Rais Putin kutangaza usiku huu Russia kutambua rasmi majimbo huru yaliyojitenga ya Donetski na Luhansk

Rais Putin kutangaza usiku huu Russia kutambua rasmi majimbo huru yaliyojitenga ya Donetski na Luhansk

Yaani Ukraine yenyewe ipo kama haipo, vurugu zinaendelea juu yake lakini wenyewe na viongozi wao wala hawajitisiki kusema chochote , imezubaa kama raia wa Tanzania.
Ukraine inaonekana kama underdog katika hili. Inapigana 'defensive war' na wala haihitaji kuzungumza kila kitu. Hata wizara yao ya ulinzi imetoa agizo kwa raia kutoweka mitandaoni picha zinazoonesha mienendo ya majeshi yao.
 
kitu kinachochekesha ni sie wa Africa kushabikia na kusifia upuuzi ooh sijui Mwanaume kasogeza kete dume, ohh wapigabe sasa, sijui nani akiwashe wapewe kichapo, wakati inajulikana fika hata likitokea la kutokea ukiacha wananchi wa nchi hizo husika kutaabika na hiyo vita, next itakua ni sisi wa Africa hata kama vita hiyo haitapiganiwa huku Africa...

hekima na busara ndio inatakiwa kutumika zaidi ya ubabe wa hizi 2 super powers ambazo zinaonyesha fika greedy ya next level..

amazing thing ni kuwa nchi kama China iko kimyaaa kwenye haya wakati yeye ni amongst majirani wakaribu kabisaaa
China wanafuatilia kwa makini na suala la usalama wao linalingana na kisiwa cha Taiwan.

Hivyo China hawawezi kuongea sana kwenye hili ila kama wafuatilia hizi taarifa, ni kwamba Putin juzijuzi alikwenda China kuongea na Xi Jingping.

China itakachofanya ni kuogpopa kuikosoa waziwazi Russia kuivamia Ukraine lakini hapohapo ikionyesha kuunga mkono misingi ya kuheshimu mipaka na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi.

Hapo kwa lugha ingine ni kwamba China anaongelea Taiwan pia kwamba ikifanya mchezo (wa kukaribisha maadui wa China sebuleni kwake) itafanyiziwa.
 
Yale yale ya Hitler.Putin atatumbukiza dunia kwenye mfarakano wa kutisha . Putin is Hitler reincanated.
Achana na propaganda za nchi za magharibi.

Kama ulisoma historia hutakosa topic ya The Rise of Hitler na kisha kuna ile topic ya Hitler most military blunders.

Putin hii game alipanga tangu 2020 wafahamu hiyo?

Na hata jana wanasema ile hutba yake ilikuwa imerekodiwa kitambo na kilichifanyika ni umaliziaji tu wa shughuli.

Ila kuibuka kwa Putin ni unique na well calculated na hakuna aleiona hiyo.

Lakini Putin si Hitler.
 
Exactly tatizo Russia has nothing to offer in economy ndo changamoto kubwa aliyokua nayo

Putin ni moja wa kiongozi wa ajabu sana yaan Russia ni kubwa sana aachen petty issues, hakuna muwekezaji atakae wekeza Crimea au donbass sababu kumushawekewa vikwazo baada ya mda uchumi utacollapse anachofanya Putin ni ujinga

Putin apambane gdp ikue ndo njia rais ya yeye kuwa na ushawishi
Mkuu, jaribu sana kutoingiza ushabiki kwenye masuala yenye kuchangamsha akili kama haya.

Hivi, waifahamu GDP ya Russia kwa sasa imesimama vipi?
 
Marekani na washirika wake alikuwa wanabwaka kila siku mara oooh watampa kipigo cha mbwa koko Putin akivaamia Ukraine sasa wameufyata.

Toka Dume la Mbegu litoe tamko na kuingia kazini bado wanatafakari cha kufanya.

Ni dhahiri walikuwa wanapima upepo. Sasa hivi hakuna taifa linaloitwa Ukraine kwasababu limegawanyika tayari, kitendo cha Putin kuingia kule bila hata upinzani kinaonyesha ushindi mkubwa sana.

Rais kigaragosi wa Magharibi kulihutubia taifa kwa kulilia msaada ni ushahidi kwamba tayari amesoma alama za nyakati na kugundua wamemuuza.

Ni masaa mangapi toka Putin afanye maamuzi? Marekani na washirika wake eti wanaitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama ambapo mwenyekiti wake ni Urusi? Hahahahahahahaah

Wanaishia kulaani na kupinga ila hawana jeuri ya kufanya lolote. Walitarajia Mchina atamkana Putin ila ndo hivyo katika tamko la Balozi wa Uchina kwenye Baraza la Usalama, hajaonyesha kuchukua msimamo mkali dhidi ya hatua ya Putin. Tayari Hiyo ni ishara kwamba wanamuunga mkono.

Marekani hana jeuri ya kumpiga Putin. Wao wataumia zaidi ya Putin. Tayari Russia ina access ya Marekani kupitia Cuba, akileta nyoko zake Putin atamnyoosha huko huko.
 
