Rais na Taasisi saidizi zirudi Dar es Salaam, Makamu wa Rais abaki Dodoma

Rais na Taasisi saidizi zirudi Dar es Salaam, Makamu wa Rais abaki Dodoma

Mkuu

Usikute huyu anayetoa maoni haya ndio msaidizi wa karibu wa Rais kwa sasa na ushauri wake kuzingatiwa, mtashuhudia hivi vituko kwa wingi sana.
Siyo vituko, ni jambo linalowezekana ingawa linaweza lisiwe muhimu sana. Kwa maoni yangu ilipaswa kila Wizara iwe na Ofisi ndogo angalau hapa Dar. Lakini pia Taasisi zilipaswa zibaki Dar, kama ambavyo Bandari by Default haiwez kuhama Dar.
 
Umetanguliza ukali wa kitoto na labda hujachangia hata kuku kama harambee ya kuhamia Dodoma.
Kwani from 1973 hadi leo walishamaliza kila kitu?
Unafikiri kufoka ndio kutaipaisha Dadoma kuwa Canberra ya Australia?
Je kwanini mhasisi Julius Nyerere alipiga about urn ,licha ya yeye kuwa ndio champion wa hiyo kuhamisha makao makuu kwenda Dodoma ,from 1975 hadi anangatuka uraisi alinywea baada ya kugundua mapungufu makubwa ya kuhamisha makao makuu.
Hata from 1985 hadi anafariki hakuligusia kabisa licha ya kuwa very active kwenye siasa za Tanzania na za mataifa?
Weka sababu za msingi zakuhamisha Capital to Dodoma.Je ni maslahi ya taifa au ni utumiaji mbovu wa pesa za umma ?
Umeongea vizuri sana mkuu!
 
Nakupinga, Dodoma ni sehemu sahihi kabisa kwa mazingira ya nchi yetu. Huduma zote za serikali zinapaswa kuwa sehemu ambayo kila mwananchi ataweza kufika kwa haraka, Dodoma ni katikati ya nchi, ni rahisi kwa kila mwananchi kutoka pande zote za nchi kufika haraka na kurudi atokako.
Katikati ya nchi ni Singida!
 
Sababu kuu ya muda wote ya kuhamisha makao makuu kutoka Dar kwenda Dodoma imekuwa ikitajwa ni uwepesi wa kufikika kutoka pembezoni hasaa ikizingatiwa Dodoma ni katikati ya nchi. Sina kumbukumbu ya sababu nyingine ya kuhamisha makao makuu kutoka Dar to Dom, labda unijuze mkuu
Akiitaja, naomba uni tag. Kwa miaka yote, sababu kuu ni Katikati ya nchi na mambo ya Security
 
Ni maoni tu kwamba ni vema Rais wa JMT na taasisi saidizi zikarudi Dar es salaam na Makamu wa Rais, Waziri mkuu na Spika wa bunge wakaendelea kubaki Dodoma pamoja na wizara zote.

Uhamiaji wa Dodoma ulifanywa kwa haraka haraka na mambo mengi ya muhimu na msingi bado yako Dar es salaam ikiwemo Ikulu ya kihistoria ya Magogoni.

Dodoma itakapokamilika kwa miundombinu na kitaasisi basi Rais wa JMT arejee kwenye Ikulu ya Chamwino kama patakuwepo na ulazima huo wakati husika.

Mungu wa mbinguni awabariki.

Kazi Iendelee!
We nae umejaza virus kichwani mwako..huna jipyaa..umeyumbaa mzee matagaaa...huelewek..mara hili mara lile..nyie ndo mnaicost hii nchi..mijitu isieleweka..
 
Umeongea vizuri sana mkuu!
Mkuu mimi nilifanya kazi prime ministers office Dodoma 1974 hadi 1975 chini ya PM Mzee Rashid Kawawa hapo Dodoma. Lakini ule moto wa kuhamia Dodoma ulizimika ghafla baada ya Mwalimu Nyerere kueleweshwa.
Lakini kwa kuwa wakati huo hakuna kuhoji,mambo yalimalizika kimya kimya.
Kaja mjomba Magufuli kakoleza moto pasipo kujua a b,c,ya kuhamia Dodoma, katutengenezea bomu la nuclear.
 
Tumeshatumia gharama sana kiusalama Dodoma ni salama zaid ukanda wa habari ni pagumu
 
Ni maoni tu kwamba ni vema Rais wa JMT na taasisi saidizi zikarudi Dar es salaam na Makamu wa Rais, Waziri mkuu na Spika wa bunge wakaendelea kubaki Dodoma pamoja na wizara zote.

Uhamiaji wa Dodoma ulifanywa kwa haraka haraka na mambo mengi ya muhimu na msingi bado yako Dar es salaam ikiwemo Ikulu ya kihistoria ya Magogoni.

Dodoma itakapokamilika kwa miundombinu na kitaasisi basi Rais wa JMT arejee kwenye Ikulu ya Chamwino kama patakuwepo na ulazima huo wakati husika.

