Inaonekana uielewi hii dunia. Usione tu mataifa yanawatetea UKRAINE na kupambana na Urusi kuna jambo nyuma ya pazia ambalo akili zetu sisi mashabiki maandazi hatuwezi kulijua
Unadhani kwa nini Russia ni taifa kubwa lakini liko kimya sana kwenye mambo yake? Jiulize. Russia ilitokana na kuvunjwa kwa USSR ambao ulikuwa ni muungano wa majimbo kama ilivyo USA na ndipo anguko hilo likasababisha kutokea mataifa haya na dunia (USA na wenzake) kwa sababu za kiuchumi na kibiashara haitaki kuona muunganiko ule wa USSR unarudi kwani ulikuwa tishio kubwa sana. Russia kuchukua hayo majimbo ni kurudisha nguvu ya USSR ya zamani ambapo dunia haitaki kusikia
Usimchukie Puttin ule ni mpango mkakati wa muda mrefu wa Russia na Marais wote wa Russia wanapigania kurudisha umoja wa USSR kimyakimya
Tulioenda kombe la Dunia Russia tulikuwa tunachunguzwa balaa wanajua kila mtu amekuja pale kwa kisingizio cha World Cup kumbe ni jasusi