Rais Omary al Bashir wa Sudan alipinduliwa kwa ongezeko la bei ya mkate, Watanzania tunachekelea Serikali kuongeza kodi lukuki

Rais Omary al Bashir wa Sudan alipinduliwa kwa ongezeko la bei ya mkate, Watanzania tunachekelea Serikali kuongeza kodi lukuki

Yani huwezi elewa hata kidogo, Zambia (a land locked country) ambao mzigo wao unapitia kwetu , bei ya mafuta ipo chini kuliko Tanzania.
Leo nimeshuhudia magari ya Tanzania pale Tunduma yameongozana kwenda Nakonde Zambia kujaza mafuta!

Aibu!
 
Hivi serikali inapowafanyia ujambazi na unyang'anyi wananchi wake, wakimbilie wapi?
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana sijui ni sababu ya upole na unyenyekevu au uoga! La sivyo wako katika lindi la ujinga!

Mwaka 2019 wananchi wa Sudan waliiondoa serikali ya Rais Omary al Bashir kwa kuongeza bei ya mkate kwa kufanya maandamano nchi nzima. Walifanikiwa na sasa Bashir anatumikia kifungo jela kwa ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Watanzania tumeongezewa kodi lukuki zingine zikipewa majina ya ajabu kama kodi za mshikamano sijui kodi za uzalendo nk, tumebaki tunanung'unika kimoyo moyo! Kodi ya miamala imepanda, bei ya mbolea imepanda, nauli za usafiri na usafirishaji zimepanda, bei ya mafuta imepanda lakini tunashindwa kuihoji serikali yetu tumebaki tunapiga makelele kama wehu!

Wakati huo huo serikali inapanga kujenga sanamu ya mabilioni ya fedha, gharama za kuendesha serikali inazidi kupanda kutokana na ukubwa wa serikali, ufujaji wa fedha za umma na ufisadi. Aidha serikali inazidi kukopa fedha kwa matumizi yale yale ambayo serikali inakusudia kutumia fedha za kodi mpya!

Watanzania tumebaki kukodoa macho kama vile hatuoni kinachoendelea na hakituhusu! Nani huyu aliyeturonga na kuzaliwa na udumavu wa akili? Kuna matumizi mabaya sana ya madaraka viongozi wetu wanafanya lakini tunashindwa kuwawajibisha!

Watanzania tuamke vinginevyo twafwa!
lolote litakalo tokea wa kulaumiwa ni .
1. Mwigulu
2. Zungu
3. Jerry Muro.
 
IMG-20210716-WA0180.jpg
 
Na sisi wakija kwenye ziara zao tuwapige mawe au sio?
 
Back
Top Bottom