Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Rais Vladimir Putin akitia saini amri (the Decree) kutambua majimbo ya Donestk na Luhansk kuwa majimbo huru. Picha na Reuters.
Rais wa Russia Vladimir Putin usiku huu anatarajiwa kutangaza majimbo ya Donetsk na Luhansk kama majimbo huru.
Majimbo haya mawili yaliyo upande wa Mashariki mwa Russia, ndiyo kiini cha mzozo unaoendelea unaozihusu nchi za Ukraine, NATO, Russia, Marekani na nchi za Magharibi.
Pia Rais Putin atasaini amri (decree) ya kutambua eneo zima lijulikanalo kama Donbass kama eneo la Russia.
Baada ya kutangaza uamuzi huo wa Russia, kiongozi huyo wa Russia ataamuru majeshi ya Russia kuingia katika majimbo hayo ili kulinda maslahi ya Russia kiusalama na kijeshi.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ameitisha kikao cha dharura cha umoja wa mataifa ambapo suala la uamuzi wa Russia kutambua majimbo ya Donetski na Luhansk litajadiliwa.
Wakati huohuo, Russia imeitisha kikao cha dharura umoja wa mataifa kujadili suala la Ukraine baada ya mkuu wa majeshi ya Russia kusema kwamba Ukraine imeweka majeshi yapatayo 60,000 katika eneo la Donbass.
Putin anadai kwamba kiongozi wa iliokuwa USSR, Lenin alifanya maamuzi ya kimakosa katika kuangalia mipaka ya USSR na ndiyo kiini cha matatizo ya leo hii.