Rais Nyerere na mkewe kwenye mazishi ya Indira Gandhi

Swali ni Swali mkuu, wengine hatujafungua video sasa tunataka kujua nini kilimuua nikaona anasema walimchoma moto nikauliza ndio akafa?
Kweli una haki ya kuuliza
Indira Gandhi alikuwa Waziri mkuu wa India
Aliuwawa na bodyguard wake nyumbani

Mtoto wake Sanjay ambae ndio alikuwa anategemewa kuwa Waziri mkuu baada ya mama yake nae akafa kwenye ajali ya ndege mwaka 1980

Baada ya hapo mtoto wake mwingine anaeitwa Rajiv Gandhi akaja kuwa Waziri mkuu nae akauwawa 1991
Familia ikawa imeisha kwenye utawala hapo
Inahuzunisha historia yao
 
Hii kweli inahuzunisha ingawa nahisi Mzee wangu alishawahi kunisimulia hii
 
Kuna mtaa wa Indira Gandhi maeneo ya posta right?
Baada ya Indira Gandhi kuuwawa, jioni ya siku hiyo hiyo, aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es salaam Kitwana Kondo alitangaza kubadirisha jina la mtaa wa Market na kuitwa Indira Gandhi.
Mtaa umeanzia Sofia Kawawa (zamani Lindi st) umeishia kwenye round about ya mitaa ya Makunganya na India.
Hii ni katika kuenzi urafiki wa nchi mbili hizi.
Mchana wa siku hiyo gazeti la Uhuru lilitoa kopy (chapisho lingine baada ya lile rasmi la asubuhi) lenye front page iliyomuhusu Indira Gandhi tu, kuhusu sababu za kifo chake na historia yake fupi.
 
Indira Gandhi aliwafanyia ugangwe wa kiserikali masingasinga kwenye msikiti wao mtakatifu kabisa kwa imani yao, huku yeye mwenyewe akiwa na walinzi masingasinga, akiamini kuwa wale walinzi wake ni waaminifu sana, hawatamdhuru.

Wakamuua.

Hili jambo nililifikiria sana wiki chache zilizopita nilivyoona viongozi wetu wanalindwa na walinzi wenye silaha nzito nyingi.

Nikajiuliza, hivi siku mmoja wa hawa walinzi wakikasirishwa na jambo, wakaamua kummiminia risasi kiongozi, itakuwaje?

Hawa viongozi wanajiamini nini?

Hata Indira Gandhi naye alijiamini hivyo hivyo.
 
Aisee.... R. I. P Nyerere......
 
Aseeh upo sahihi nimekumbuks pia makunganya street..... Unajua history na Jiji la mzizima vzr
 
What’s your point, exactly?
 
Laurent Kabila naye aliuliwa na mmoja wa walinzi wake!

Baada ya operesheni ya kijeshi aliyoiamuru Indira Gandhi kumalizika, alishauriwa kuwa aachane na walinzi wake ambao walikuwa masinga singa. Akakataa kuachana nao kwa sababu alikuwa anawaamini. Akaishia kuuliwa.

Mambo ya ulinzi wa viongozi yanategemea imani na uaminifu wa hali ya juu sana.

Wakati mwingine huwa nahisi huenda hata wao kwa wao huwa wanaangaliana kwa umakini sana endapo mmoja wao au baadhi yao watakuwa rogue na kumdhuru wanayemlinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…