Unaishi urusi au umeangalia kwa glogloo.

Nimeangalia TV ya Urusi. Ziko nyingi tv Urusi. Kama unafahamu kirusi , angalia au Kama Una mtu Urusi mpigie simu atakuambia maisha yalivyoanza kuwa magumu
 
Mkuu, jaribu sana kutoingiza ushabiki kwenye masuala yenye kuchangamsha akili kama haya.

Hivi, waifahamu GDP ya Russia kwa sasa imesimama vipi?
Urusi mkuu vyuma vinakaza , Putin ni Jiwe kafufuka Urusi
 
Marekani na washirika wake alikuwa wanabwaka kila siku mara oooh watampa kipigo cha mbwa koko Putin akivaamia Ukraine sasa wameufyata.

Toka Dume la Mbegu litoe tamko na kuingia kazini bado wanatafakari cha kufanya.

Ni dhahiri walikuwa wanapima upepo. Sasa hivi hakuna taifa linaloitwa Ukraine kwasababu limegawanyika tayari, kitendo cha Putin kuingia kule bila hata upinzani kinaonyesha ushindi mkubwa sana.

Rais kigaragosi wa Magharibi kulihutubia taifa kwa kulilia msaada ni ushahidi kwamba tayari amesoma alama za nyakati na kugundua wamemuuza.

Ni masaa mangapi toka Putin afanye maamuzi? Marekani na washirika wake eti wanaitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama ambapo mwenyekiti wake ni Urusi? Hahahahahahahaah

Wanaishia kulaani na kupinga ila hawana jeuri ya kufanya lolote. Walitarajia Mchina atamkana Putin ila ndo hivyo katika tamko la Balozi wa Uchina kwenye Baraza la Usalama, hajaonyesha kuchukua msimamo mkali dhidi ya hatua ya Putin. Tayari Hiyo ni ishara kwamba wanamuunga mkono.

Marekani hana jeuri ya kumpiga Putin. Wao wataumia zaidi ya Putin. Tayari Russia ina access ya Marekani kupitia Cuba, akileta nyoko zake Putin atamnyoosha huko huko.

Mkuu Putin ataangushwa na warusi wenyewe. West hawana haraka
 
Je kama Putin amesaini mkataba wa kuyatambua hayo majimbo, Ukraine bado inasubiri nini kuwa mwanachama wa NATO au NATO wanasubiri nini kutompa uanachama Ukraine? , hebu wataalamu wa geopolitics mnidadavulie hapa.
 
Ukraine ethnicity hawataki kuwa upande wa Russia sababu hawaoni faida yake,inekuwa wanataka kuwa upande wa Russia kama watu humu wanavyotaka kutuaminisha,ile Kyiv ingeshachafuka siku nyingi,Russia wanajua weak point ya Ukraine ni ule upande wa East penye Russian ethnicity wengi na ndio wanaoi support Urusi,Siku Russia akirogwa akaivamia Kyiv ndio vita pale itakuwa mbaya sana maana hadi sasa kila raia wa Ukraine amepewa bunduki na kuwa trained kuilinda nchi yao,hiyo vita itakuwa mbaya sana na watu watakufa wengi mno kitu ambacho hata Putin mwenyewe nina uhakika hatotaka kitokee maana hata raia wake wengi hawaungi mkono kuivamia kijeshi Ukraine...
Ukraine kama nchi na raia wake wanataka kuwa upande wa magharibi hao wengine wanaojitenga ni ethnicity inawasumbua to nothing else...
Ukraine ni lost territory na Russia wataichukua ikiwa wataingia Kyiv kupitia ardhini, majini na hewani -land sea and air invasion.

Hivi sasa wameweka kitu chaitwa corridor au springboard yaani eneo maalum la kupita kuingia rasmi ndani zaidi ya eneo la Donbass.

Upo sahihi majeshi ya Ukraine yapo sawasawa yanasubiri na itakuwa vita kwelikweli na wengi raia wa Ukraine watapoteza maisha.

Putin sio mjinga amepanga hii mavitu tangu 2020 na Marekani wanafahamu hilo kupitia CIA na majasusi wa NATO.

Akifanikiwa next, regime change na kumuondoa Zelensky, kumbuka jana amesema serikali ya sasa ya Ukraine ni ya vibaraka na wameifanya Ukraine koloni la Marekani.

Baada ya hapo kuna kitu chaitwa "incorporate lost territory".

Mwisho Ukraine itakuwa kama Crimea.

Mimi sipendi vita ila napenda kuona haki sawa na kwamba hizi vita za kijiografia ili mataifa makubwa kujiweka sawa zina ulazima endapo taifa jingine latumia hila dhidi ya taifa jingine.

NATO, West na Marekani lazima waiheshimu Russia kama ni superpower na ana mabomu ya nyuklia pamoja na kiti cha kudumu UN.

Pia Russia ana kura ya Veto UN hivyo jaribio lolote la kuishinikiza kuhusu masuala yoyote yanotishia usalama wake atapinga.
 
