Rais Mwinyi: Watu wanadhani kuweka kodi kubwa ndio pato kubwa kwa Serikali, kodi kubwa inapunguza wafanyabiashara

Rais Mwinyi: Watu wanadhani kuweka kodi kubwa ndio pato kubwa kwa Serikali, kodi kubwa inapunguza wafanyabiashara

Leo Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ameitisha kikao na wafanyabiashara na kuongelea changamoto zinazoikabili sekta ya biashara Zanzibar na muelekeo wa kuzitatua. Kikao hiko kimehudhuriwa na wafanyabiashara pamoja na mawaziri wa serikali ya Zanzibar

Pamoja na mambo mengine, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema hatafuatilia wafanyabiashara waliokwepa kodi kipindi cha nyuma lakini kuanzia sasa wote walipe kodi.

Huu ukiwa utaratibu tofauti sana na aliotumia Rais wa Jamhuri, Dkt. John Magufuli alipoingia madarakani kwa kufukua makaburi ya makontena yaliyoingizwa kupitia bandari na wahusika kutakiwa kulipa tofauti ya kodi yote iliyoonekana kukwepwa kwenye awamu iliyotangulia. Wapo walioshindwa na kampuni zao kufa na wengine kuonja chungu ya gereza kwa makosa ya uhujumu uchumi.

========

MWINYI: Zipo tabia za kufanya mikutano mingi bila ufumbuzi, mimi katika utawala wangu tabia hiyo sitoitaka. Tunapokutana, ninapozungumza changamoto ikawekwa, mkachukua halafu mkawa hamjazifanyia kazi ni kupoteza muda na mimi nataka niwaambie watendaji wote serikalini kwamba nina ahadi na wananchi ya muda wa miaka mitano, sina muda wa kupoteza, lazima tufanye kazi hii kwa haraka, lazima tujitahidi kuondoa changamoto zote na zile ambazo zitakuwa ngumu kwenu, mimi nipo, nileteeni nitahahakisha tunazimaliza.

Lengo la mkutano huu nimeuitisha kwa madhumuni ya kuwahakikishieni wafanyabiashara kwamba serikali yangu itatoa msukumo mpya katika kutatua changamoto zinazokabili biashara Zanzibar.

Ahadi yangu kwenu ni kuondoa changamoto zote zinazokwamisha biashara hapa Zanzibar. Najua kuna changamoto ya kodi mathalan, mimi sio muumini wa masuala ya kuweka kodi kubwa kwa sababu watu wanadhani kuweka kodi kubwa ndio pato kubwa kwa serikali, ni kinyume chake.

Kodi kubwa inapunguza wafanyabiashara, watakaofanya biashara kwa kodi kubwa ni wachache lakini tukipunguza kodi watakaofanya biashara ile ni wengi. Lakini serikali haiishi kwenye kodi tu.

Tukiweka kodi ndogo maana yake kuna watu nje ya Zanzibar watakuja kufanya shopping hapa Zanzibar, hoteli zetu zitajaa, teksi zetu zitakuwa na wateja, migahawa yetu itajaa, hiyo itaongeza mzunguko wa fedha katika uchumi.

Uchumi wetu utaendeshwa na sekta binafsi, ahadi kwenu ni kwamba serikali itaweka mazingira rafiki ya kufanya biashara na tutaondoa urasimu, tutaondoa rushwa, tutaondoa vikwazo vyote vinavyosababishwa na utendaji katika serikali. Maono yangu ni kuifanya Zanzibar iwe kituo cha biashara katika ukanda wetu. Mwenyezi Mungu ametujaalia tupo katika jiografia nzuri sana, tuna uwezo wa kuwa kitovu cha biashara.
Zanzibar kuwa kitovu cha biashara? Hizi ni ahadi zile zile za rais aliyepita hakuna tofauti Dr Sheni alisema Zanzibar itakuwa Dubei, haya maneno laini anayotoa ni kutafuta upendo kwa wazanzibari ingawa mikono yake tayari imesharukiwa na damu za watu. Kwa kauli hizi Je tusahau pia ndugu zetu waliouliwa na kuteshwa kikatili paka leo kule Pemba? Hakuchaguliwa kwa kura aliingia madakani kwa mapinduzi, Waunguja hawakumpenda hawakumpa kura ata 1 kule dodoma.
 
....watu wanadhani kuweka kodi kubwa ndio pato kubwa kwa serikali, ni kinyume chake.

Kodi kubwa inapunguza wafanyabiashara, watakaofanya biashara kwa kodi kubwa ni wachache lakini tukipunguza kodi watakaofanya biashara ile ni wengi. Lakini serikali haiishi kwenye kodi tu.

