Muungano unavyofikirisha ndivyo ilivyo kwa Rais wa JMT wa Tanzania kuwakilishwa nje ya nchi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Kwa Katiba ya JMT (1977), Rais Mwinyi ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri Serikali ya JMT, lakini kwa Katiba hiyo hiyo, Baraza la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, japo Zanzibar ni sehemu ya nchi ya Tanzania. Hii ina maana maamuzi yanayogusa masuala ya Muungano yaweza kufanyiwa maamuzi bila upande wa pili wa Muungano (Tanzania bara) kuwakilishwa. Ingefaa Waziri anayeshughulikia masuala ya muungano, kama siyo Waziri Mkuu, awakilishe Serikali ya Muungano.
Nukuu ya Ibara husika za Katiba ya JMT (1977):
54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.
(2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye atakayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza
Mikutano hiyo.
Kwa msingi huo wa Ibara ya 54.-(2) Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kumwakilisha Rais wa JMT kiKatiba inafikirisha.
105.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar litakalokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi;
(b) Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(c) Mawaziri wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(d) Wajumbe wengine watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Zanzibar.
Kwa Ibara hiyo ni dhahiri maamuzi ya Baraza yanakuwa hayana baraka za uongozi wa Serikali ya JMT. Yawezekana hii ndio ikawa kiini cha migogoro ya Muungano kwa kuwa yanayoamriwa katika hilo Baraza hayapingwi mahala popote.
Nukuu ya Katiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (1984), Toleo la 1995:
1. Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
...
4. Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yo yote inatofautiana na Katiba hii, basi Kaliba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.
80.-(1) Kwa masharti ya kifungu hiki Baraza la Wawakilishi linaweza
kubadilisha kifungu chochote katika Kaliba hii.
Kimsingi maamuzi ya Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi, ambayo hayana mwakilishi wa Serikali ya Muungano yanaweza kuathiri shughuli za Muungano na ustawi wake.
43.-( 1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi ambalo litajumuisha Rais, Waziri Kiongozi, Mawaziri pamoja na Wajumbe wengine kama Rais atavyoona inafaa.
...
(5) Baraza la Mapinduzi kwa pamoja litawajibika kwa Baraza la Wawakilishi p.unoja na watu kwa ujumla kuhusiana ua mambo yate yaliyotenowa na au kwa amri ya Rais au Waziri Kiongozi au Waziri mwengine kalika utekelezaji wa shughuli zake za kazi.
Vifungu hivyo vya Katiba vinalipa Baraza la Mapinduzi, ambalo halina mwakilishi kutoka upande wa pili wa Muungano, kufanya maamuzi, km kwa kifungu cha 80.-(1) ambayo yanaweza kuathiri afya ya muungano.
Yafuatayo ni majumuisho yangu kwa mtazamo wangu binafsi. Awali Rais wa JMT kutoka Zanzibar alikuwa Ali Hasani Mwinyi. Pamoja kwamba mwanzilishi wa muungano, Baba wa Taifa, Mwl Nyerere, alikuwa bado hai, aliweza kuvunja Azimio la Arusha na kuruhusu Katiba ya Serikali ya Mapinduzi kufanyiwa marekebisho yaliyotambua Zanzibar kama nchi na Taifa kiasi cha kuwa na wimbo na bendera. Nanukuu hiyo Katiba (2) Serika.li ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na uwezo wa kuweka kitu chochote kitakachokuwa kielelezo cha Serikali kama itavyokubaliwa na sheria iliotungwa na Baraza la Wawakilishi ambalo halina mwakilishi kutoka Tanzania bara kama ilivyo kwa Bunge la JMT
Sasa Serikali ya JMT inaongozwa na Mzanzibari tutegemee mabadiliko makubwa ya Kijamii, Kisiasa na Kiuchumi kwa faida ya Zanzibar.