Je kama Putin amesaini mkataba wa kuyatambua hayo majimbo, Ukraine bado inasubiri nini kuwa mwanachama wa NATO au NATO wanasubiri nini kutompa uanachama Ukraine? , hebu wataalamu wa geopolitics mnidadavulie hapa.

Haya mambo hayana haraka hivyo Kama tunavyofikiria. Hata Zanzibar ilichukua miezi 4 kwa Tanganyika kutangaza muungano, ingawa jeshi lake lilikuwepo kuanzia day one
 
Je kama Putin amesaini mkataba wa kuyatambua hayo majimbo, Ukraine bado inasubiri nini kuwa mwanachama wa NATO au NATO wanasubiri nini kutompa uanachama Ukraine? , hebu wataalamu wa geopolitics mnidadavulie hapa.
Kuna masuala mengi Ukraine inabidi iyapitie ili iweze kuingizwa NATO mojawapo ni vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Pili, hilo jambo (kujiunga na NATO) si la kuamka asubuhi basi weye ni NATO member kuna masharti mengine kadhaa ambayo nchi hutakiwa kuyafaulu.

Mwisho ni katazo la Russia ambalo NATO imeshindwa kulitimiza kwamba Ukraine isiingizwe NATO na Putin kuona kuna upenyo ndi kachukua hatua hiyo kuivamia Ukraine.

Hivyo sasa hivi NATO hawawezi kuisaidia Ukraine ikivamiwa kwani si mwanachama wake.

Ila imewasaidia tu vifaa vya kivita na mafunzo maalum ambayo Russia imeyaona na imeyachambua.
 
Mkuu Putin ataangushwa na warusi wenyewe. West hawana haraka

Ukraine siyo mwanachama wa NATO hivyo Ulaya na Marekani hawawezi kuingia vitani.

Ili kujiunga na NATO, kuna utaratibu maalumu ikiwemo kura ya maoni, bunge kujadili na mambo mengine. Ina maana siyo jambo la kufanyika kwa haraka.

Sahau NATO kwa sasa.
 
Urusi mkuu vyuma vinakaza , Putin ni Jiwe kafufuka Urusi
Uchumi wa Russia kwa mujibu wa WIKIPEDIA.

1. Russia ni nchi ya 11 kwa uchumi mkubwa duniani kwenye GDP na PPP.

2. GDP - sekta ya huduma ni 62%, sekta ya viwanda 32% na sekta ya kilimo ni 5% na watu wasoajiriwa ni 4.3%

3. Akaunti ya fedha za kigeni ni bilioni 638 na ni ya 4 kwa ukubwa huo duniani.

4. Wafanyakazi au "labour force" ni milioni 70 na inaifanya Russia kuwa ya 6 duniani.

5. Russia ni ya 10 duniani kwa utengenezaji magari.

6. Russia ni moja ya nchi duniani zenye madeni madogo sana.

7. Russia ni nchi ya 20 duniani kwa uingizaji na usafirishaji bidhaa duniani.
 
Je kama Putin amesaini mkataba wa kuyatambua hayo majimbo, Ukraine bado inasubiri nini kuwa mwanachama wa NATO au NATO wanasubiri nini kutompa uanachama Ukraine? , hebu wataalamu wa geopolitics mnidadavulie hapa.
Kuupata uanachama wa NATO huwa ni mchakato mrefu. Kwanza kuna vigezo kadhaa ambavyo lazima nchi husika iwe imekidhi vigezo hivyo. Pia, lazima kuwe na makubaliano ya pamoja (consensus) ya wanachama wote waliopo ndani ya jumuiya hiyo.

Nchi wanachama zitaendesha mchakato maalumu wa kukubaliana na ombi hilo la uanachama kutoka kwa nchi husika. Mfano; kwa Marekani, mchakato utahusisha bunge (congress) pia. Nchi zingine zitafanya mchakato huo pia baada ya kupitia katika vyombo vyao vya maamuzi.

Moja ya vigezo vya kupewa uanachama ni nchi husika kutokuwa na migogoro hasa ya kimipaka inayoweza kuchochea nchi kugawanyika. Hili ndilo linalosababisha baadhi ya nchi za NATO kama Ujerumani na Ufaransa kutilia mkazo kuwa Ukraine haistahili kupewa uanachama kwa sasa mpaka hapo baadaye.

Ukraine kwa sasa imewekwa katika mpango maalumu wa NATO wenye nchi sita unaofahamika kama Enhanced Opportunities Partnership (EOP) kama mpango maalumu wa ushirikiano wa karibu baina ya NATO na Ukraine pamoja na baadhi ya nchi zingine.
 
Ok mkuu weye endelea kuamini hivyo.

Ila Russia muziki wake USA hauwezi.

Alifanya hivyo, Syria na sasa ni Ukraine.

USA atakaa akiangalia tu.

There were supposed to watch (closely) the rise of Vladmir Putin.
Ngoja asaini kuwa member NATO.
 
Back
Top Bottom