Rais Putin kutangaza usiku huu Russia kutambua rasmi majimbo huru yaliyojitenga ya Donetski na Luhansk

hizo hizo mzee baba kumbukuka bomber inategemea flares so haina manuva
 
Nimesema mkataba uwekwe hadharani ili dunia iuone. Dunia ikishauona, humu JF utafika pia!

Walipewa ahadi bila mkataba?!

Makubaliano katika masuala mbalimbali na muhimu ya kimataifa kama suala hilo huwa hayaishii kwenye mazungumzo bila ya mkataba.

Putin anajaribu kushawishi watu hasa umma wa Warusi kuwa kulikuwa na makubaliano hayo, lakini anazungumza maneno matupu. Kama huo mkataba ungekuwepo, unafikiri kungekuwa na haja ya kushawishi watu kwa maneno tu?

Tunawezaje kuamini maneno matupu tu kwamba kulikuwa na makubaliano, kwamba Urusi iliomba [rasmi] kujiunga NATO mwaka 2000? Haya ni masuala ya kuzungumza tu kwenye media bila ya backup ya uthibitisho?

Hilo suala la Urusi kujiunga NATO liliwahi kuibuliwa miaka ya nyuma na huyuhuyu Vladimir Putin kwenye interview na vyombo vya habari, ni vile tu watu huwa hamfuatilii taarifa vizuri.

Kwa maneno yake mwenyewe, aliwahi kusema kuwa Clinton alikubali hilo pendekezo la Urusi kujiunga na NATO ingawa halikuwa ombi rasmi kwa sababu suala la kujiunga NATO lina mchakato mrefu sana. Leo akisema kuwa hakujibiwa, tuamini lipi? Na tumuamini Putin yupi? Huyu wa jana ama wa hapo kabla?!
 
Kuhusu Nato nilimponda USA.Leo nimemponda Putin kwa kutambua sehemu ya Ukraine ambao ni pro Russia kama sehemu huru.Mimi sina upande. Ukitaka ujadili vizuri hawa mataifa wawili ni vyema kutokuwa na upande maana wote ni wapumbavu.
Mkuu siuende kwenye jukwaa la mapishi na mapenzi la wanawake wenzako na makolo
 
Putin anajua kucheza na maneno kuhalalisha misimamo yake,watu humu wanamuona kama Mungu mtu,kwamba kila anachokisema kuhusu west ni sahihi,...
Ila wajue tu Putin amesha set precedence,kesho tusishangae kusikia China ameivamia Taiwan kimabavu au marekani imeivamia Cuba far same same reason,....security concern...
 
Marekani alishaanza uvamizi miaka mingi, kusema Putin katengeneza precedence ni uongo.
Marekani kavamia, Iraq, Afghan, Libya na kwingine.
 
On 27 May 1997, at the NATO Summit in Paris, France, NATO and Russia signed the Founding Act on Mutual Relations, Cooperation and Security, a road map for would-be NATO-Russia cooperation. ... NATO said it had no plans to station nuclear weapons in the new member states or send in new permanent military forces.

Putin hakuwa na mpango wakujiunga na NATO alionya waache kuendelea kujitanua East kumwambia Clinton ilikuwa kuona nia yake ni nini? Russia hawezi kukubali maadui zake waje wawekeze black sea kwa visingizio Ukraine ni NATO. Shida ya yote haya ni Ukraine kutaka kujiunga na NATO kwa maneno ya Putin jana kasema aliambiwa na nchi za NATO kuwa asiwe na wasiwasi hili jambo sio la kesho akawajibu na baada ya kesho? Ni sawa na Russia wakaweke jeshi lao Mexico unadhani USA atakubali? NATO ni jambo jepesi tu ni kusema NATO tuko salama na Russia wako salama wala hatuna haja ya wanachama wapya huko EAST tukae kwa amani lakini wewe kila siku unamsogelea mwenzako tu kwa kisingizio cha kulinda amani zenu ila yeye hana haki ya kulinda nchi yake.
 
Hamna raia anaweza kukaa kwenye maeneo ya mapambano ya kivita. Tutengeneze kuona wakimbizi wakielekea nchi nyingine tena zile zilizokuwa kwenye USSR.
Mpaka sasa Russia hawajapata upinzani wowote toka ukraine.

Nadhani hayo maeneo yalioyokaliwa ya luhansky na donesky ndio maeneo yaliyo na vinu vya nyuklia.
 
Putin ni mbabe wa dunia, Wamagharibi watabaki wanabwekabweka tu.
Watabweka wanyonge wa Urusi kwani shares zinaanguka vibaya juzi Tu paketi ya maziwa ilikuwa rubel 50 ,Jana 60 sijui leo itafika ngapi.
Wazee wenye nchi hawajali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…