Rais Ramaphosa anafikiria kujiuzulu kutokana na kashfa ya kuficha Mabilioni shambani

Rais Ramaphosa anafikiria kujiuzulu kutokana na kashfa ya kuficha Mabilioni shambani

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,860
Vyanzo mbalimbali ikiwemo Bloomberg vimeripoti kuwa Rais Cyril Ramaphosa yuko kwenye mashauriano na watu wake wa karibu juu ya uamuzi huo kutokana na ripoti ya uchunguzi kuonesha alivunja Katiba ya Nchi.

Ramaphosa anakabiliwa na kashfa ya kuficha zaidi ya Tsh. Bilioni 9 kwenye shamba lake, fedha hizo ziliibwa na wafanyakazi wake ambao inadaiwa aliwateka ili kuwanyamazisha.

Mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa, Arthur Fraser alimfungulia kesi Rais Ramaphosa Juni 2022 juu ya kuficha pesa shambani. Chama Tawala (ANC) kimetangaza kukutana Desemba 16, 2022 kujadili kashfa hiyo.
 
Hiki ndicho kinakitofautisha chama cha ANC na vyama vingine tawala vya ukombozi.

Rais ana chombo cha kumuwajibisha ikitokea amevunja katiba au amepata kashfa yenye mashiko badala ya kusubiri mpaka ballot box.

Rais kuwa kiongozi wa chama chake cha siasa kinachotakiwa kuisimamia serikali ambayo nayo anaiongoza yeye ni jambo la ajabu sana.
 
Auae kwa upanga naye huuawa kwa upanga!

Ripoti ya Kamati maalum iliyoundwa kuchunguza upotevu/wizi wa pesa za umma huko Afrika Kusini imetoka na inamtuhumu moja kwa moja bwana Ramaphosa kuwa alihusika.

Duru zinatabanaisha huenda Rais huyo wa Afrika ya Kusini aliye mfitini mtangulizi wake bwana Zuma atajihudhuru muda wowote kuanzia sasa.
 
Kwetu hata ndege zote zishikilìwi hamna anae ajibika congrats Africa kusini kuajibisha viongozi wenu
 
Hivi pana mtawala wa kiafrica asiyedokoa mboga jikoni. Kwa uzoefu wangu naona wote wanafanana. Kwao uongozi ni ajira na sio wito.
 
Auae kwa upanga naye huuawa kwa upanga!

Ripoti ya Kamati maalum iliyoundwa kuchunguza upotevu/wizi wa pesa za umma huko Afrika Kusini imetoka na inamtuhumu moja kwa moja bwana Ramaphosa kuwa alihusika.

Duru zinatabanaisha huenda Rais huyo wa Afrika ya Kusini aliye mfitini mtangulizi wake bwana Zuma atajihudhuru muda wowote kuanzia sasa.
atajiuzuru
 
SA km China ukizingua wanakusekwa ndani sio km bongo ukiiba unaishia kuchekewa ikaulizwe system
 
Back
Top Bottom