Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Rais William Ruto ameapa kutumia nguvu zote alizonazo kuhakikisha maandamano ya Azimio yaliyopangwa kufanyika Jumanne wiki ijayo, hayatazidi kuwa machafuko na ghasia.
Hisia za Ruto zinafuatia hatua ya Muungano wa Azimio la Umoja kurejesha maandamano nchi nzima juu wakidai Kenya Kwanza kushindwa kufanya mazungumzo yenye manufaa ya pande mbili.
Akizungumza mjini Malava, Kaunti ya Kakamega siku ya Jumamosi, Rais Ruto alisema aliwasiliana na kiongozi wa Azimio, Raila Odinga katika juhudi za kutafuta suluhu ili kumaliza mzozo unaoendelea kati ya upinzani na serikali yake.
Licha ya juhudi zake, Ruto anasema Raila ameonekana kukataa n kuwaelekeza wafuasi wake kushiriki maandamano hayo.
"Mimi niliwaambia ile wiki ingine; nikaita yule mzee wa kitendawili na nikamwambia wewe wacha hii maandamano tupeleke hii maneno yote unasema bunge; wabunge waangalie kama kuna maneno ya ukweli," alisema Ruto.
"Sasa ati wamekataa hiyo ya kwenda kuongea kwa amani kwa bunge. Ati wanataka kurudi maandamano. Ati waende wavunje mali na kuharibu biashara ya wananchi. Mimi ndio commander-in-chief. Nyinyi mtajua hamjui. Wawache hiyo mchezo."
Huku akiyafananisha maandamano ya Azimio na uhujumu uchumi, Ruto aliongeza kuwa kipaumbele cha serikali yake ni kuboresha maisha ya Wakenya na kutokuwa na ugomvi na upinzani.
"Mambo ya uchaguzi tulimaliza last year. Ile kazi imebaki sasa si ya viongozi; kazi imebaki ni maendeleo ya wananchi," aliongeza.
"Hakuna mali au biashara ya wananchi itaharibika tena. Serikali ya Kenya itasimama imara kuhakikisha inalinda maisha, mali na biashara ya kila mwananchi."