Rais Nicolas Maduro wa Venezuela Anusurika Kuuawa

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela Anusurika Kuuawa

Of course. Pata picha Venezuela ndo wanashika namba 5 kwa ku export crude oil,kwenda Kwa Trump.

Na kwa Europe ni exporter namba 3 baada ya Marekani na China wa bidhaa zake.

Lazima wampangie mkakati wa kum destabilize wajinyakulie chao mapemaaaa.😕😕
Ehhh Mola tusaidie walahi!
 
Dah! Nawaonea huruma Venezuela na mikakati michafu ya wale washikaji
Nalog off
 
Ni vile hatuoni upande wa pili.

Huenda huyo aliyeendesha hilo zoezi saa hizi anakula vichambo, kama sio vifuti kwa kukosa target.
 
Hawa madikteta hakika watapata tabu sana. Maduro anafikiri ubabe unalipa na mara ya tatu hatapona, ataenda kuungana na Hugo Chavez.

Huwezi wewe unakula bata ikulu huku wengine wakifa na "Hyperinflation" uliyosababisha wewe.

Hutakuwa salama hata ulindwe na makomandoo milioni kumi. Ni yale yale yaliyompata "The biblical Saul". Atubu na amrejee Mungu.
 
Rais Nicolas Maduro anusurika kuuwawa

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameapa kuhakikisha kuwa sheria inachukua mkondo wake baada ya jaribio linalodaiwa kufanyika dhidi ya maisha yake ambalo anasema limeamriwa na rais wa Colombia Juan Manuel Santos.







"Naahidi kuchukua hatua za kisheria, kwa yeyote atakayekuwa, baada ya shambulio hilo la kihalifu lililoamriwa kutoka Bogota," aliandika katika maandishi mfululizo katika ukurasa wa Twitter.


Rais Nicolas Maduro(katikati) na mkewe Cilia Flores wakiangalia juu ambako kulitokea ndege hizo zisizo na rubani

Pia amesema anadhamira kuu zaidi kuliko huko ilivyokuwa huko nyuma " kuimarisha amani, utulivu, maendeleo na ustawi" na kwamba na hii ni kutokana na "shukurani kwa ngao ya wananchi na baraka za Mwenyezi Mungu ambapo aliondoka bila ya kuathirika."

Ndege zisizokuwa na rubani zikiwa na miripuko ziliripuka karibu na rais wa Venezuela Nicolas Maduro katika jaribio la kutaka kumuua ambalo lilitokea wakati akitoa hotuba kwa maelfu ya wanajeshi ambayo ilikuwa inatoka moja kwa moja katika televisheni, maafisa wamesema.

Ilikuwa bila kutarajiwa katika ya hotuba yake, Maduro na mke wake, Cilia Flores, waliangalia hewani katika mawingu na kukunja uso baada ya kusikia milio ya miripuko ikipasua anga.

"Hili lilikuwa jaribio la kutaka kuniua," alisema baadaye alipolielezea tukio hilo. "Leo walijaribu kuniuwa."


Mwanajeshi akitoka damu kichwani baada ya kujeruhiwa na mripuko

Waziri wa habari Jorge Rodriguez alisema tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya saa 11.30 jioni saa za Venezuela , wakati Maduro alikuwa akisherehekea siku ya jeshi la taifa. Kiongozi huyo wa taifa ambaye alionekana dhahiri kuingiwa woga alisema aliona "kitu kinaruka angani " ambacho ´kiliripuka mbele ya macho yake. Alidhani huenda ni kitu kwa ajili ya maonesho kwa heshima ya tukio hilo.

Miripuko

Katika muda wa sekunde kadhaa, Maduro alisema alisikia mripuko wa pili na mtafaruku ulifuatia. Walinzi wake walimuondoa Maduro kutoka katika mahali hapo na picha za televisheni zilionesha wanajeshi waliokuwa katika sare za jeshi wakisimama katika utaratibu fulani haraka wakitawanyika kutoka katika eneo hilo.

Alisema , "kundi la mrengo wa kulia" likifanyakazi kwa uratibu na wapinzani mjini Bogota na Miami, ikiwa ni pamoja na rais wa Colombia Juan Mnuel Santos, wanahusika. Baadhi ya "wale waliotoa baadhi ya vifaa " vilivyotumika katika shambulio hilo tayari wameshakamatwa.

"Uchunguzi utafanyika kubaini kiini cha shambulio hilo," amesema. "Bila kujali nani ataanguka."


Wanajeshi wakikagua jengo la karibu na tukio baada ya kutokea mripuko

Serikali ya Venezuela mara kwa mara inawashutumu wanaharakati wa upinzani kwa kupanga mashambulizi na kumuongusha rais Maduro kutoka madarakani, rais ambaye si maarufu kabisa kwa umma wa nchi hiyo ambaye alichaguliwa tena hivi karibuni kuanza muhula mpya madarakani hatua inayopingwa na mataifa mengi. Maduro amechukua hatua ya kuimarisha madaraka yake wakati taifa hilo linakabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi.

Katika hatua ya maandamano ya karibu kila siku mwaka jana, ofisa muasi wa polisi alirusha helikopta iliyoibiwa katika mji mkuu na kuvurumusha maguruneti katika majengo kadhaa ya serikali. Oscar Perez baadaye aliuwawa katika mapambano makali ya silaha.

Mwanasheria mkuu wa serikali Tarek William Saab alisema jaribio hilo la mauaji halikumlenga Maduro pekee, bali viongozi wote wakuu wa jeshi waliokuwapo pamoja na rais.


Wanajeshi wa Venezuela wakitawanyika baada ya kutokea miripuko wakati wa maadhimisho ya jeshi la nchi hiyo

Kundi lisilojulikana la waasi ambalo linajengwa na raia wa Venezuela na wanajeshi lilidai kuhusika na shambulio hilo la kutaka kumuua rais Nicolas Maduro, kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika mtandao wa kijamii. "Ni kinyume na hadhi ya jeshi kuwalinda watu katika serikali ambao hawakusahau tu katiba , lakini pia ambao wamefanya ofisi za umma kuwa ni fursa ya kujitajirisha," kundi hilo limesema.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape

Mhariri: Isaac Gamba
 
Yaani inafika mahali ni kuombea amani tu katika nchi ndogo zenye utajiri mkubwa maana mdhungu ndio anaziwinda kama simba.
Ni kuomba" ulinzi wa" kimungu" tu walahi!
ulinzi" wa" kimungu" utatoka wapi" dada Yangu",wakati kila kukicha "hayo "mabepari yanapora rasilimali na kusabbisha" mauaji" kwa "watu " lakini mungu anawaangalia tu""daaah USA sijui wakoje''? aisee..wanaroho ya kichawi mnoo
 
USA inataka kuweka kiongozi wake Venezuela.. si waache tu watu na nchi yao bana.
 
Back
Top Bottom