Nimesema mkataba uwekwe hadharani ili dunia iuone. Dunia ikishauona, humu JF utafika pia!
Walipewa ahadi bila mkataba?!
Makubaliano katika masuala mbalimbali na muhimu ya kimataifa kama suala hilo huwa hayaishii kwenye mazungumzo bila ya mkataba.
Putin anajaribu kushawishi watu hasa umma wa Warusi kuwa kulikuwa na makubaliano hayo, lakini anazungumza maneno matupu. Kama huo mkataba ungekuwepo, unafikiri kungekuwa na haja ya kushawishi watu kwa maneno tu?
Tunawezaje kuamini maneno matupu tu kwamba kulikuwa na makubaliano, kwamba Urusi iliomba [rasmi] kujiunga NATO mwaka 2000? Haya ni masuala ya kuzungumza tu kwenye media bila ya backup ya uthibitisho?
Hilo suala la Urusi kujiunga NATO liliwahi kuibuliwa miaka ya nyuma na huyuhuyu Vladimir Putin kwenye interview na vyombo vya habari, ni vile tu watu huwa hamfuatilii taarifa vizuri.
Kwa maneno yake mwenyewe, aliwahi kusema kuwa Clinton alikubali hilo pendekezo la Urusi kujiunga na NATO ingawa halikuwa ombi rasmi kwa sababu suala la kujiunga NATO lina mchakato mrefu sana. Leo akisema kuwa hakujibiwa, tuamini lipi? Na tumuamini Putin yupi? Huyu wa jana ama wa hapo kabla?!