Nalendwa
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 7,467
- 13,026
Rais wa Venezuela amenusulika katika jaribio linalosemekana la kutaka kumuua kwa kutumia drone device, wakati akihutubia mkutano mjini Caracas. Rais Maduro hakupata madhara yoyote katika tukio hilo ingawa wanajeshi saba waliumia.
Television ya Taifa ilionyesha hotuba ya Rais ikikatishwa ghafla wakati wa sherehe (National Guard's 81 anniversary)
Waziri wa habari wa Venezuela amenukuliwa akisema, "There had been an "attack" against the president involving drones loaded with explotives. Maduro is "fine" and continuing to work"
==========
Rais wa Venezula Nicolás Maduro anasema amenusurika jaribio la kumuua kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani iliyokuwa na vilipuzi.
Bwana Maduro alikuwa akizungumza wakati wa warsha moja ya kijeshi mjini Caracas wakati jaribio hilo la kumuua lilitokea.
Video ya hotuba yake inaonyesha rais akitazama juu ghafla kwa hofu huku wanajeshi kadhaa wakikimbia.
Bw Maduro ameilaumu Colombia kwa shambulizi hilo madai ambayo yakananushwa na Colombia.
Wanajeshi saba walijeruhiwa na watu kadhaa wakakamatwa kwa mujibu wa mamlaka za Venezuela.
Kipi kinafahamika kuhusu shambulizi hilo?
Kisa hicho kilitokea wakati Bw Maduro alikuwa akizungumza kwenye warsha ya kuadhimisha miaka 81 ya jeshi la taifa.
Ndege mbili zisizokuwa na rubani zilizokuwa zimejazwa milipuko zililipuka karibu na jukwaa la rais, kwa mujibu wa waziri wa mawasiliano Jorge Rodriguez
Bw Maduro baadaye alisema kuwa "kifaa kilichokuwa kinaruka kililipuka karibu na mimi, mlipuko mkubwa. Sekunde chache baadaye kulikuwa na mlipuko wa pili."
Picha kwenye mitandao wa kijamii zilionyesha walinzi wakimlinda Maduro wakitumia vifaa visivyopenya risasi baada ya shambulizi hilo.
Bw Maduro aliilaumu nchi jirani ya Colombia na vikundi vingine vyenye uhusiano na Marekani kwa njama hiyo ya kutaka kumuua.
Aliongeza kuwa haka shaka kuwa rais wa Colombia Juan Manuel Santos alihusika na jaribio hilo.
Rais huyo wa Venezuela awali ameilaumu Marekani kwa kupanga kumuua lakini hajatoa ushahidi kuhusu hilo.
Serikali ya Colombia imekanusha kuhusika ikisema hakuna ushahidi kwa madai yake Maduro.