Rais Mwinyi wa Zanzibar naye atakuwa anamuachia Mama awe anaenda Safari zake kama Mama afanyavyo Kwake?

Rais Mwinyi wa Zanzibar naye atakuwa anamuachia Mama awe anaenda Safari zake kama Mama afanyavyo Kwake?

Rais Mwinyi ndiye Rais Mtarajiwa wa JMT mwaka 2025 kimsingi mama anakamilisha tu kipindi cha mpito kuja kumkabidhi kijiti mwinyi 2025 hili litasimamiwa kwa ukaribu sana na vyombo vya dola kuhakikisha the chosen anakuwa Rais wa JMT hili liko wazi
Yeye Mama aliwaambia Urais hautaki 2025? Hivi kwa Afrika hii uijuayo Wewe kuna Mtu ' akiuonja ' tu ' Urais ' atatamani Kuondoka mapema Madarakani na Kumkabidhi Mtu mwingine ' Kiurahisi ' tu kama msemavyo?
 
Yeye Mama aliwaambia Urais hautaki 2025? Hivi kwa Afrika hii uijuayo Wewe kuna Mtu ' akiuonja ' tu ' Urais ' atatamani Kuondoka mapema Madarakani na Kumkabidhi Mtu mwingine ' Kiurahisi ' tu kama msemavyo?
Na mie nashangaa hapo.
 
Matukio na mazingira yanatufanya tuelewe kuwa tatizo la nchi hii ni mfumo wake,tuna mfumo wa kisanii na sio wa kiesheria na kiutaalamu, mkuu wa nchi Anakuwa mfalme anaweza kufanya chochote anachoamua, anachosema ndio kinakuwa protocol wakati wowote,tunaishi kwa kusubiri hisani,huruma na ubinafsi wa mkuu
Ili kuondoa ubinafsi na kusubiri huruma za mtu binadamu tunatakiwa tuongozwe na mfumo imara wa kimikataba na sheria imara
 
Bado zipo Safari nyingi tu za huko nje za VP kuweza kuhudhuria.

Awamu iliyopita Chato paliongelewa vibaya na naona awamu hii Unguja itaongelewa vibaya.

JPM alimpa Safari KMM, upo uwezekano wa Awamu hii kupewa Safari. Bado mapema sana kumhukumu Madame kwamba anapendelea kwao.

Na hata kwao ni sehemu ya Tanzania.
 
Bado zipo Safari nyingi tu za huko nje za VP kuweza kuhudhuria.

Awamu iliyopita Chato paliongelewa vibaya na naona awamu hii Unguja itaongelewa vibaya.

JPM alimpa Safari KMM, upo uwezekano wa Awamu hii kupewa Safari. Bado mapema sana kumhukumu Madame kwamba anapendelea kwao.

Na hata kwao ni sehemu ya Tanzania.
Hakika.....
 
Mtaongea katiba na sheria ila kiukweli hii nchi inaongozwa kadri rais atavyotaka.

Naona wazenji wameshika usukani.

Tanzaniaa (Tanganyika + Zenji) anaongoza Mzenji na huko zenji anaongoza mzenji...acha wazenji wajipe raha.

Bara kubwa lkmepanuliwa naona kakisiwa kadogo ka zenji kanaingiza tu 😂😂😂, Nyie kuna raha ya kuwa mzenji acheni tu, wanaoukataa muungano huko zenji ni wasio na kazi tu ila viongozi hawa ambao wanakuja kuongoza mpaka wizara na idara mbali mbali
za Tz na kupiga mishahara minono hawawezi kukuelewa.


Nao kina Mkwawa wangekomaa wawe kama zenji kujipa ka nchi kao na kuunda serikali ya muungano saizi wangekuwa wanakula vinono
 
Waanakausha vipi, wamuambie ukweli tyuuh kwani protokali inasemaje?
Nani amuambie ukweli Rais ,VP?!!!

Mbona VP alikuwepo kipindi cha hayati JPM ,alikuwa anaweza kumuambia kitu Rais ?!!!

By the way VP ni msaidizi wa Rais akiwa hayupo....ila KATIBA yetu inampa mamlaka makubwa Rais wa nchi.....na ndivyo zilivyo katiba za nchi nyingi duniani......

Presidential decree haimzuii Rais kumtuma Rais wa Zanzibar kumuwakilisha nje ya nchi....