Mungu wa mbinguni awabariki.

Kazi Iendelee!
Ushauri wako haufai kufuatwa.. kabla hata Magufuli kuingia madarakani tayari hizo plan za kuhamia Dodoma zilikuwepo,

Nikupe dokezo tu.. adui kufikia ikulu ya Dar Es Salaam ni rahisi kuliko ile ya Dodoma.. watu hawakukurupuka alafu Mbona Dodoma pashakuwa patamu tu.

Dar es salaam klibaki kuwa jiji la kibiashara tu..
 
Kamwulize ambaye ameanza kusihi kwenye hilo jumba jeupe magogoni amekutana na kitu gani halafu urejee kutetea mawazo mfu. Makao makuu ya nchi ni sharti yabaki DODOMA. Mtwara na Kigoma ni lazima zipewe hadhi ya JIJI kwa kuonesha maendeleo ya akili, watu na vitu

Wabaguzi pekee ndio wanaotetea Ikulu kubaki Dar Es Salaam kwa kuwa ni wavivu na hawako kwa ajili ya kushiriki changamoto za wananchi wa chini.

Nilitegemea wapinzani kama ninyi mngetilia maanani suala la serikali kuwa DODOMA kiukamilifu badala ya kukimbilia raha za Dar huku wananchi maskini wakiendelea kuwa duni bila tumaini la kupata nafuu.

Hao wananchi unaosema wanapata shida si ndio hao mlisema waliichagua ccm, sasa kwakuwa viongozi wote ni wa ccm wawaulize kwanini wanarudi Dar. Ni hivi kuhamia Dodoma kwa sasa ilikuwa ni utashi wa Magufuli pekee, na ukitaka kuamini kawaulize viongozi waliokuwa wanamuunga Magufuli kuhamia Dodoma wabaki Dodoma, na wale waliokuwa hawakubaliani kuhamia Dodoma warudi Dar. Utashangaa watakaorudi Dar wa kwanza ni wale waliokuwa wanamsifia Magufuli kuhamia Dodoma kwa kiwango cha juu.
 
Ushauri wako haufai kufuatwa.. kabla hata Magufuli kuingia madarakani tayari hizo plan za kuhamia Dodoma zilikuwepo,

Nikupe dokezo tu.. adui kufikia ikulu ya Dar Es Salaam ni rahisi kuliko ile ya Dodoma.. watu hawakukurupuka alafu Mbona Dodoma pashakuwa patamu tu.

Dar es salaam klibaki kuwa jiji la kibiashara tu..

Adui gani wa maana atashindwa kufika Dodoma lakini aweze kufika Dar tu? Mkuu au unazungumzia adui anayetumia mawe nini?
 
Kuna watu wanaambiwa wapanue mawazo wao wanabanua [emoji527][emoji527] mata.ko kama mwanzisha uzi
 
Hao wananchi unaosema wanapata shida si ndio hao mlisema waliichagua ccm, sasa kwakuwa viongozi wote ni wa ccm wawaulize kwanini wanarudi Dar. Ni hivi kuhamia Dodoma kwa sasa ilikuwa ni utashi wa Magufuli pekee, na ukitaka kuamini kawaulize viongozi waliokuwa wanamuunga Magufuli kuhamia Dodoma wabaki Dodoma, na wale waliokuwa hawakubaliani kuhamia Dodoma warudi Dar. Utashangaa watakaorudi Dar wa kwanza ni wale waliokuwa wanamsifia Magufuli kuhamia Dodoma kwa kiwango cha juu.
Nakubaliana na wewe bwashee!
 
Hiii ndio Jf mama amashinda humu kila dakika na ssi wana JF MAMA ANATUSIKILIZA SANA SO TUENDELEEE KUMSHAURI TUMPE MADINI NA SS WANA JF TU WAWAKILISHE WENZETU TZ
 
Mkuu mimi nilifanya kazi prime ministers office Dodoma 1974 hadi 1975 chini ya PM Mzee Rashid Kawawa hapo Dodoma. Lakini ule moto wa kuhamia Dodoma ulizimika ghafla baada ya Mwalimu Nyerere kueleweshwa.
Lakini kwa kuwa wakati huo hakuna kuhoji,mambo yalimalizika kimya kimya.
Kaja mjomba Magufuli kakoleza moto pasipo kujua a b,c,ya kuhamia Dodoma, katutengenezea bomu la nuclear.

Bado hujafafanua vizuri.
 
Dar ishaelemewa, miundombinu mibovu sana. At least hiyo Dom maana iko well planned.
 
Adui gani wa maana atashindwa kufika Dodoma lakini aweze kufika Dar tu? Mkuu au unazungumzia adui anayetumia mawe nini?

Binafsi nina sababu 2.
1. Divesification, kwamba miji mingine ijengeke ili vijana wawe na sehemu kadhaa ya kwenda kujitafutia.
2. Congestion reduction. Wazia nalo bunge lingekuwa Dar. Halafu unakuwa kipindi cha bunge la bajeti kama hili.
 
Back
Top Bottom