Rais Putin kutangaza usiku huu Russia kutambua rasmi majimbo huru yaliyojitenga ya Donetski na Luhansk

Rais Putin kutangaza usiku huu Russia kutambua rasmi majimbo huru yaliyojitenga ya Donetski na Luhansk

Kweli brother eti Tanzania Ina uchumi mkubwa kuliko North Korea?
Kwamba korea anayejaribu kila siku makombora anashindwa kujenga kiwanda cha mbolea kisa hana pesa, ila pesa za kujaribia kombora anazo, hivi wanajua gharama kweli ya kurusha kombora hata 1 hawa watu? Iran uchumi mbovu shida BBC na CNN
 
kitu kinachochekesha ni sie wa Africa kushabikia na kusifia upuuzi ooh sijui Mwanaume kasogeza kete dume, ohh wapigabe sasa, sijui nani akiwashe wapewe kichapo, wakati inajulikana fika hata likitokea la kutokea ukiacha wananchi wa nchi hizo husika kutaabika na hiyo vita, next itakua ni sisi wa Africa hata kama vita hiyo haitapiganiwa huku Africa...


hekima na busara ndio inatakiwa kutumika zaidi ya ubabe wa hizi 2 super powers ambazo zinaonyesha fika greedy ya next level..

amazing thing ni kuwa nchi kama China iko kimyaaa kwenye haya wakati yeye ni amongst majirani wakaribu kabisaaa
Sijui hatuelewi madhara ya hii kitu kwenye uchumi wa dunia? Ndio kuna watakao faidikia, ila bei za vitu zikianza kupanda huku kwetu tutaishia kulaumu serikali kama kawaida.

Kenya washaanza kuliongelea hili: Kenyans brace for higher cost of living over Russia-Ukraine conflict

Siku hizi vita zinapigwa zaidi kwenye uchumi, ila nyasi sisi bado tutaumia.
 
Hii ultimatum Putin alishapewa mapema kabisa na Nato akiivamia ukranie Nord stream 2 is dead...Labda hufuatilii vitu...
We unafkiri Russia hataki kuuza gas ulaya?...Tena in long run Nato watatafuta alternative ya Nord Stream 1 halafu nayo waipige chini
Russia anajiandaa kuhamisha soko lake kutoka Ulaya kuelekea China na ndio maana wanajenga mtambo mkubwa wakusafirisha gesi kulekea China. Kutokana na mpango wa dunia wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, China itaongeza matumizi ya gesi ilikukidhi uhitaji wa viwanda vyake. Russia wameshapata soko jipya. Ndio maana hata Ujerumani wanahaha kutafuta mbadala wa nishati ya gesi.
 
Putin na vitabia vya kijinga sana ila atafanyiziwa na USA mpaka ataomba poo sema ana matabia yake kama ya Kagame kuua watu.
Unamchukia sana Putin bwana Ako yupo Jimbo gani State au yupo hapa Yombo kwa Limbooa
 
View attachment 2126631

Rais Vladimir Putin akitia saini amri (the Decree) kutambua majimbo ya Donestk na Luhansk kuwa majimbo huru. Picha na Reuters.

Rais wa Russia Vladimir Putin usiku huu anatarajiwa kutangaza majimbo ya Donetsk na Luhansk kama majimbo huru.

Majimbo haya mawili yaliyo upande wa mashariki mwa Russia, ndio kiini cha mzozo unoendelea unaozihusu nchi za Ukraine, NATO, Russia, Marekani na nchi za magharibi.

Pia Rais Putin atasaini amri (decree) ya kutambua eneo zima lijulikanalo kama Donbass kama eneo la Russia.

Baada ya kutangaza uamuzi huo wa Russia, kiongozi huyo wa Russia ataamuru majeshi ya Russia kuingia katika majimbo hayo ili kulinda maslahi ya Russia kiusalama na kijeshi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameitisha kikaao cha dharura cha umoja wa mataifa ambapo suala la uamuzi wa Russia kutambua majimbo ya Donetski na Luhansk litajadiliwa.

Wakati huohuo Russia imeitisha kikao cha dharura umoja wa mataifa kujadili suala la Ukraine baada ya mkuu wa majeshi ya Russia kusema kwamba Ukraine imeweka majeshi yapatayo 60,000 katika eneo la Donbass.

Putin anadai kwamba kiongozi wa ilokuwa USSR Lenin alifanya maamuzi ya kimakosa katika kuangalia mipaka ya USSR na ndio kiini cha matatizo ya leo hii.


 
Imagine the outrage if China built an impressive military alliance and tried to include Canada and Mexico in it.
 
Haitakuja kutokea hii labda USA iwe already divided.
Basi waza siku serikali ya Mexico iingie ambayo haina mahusiano mazuri na Washington kisha ikaombe msaada wa ulinzi kutoka kwa Urusi, unadhani Marekani itakubali? Kama haitakubali kwanini Urusi yeye ndo akubali?
 
propaganda gani na vitu viko wazi mkuu, ingia kwenye shares za soko la moscow au St petersburg uone mwenyewe au haya mambo huelewi.
Nchi za kikomunisti lini zimetoa takwimu za ukweli, sawa na kisema korea kaskazini wanashindwa hata kujenga kiwanda cha mbolea ila wanaweza kutengeneza kombola la masafa marefu na wakalifanyia majaribio, wajua gharama za kufanya majaribio ya kombola moja?
 
Nchi za kikomunisti lini zimetoa takwimu za ukweli, sawa na kisema korea kaskazini wanashindwa hata kujenga kiwanda cha mbolea ila wanaweza kutengeneza kombola la masafa marefu na wakalifanyia majaribio, wajua gharama za kufanya majaribio ya kombola moja?

Soko Si takwimu, au huelewi soko la hisa linakuwa unaweza kununua Na kuuza shares hata Kama uko Tz. Inaelekea huelewi hivi vitu
 
Putin ni hatari kwa hii dunia. Yaani natamani afe tu. Dictator mkubwa huyu.
Inaonekana uielewi hii dunia. Usione tu mataifa yanawatetea UKRAINE na kupambana na Urusi kuna jambo nyuma ya pazia ambalo akili zetu sisi mashabiki maandazi hatuwezi kulijua

Unadhani kwa nini Russia ni taifa kubwa lakini liko kimya sana kwenye mambo yake? Jiulize. Russia ilitokana na kuvunjwa kwa USSR ambao ulikuwa ni muungano wa majimbo kama ilivyo USA na ndipo anguko hilo likasababisha kutokea mataifa haya na dunia (USA na wenzake) kwa sababu za kiuchumi na kibiashara haitaki kuona muunganiko ule wa USSR unarudi kwani ulikuwa tishio kubwa sana. Russia kuchukua hayo majimbo ni kurudisha nguvu ya USSR ya zamani ambapo dunia haitaki kusikia

Usimchukie Puttin ule ni mpango mkakati wa muda mrefu wa Russia na Marais wote wa Russia wanapigania kurudisha umoja wa USSR kimyakimya
Tulioenda kombe la Dunia Russia tulikuwa tunachunguzwa balaa wanajua kila mtu amekuja pale kwa kisingizio cha World Cup kumbe ni jasusi
 
Back
Top Bottom