Safari ni nyingi....na kila safari ina malengo yake na umuhimu wa kipekee.........

#KaziIendelee
 
Yeye Mama aliwaambia Urais hautaki 2025? Hivi kwa Afrika hii uijuayo Wewe kuna Mtu ' akiuonja ' tu ' Urais ' atatamani Kuondoka mapema Madarakani na Kumkabidhi Mtu mwingine ' Kiurahisi ' tu kama msemavyo?
Mama ni Rais wa mpito na bado vyombo vya dola vina mamlaka kwa sasa vinakuwa bega kwa bega kuhakikisha utaratibu u unafuatwa ukiwemo na utaratibu wa kumpata Rais baada yake maana yake vina nguvu ya kuamua aliyeko kwenye list anakuwa na hili zoezi litakamilishwa kwa ustadi mkubwa Sana na kwa kweli hili jambo ni la kuigwa sana kwa kucishukuru vyombo vya dola vinaivusha nchi yetu salama salmini
 
Hapo maza anaharibu wasijisahaulishe wao wako milioni moja na nusu tu, wanapotaka fursa sawa wajue wengi ndio tunaoamua hatma ya Muungano feki unaowanufaisha Zanzibar kuliko Tanganyika Mbona magufuli alimwagiza sana Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuliko mwingine yoyote,
 
Bora hata VP ila PM ni ' Muoga ' mno tu.
Katika hiki nadhani linaonesha umuhimu mkubwa wa marekesho ya katiba (Katiba mpya). Maana ukiangalia Kijamhuri Rais wa Zanzibar hana mamlaka yoyote bara, na PM hana mamlaka ya maana Zanzibar na pengine huwa analazimisha kwenda ziara katika nchi ambayo yeye hana mamlaka yoyote. Ukichungulia nyuma ya pazia utaona uwazi katika cheo cha PM kwa upande wa Zanzibar.
Lakini mbali ya mauzauza haya bado kuna watu hawaoni uhitaji wa katiba itakayotufanya tuendeshe nchi kwa misingi ya Sheria.
 
Mama ni Rais wa mpito na bado vyombo vya dola vina mamlaka kwa sasa vinakuwa bega kwa bega kuhakikisha utaratibu u unafuatwa ukiwemo na utaratibu wa kumpata Rais baada yake maana yake vina nguvu ya kuamua aliyeko kwenye list anakuwa na hili zoezi litakamilishwa kwa ustadi mkubwa Sana na kwa kweli hili jambo ni la kuigwa sana kwa kucishukuru vyombo vya dola vinaivusha nchi yetu salama salmini
Unaota ndoto, Samia bado yupo sana, kuondoka ni 2035
 
Na ukiona nimeanzisha Uzi jua kuna ' nilichokibaini ' na nakiona ama hakija kaa sawa au kina ' Ulakini ' hivyo ' nawachokozeni ' tu Great Thinkers ninaowapendeni ( JF Members ) ili tujadili na kwa marefu na mapana yake. Ubunifu huu ' Mama ' nahisi utaanza ( au umeshaanza ) kuzaa ' Visununu ' kwa upande wa Tanzania Bara na najua akina Mpango ( VP ) na Majaliwa ( PM ) linawauma mno ila ' wanajikausha ' tu.
Kama ulivyo Muungano unavyofikirisha ndivyo ilivyo kwa Rais wa JMT wa Tanzania kuwakilishwa nje ya nchi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Kwa Katiba ya JMT (1977), Rais Mwinyi ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri Serikali ya JMT, lakini kwa Katiba hiyo hiyo, Baraza la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, japo Zanzibar ni sehemu ya nchi ya Tanzania. Hii ina maana maamuzi yanayogusa masuala ya Muungano yaweza kufanyiwa maamuzi bila upande wa pili wa Muungano (Tanzania bara) kuwakilishwa. Ingefaa Waziri anayeshughulikia masuala ya muungano, kama siyo Waziri Mkuu, awakilishe Serikali ya Muungano.

Nukuu ya Ibara husika za Katiba ya JMT (1977):

54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.
(2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye atakayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza
Mikutano hiyo.


Kwa msingi huo wa Ibara ya 54.-(2) Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kumwakilisha Rais wa JMT kiKatiba inafikirisha.

105.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar litakalokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi;
(b) Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(c) Mawaziri wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(d) Wajumbe wengine watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Zanzibar.


