Tetesi: Rais Paul Kagame kufunguliwa mashitaka The Hague kwa uhalifu nchini Congo DRC

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari za siri zimeanza kuvuja kuwa Kagame kageukwa na wazungu.

Leo mwendesha mashitaka wa mahakama ya ICC ameanza uchunguzi wa uhalifu wa kivita mashariki mwa Congo.

Inadaiwa mlengwa sio mwingine bali ni Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Tusubiri tuone kama watafanikiwa kumnasa Chuma cha Pua.
 
Ni ukatili wa kutisha wamama na watoto wanazikwa wakiwa hai

Huu Umoja wa Africa ulishajifia zamani sana waliopo ni kuvimbisha matumbo tu
Inadaiwa ktk taarifa za siri kuwa Wakongoman millions 6 wamepoteza maisha kwa athari za vita anavyopigana Kagame kwa mgongo wa waasi. Wengi kwa njaa, magonjwa na vita vyenyewe.
 
Wanataka kumpaisha tu
 
About time..
 
umoja wa afrika uwe na RAIS wake ,wasiwe hawa wahuni kubadilishana uenyekiti kilamwaka
 
Safi sana, hili liuuaji linatakiwa kunyonywa na sio kufungwa!
Huyu ndie aliongoza kumuua yule Raisi hadi machufuko ya kimbari yakaanza.
Huyu kaua wenzake wa RPF aliopigana nao bega kwa bega kuingia Ikulu.
Huyu amesababisha vifo vya wengi na mateso makubwa mashariki mwa DRC
Akamatwe, ashitakiwe, anyongwe hadi kufa.
 
Ni ukatili wa kutisha wamama na watoto wanazikwa wakiwa hai

Huu Umoja wa Africa ulishajifia zamani sana waliopo ni kuvimbisha matumbo tu
Malema wa SA aliishaga wahi kusema, "AU? There is no such a thing, is a group of old people who protect each other, is a club, they don't discuss issues, they don't challenge each other, my brother you are wrong here, you were wrong there..." ndio maana Magufuli hadi anafariki dunia, hakuwahi kwenda kijiweni kwao!
 
Alipokuwa anawavushia madini ya damu toka DRC hawakumuona kama mhalifu, leo hii kawa mbaya kwao?
 
Na hayo makanisa ya kikatoliki aliyofunga, huenda Vatican inamjibu.
Hamna lolote wanaloweza wakamfanya huyo jamaa........upepo umeshabadilika.....,,,mzee katulia zake msumbiji anawatuliza magaidi na EU wanampa support, kwahio kutegemea jamaa atapelekwa huko ICC ni ndoto
 
Wakimaliza nayeee wahamiage lile litaifa la kijaaanii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…