Tukiweka kodi ndogo maana yake kuna watu nje ya Zanzibar watakuja kufanya shopping hapa Zanzibar, hoteli zetu zitajaa, teksi zetu zitakuwa na wateja, migahawa yetu itajaa, hiyo itaongeza mzunguko wa fedha katika uchumi.
Kumbe huyu angalau ana hekima.

Nchi imekosa maono muda mrefu.

Tuna bandari kubwa. Waganda wanaagiza bidhaa zao kupitia bandari ya Dar. Zinasafirishwa zaidi ya 1000km hadi Uganda. Wafanya biashara wa kkoo wanasafiri hadi Uganda kununua hizo bidhaa, wanasafirisha tena kurejesha kkoo, wanauza na kupata faida!

Yaani, badala ya waganda waje kushop kkoo maana tuna bandari, watz ndo wanaenda ku shop Uganda. Sabb ni sera zetu mbovu za Kodi, na Kodi rafiki kibiashara za Uganda. Hatuangalii athari za sera zetu kiuchumi. Walau huyo Hussein anaeza onyesha njia
 
Kama kaamua kuanza upya na kusamehe wakwepa kodi wa nyuma sawa.

Ila nina uhakika somewhere kwenye sheria zetu za kodi kuna maelezo mfanyabiashara anatakiwa atunze record zake za kibiashara kwa miaka kadhaa (nchi nyingine kwa muda wa miaka sita).

Vinginevyo jamaa wakidhani kodi yako unayolipa sio sahihi wakija kukukagua ikabainika kweli unatakiwa kulipa zaidi.

Wanaweza kukagua na miaka ya nyuma pia kama ulikuwa unawaibia. Iwapo huna records kwa kipindi unachotakiwa kutunza kumbukumbu kwa mujibu wa sheria. Tegemea estimates itakuwa kiwango walichobaini wanakudai mwaka huo na wanaweza backdate miaka kadhaa nyuma kwa mujibu wa sheria.

Huo ndio utaratibu nchi nyingi duniani; sio jambo la kushangaza kabisa kudaiwa kodi miaka 5 nyuma. Busara ni kuilipa tu.
 
Suala la Kodi hutegemea na falsafa ya mtawala. Mfano kuna mtawala yeye hana confidence ya kuongoza wasomi na matajiri sababu hana confidence ya kujibu ukosoaji. Huyu utumia Kodi Kama fimbo ya kuwafanya watu wawe masikini inaitwa kuisoma namba kwake ni salama zaidi kuwafanya watu wawe masikini kwa kuwakomoa wafanyabiashara kwa kuwapiga Kodi kubwa lengo wengi wafikisike. Na kuna mtawala kwake lengo kuu ni kuzalisha idadi ya wafanyabiashara akiamini ni heri kutoza kidogo ukusanye kingi kuliko kingi ukusanye kidogo.
 
Yaonekana Dr. Mwinyi ana washauri wazuri wa masuala ya uchumi na anafuata ushauri wao. Ameongea kwa hekima na kwa mustakabali wa kuwabeba wafanyabiashara na sekta binafsi kuing'arisha Z'bar. Naiona Z'bar iliyojaa watalii na Soko huria baada ya miaka miwili kuanzia sasa.
 
Mungu saidia na huku kwetu iwe hivi.. maana wengine TRA wanatufanya tunakonda kila siku 🥲🥲
Si ununue skinjeans?..! Hata kama akipunguza kodi bidhaa kuja bara zitakuwa na kodi kabambe, labda uuzie Comoro na Kenya..
 
Yaonekana Dr. Mwinyi ana washauri wazuri wa masuala ya uchumi na anafuata ushauri wao. Ameongea kwa hekima na kwa mustakabali wa kuwabeba wafanyabiashara na sekta binafsi kuing'arisha Z'bar. Naiona Z'bar iliyojaa watalii na Soko huria baada ya miaka miwili kuanzia sasa.
Nahisi watamuua maana amewazidi maarifa
 
Si ununue skinjeans?..!hata kama akipunguza kodi bidhaa kuja bara zitakuwa na kodi kabambe,,labda uuzie comoro na kenya..
Mkuu mie ni mkandarasi.. nishapunguza watu kibao kazini, na mie mwenyewe nataka kujipunguza kama TRA na mie hatutofikia good terms
 
Huo ndo udakitari wa kusomea kweli kweli, huyu wa huku yeye kudhani ana PHD anadhani ana akili kuliko wote, kejeli, ubabe, dharau, unyama yaani. nami nahamia Zanzibar
 
Back
Top Bottom