Kwa Ibara hiyo ni dhahiri maamuzi ya Baraza yanakuwa hayana baraka za uongozi wa Serikali ya JMT. Yawezekana hii ndio ikawa kiini cha migogoro ya Muungano kwa kuwa yanayoamriwa katika hilo Baraza hayapingwi mahala popote.

Nukuu ya Katiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (1984), Toleo la 1995:

1. Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
...
4. Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yo yote inatofautiana na Katiba hii, basi Kaliba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.

80.-(1) Kwa masharti ya kifungu hiki Baraza la Wawakilishi linaweza
kubadilisha kifungu chochote katika Kaliba hii.


Kimsingi maamuzi ya Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi, ambayo hayana mwakilishi wa Serikali ya Muungano yanaweza kuathiri shughuli za Muungano na ustawi wake.

43.-( 1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi ambalo litajumuisha Rais, Waziri Kiongozi, Mawaziri pamoja na Wajumbe wengine kama Rais atavyoona inafaa.
...
(5) Baraza la Mapinduzi kwa pamoja litawajibika kwa Baraza la Wawakilishi p.unoja na watu kwa ujumla kuhusiana ua mambo yate yaliyotenowa na au kwa amri ya Rais au Waziri Kiongozi au Waziri mwengine kalika utekelezaji wa shughuli zake za kazi.


Vifungu hivyo vya Katiba vinalipa Baraza la Mapinduzi, ambalo halina mwakilishi kutoka upande wa pili wa Muungano, kufanya maamuzi, km kwa kifungu cha 80.-(1) ambayo yanaweza kuathiri afya ya muungano.

Yafuatayo ni majumuisho yangu kwa mtazamo wangu binafsi. Awali Rais wa JMT kutoka Zanzibar alikuwa Ali Hasani Mwinyi. Pamoja kwamba mwanzilishi wa muungano, Baba wa Taifa, Mwl Nyerere, alikuwa bado hai, aliweza kuvunja Azimio la Arusha na kuruhusu Katiba ya Serikali ya Mapinduzi kufanyiwa marekebisho yaliyotambua Zanzibar kama nchi na Taifa kiasi cha kuwa na wimbo na bendera. Nanukuu hiyo Katiba (2) Serika.li ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na uwezo wa kuweka kitu chochote kitakachokuwa kielelezo cha Serikali kama itavyokubaliwa na sheria iliotungwa na Baraza la Wawakilishi ambalo halina mwakilishi kutoka Tanzania bara kama ilivyo kwa Bunge la JMT

Sasa Serikali ya JMT inaongozwa na Mzanzibari tutegemee mabadiliko makubwa ya Kijamii, Kisiasa na Kiuchumi kwa faida ya Zanzibar.
 
Sasa ni mara ya Pili au ya Tatu hivi naona Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ' Safari ' zake nyingi ( hasa za Ziara za Mikutano na hata nyinginezo ) anapenda mno ' Kuwakilishwa ' na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Hivyo basi nami GENTAMYCINE nauliza je, na Yeye Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Yeye pia akiwa na Safari za ' Mialiko ' au za ' Uwakilishi ' atakuwa anamuomba ( anamuachia ) Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan awe anaenda?

Nimeupenda sana huu Utaratibu alioubuni Rais Samia Suluhu Hassan hasa wa Kupenda ' Kuwakilishwa ' Safari zake za nje ( za Kimataifa ) na Rais wa Zanzibar tu Dkt. Hussein Ali Mwinyi hivyo kuwafanya Makamu wa Rais JMT Dkt. Philip Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wawe ni ' Wabobezi ' tu wa Safari za ndani ya nchi kama vile Tandahimba - Ibirizi na Biharamuro - Nachingwea za Kukagua Madaraja na Kuhesabu tu Kuku ' waliototolewa ' Kitaalamu SUA Mkoani Morogoro.
Ni walakini mkubwa sana; kama anapenda Zanzibar isikikike zaidi, basi ateuwe Waziri wa mambio ya nje kutoka Zanzibar ndiye awe anamwakilisha, kama ambavyo Mwinyi alikuwa amemuweka Hassan Diria. Lakini kumtumia Rais wa Zanzibar kumwakilisisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ni kosa kubwa na ni uvunjaji mkubwa wa katiba. Mama asilewe madaraka kupita kiasi!
 
Back
Top Bottom