Ukraine ethnicity hawataki kuwa upande wa Russia sababu hawaoni faida yake,inekuwa wanataka kuwa upande wa Russia kama watu humu wanavyotaka kutuaminisha,ile Kyiv ingeshachafuka siku nyingi,Russia wanajua weak point ya Ukraine ni ule upande wa East penye Russian ethnicity wengi na ndio wanaoi support Urusi,Siku Russia akirogwa akaivamia Kyiv ndio vita pale itakuwa mbaya sana maana hadi sasa kila raia wa Ukraine amepewa bunduki na kuwa trained kuilinda nchi yao,hiyo vita itakuwa mbaya sana na watu watakufa wengi mno kitu ambacho hata Putin mwenyewe nina uhakika hatotaka kitokee maana hata raia wake wengi hawaungi mkono kuivamia kijeshi Ukraine...
Ukraine kama nchi na raia wake wanataka kuwa upande wa magharibi hao wengine wanaojitenga ni ethnicity inawasumbua to nothing else...
Ukraine ni lost territory na Russia wataichukua ikiwa wataingia Kyiv kupitia ardhini, majini na hewani -land sea and air invasion.
Hivi sasa wameweka kitu chaitwa corridor au springboard yaani eneo maalum la kupita kuingia rasmi ndani zaidi ya eneo la Donbass.
Upo sahihi majeshi ya Ukraine yapo sawasawa yanasubiri na itakuwa vita kwelikweli na wengi raia wa Ukraine watapoteza maisha.
Putin sio mjinga amepanga hii mavitu tangu 2020 na Marekani wanafahamu hilo kupitia CIA na majasusi wa NATO.
Akifanikiwa next, regime change na kumuondoa Zelensky, kumbuka jana amesema serikali ya sasa ya Ukraine ni ya vibaraka na wameifanya Ukraine koloni la Marekani.
Baada ya hapo kuna kitu chaitwa "incorporate lost territory".
Mwisho Ukraine itakuwa kama Crimea.
Mimi sipendi vita ila napenda kuona haki sawa na kwamba hizi vita za kijiografia ili mataifa makubwa kujiweka sawa zina ulazima endapo taifa jingine latumia hila dhidi ya taifa jingine.
NATO, West na Marekani lazima waiheshimu Russia kama ni superpower na ana mabomu ya nyuklia pamoja na kiti cha kudumu UN.
Pia Russia ana kura ya Veto UN hivyo jaribio lolote la kuishinikiza kuhusu masuala yoyote yanotishia usalama wake atapinga.