Rais Ruto aapa kuwachakaza wapinzani wakiendeleza maandamano

Rais William Ruto ameapa kutumia nguvu zote alizonazo kuhakikisha maandamano ya Azimio yaliyopangwa kufanyika Jumanne wiki ijayo, hayatazidi kuwa machafuko na ghasia.

Hisia za Ruto zinafuatia hatua ya Muungano wa Azimio la Umoja kurejesha maandamano nchi nzima juu wakidai Kenya Kwanza kushindwa kufanya mazungumzo yenye manufaa ya pande mbili.

Akizungumza mjini Malava, Kaunti ya Kakamega siku ya Jumamosi, Rais Ruto alisema aliwasiliana na kiongozi wa Azimio, Raila Odinga katika juhudi za kutafuta suluhu ili kumaliza mzozo unaoendelea kati ya upinzani na serikali yake.

Licha ya juhudi zake, Ruto anasema Raila ameonekana kukataa n kuwaelekeza wafuasi wake kushiriki maandamano hayo.

"Mimi niliwaambia ile wiki ingine; nikaita yule mzee wa kitendawili na nikamwambia wewe wacha hii maandamano tupeleke hii maneno yote unasema bunge; wabunge waangalie kama kuna maneno ya ukweli," alisema Ruto.

"Sasa ati wamekataa hiyo ya kwenda kuongea kwa amani kwa bunge. Ati wanataka kurudi maandamano. Ati waende wavunje mali na kuharibu biashara ya wananchi. Mimi ndio commander-in-chief. Nyinyi mtajua hamjui. Wawache hiyo mchezo."

Huku akiyafananisha maandamano ya Azimio na uhujumu uchumi, Ruto aliongeza kuwa kipaumbele cha serikali yake ni kuboresha maisha ya Wakenya na kutokuwa na ugomvi na upinzani.

"Mambo ya uchaguzi tulimaliza last year. Ile kazi imebaki sasa si ya viongozi; kazi imebaki ni maendeleo ya wananchi," aliongeza.

"Hakuna mali au biashara ya wananchi itaharibika tena. Serikali ya Kenya itasimama imara kuhakikisha inalinda maisha, mali na biashara ya kila mwananchi."
Alipe mishahara aache ujinga
 
Amchinje kisa Nini?. Yeye akomae na mishahara ya wafanyakazi. Halafu shughuli za kaunti zimezorota yeye anahanagaika na maandamano.
Amchinje kwa sababu anapoteza aman ya inchi biashara za watu zinaporwa na mali kuhalibiwa. Njia rahisi ya kukomesha hili swala atume tu makachero wamtwange shaba bac
 
  • Mtoto wa mjini Vs Mzee wa mjini.
  • Bila proportional representation kwenye nafasi muhimu kitaifa, hayo ndio matokeo yake.
  • Anayeharibu nchi ni mwananchi
 
Rais William Ruto ameapa kutumia nguvu zote alizonazo kuhakikisha maandamano ya Azimio yaliyopangwa kufanyika Jumanne wiki ijayo, hayatazidi kuwa machafuko na ghasia.

Hisia za Ruto zinafuatia hatua ya Muungano wa Azimio la Umoja kurejesha maandamano nchi nzima juu wakidai Kenya Kwanza kushindwa kufanya mazungumzo yenye manufaa ya pande mbili.

Akizungumza mjini Malava, Kaunti ya Kakamega siku ya Jumamosi, Rais Ruto alisema aliwasiliana na kiongozi wa Azimio, Raila Odinga katika juhudi za kutafuta suluhu ili kumaliza mzozo unaoendelea kati ya upinzani na serikali yake.

Licha ya juhudi zake, Ruto anasema Raila ameonekana kukataa n kuwaelekeza wafuasi wake kushiriki maandamano hayo.

"Mimi niliwaambia ile wiki ingine; nikaita yule mzee wa kitendawili na nikamwambia wewe wacha hii maandamano tupeleke hii maneno yote unasema bunge; wabunge waangalie kama kuna maneno ya ukweli," alisema Ruto.

"Sasa ati wamekataa hiyo ya kwenda kuongea kwa amani kwa bunge. Ati wanataka kurudi maandamano. Ati waende wavunje mali na kuharibu biashara ya wananchi. Mimi ndio commander-in-chief. Nyinyi mtajua hamjui. Wawache hiyo mchezo."

Huku akiyafananisha maandamano ya Azimio na uhujumu uchumi, Ruto aliongeza kuwa kipaumbele cha serikali yake ni kuboresha maisha ya Wakenya na kutokuwa na ugomvi na upinzani.

"Mambo ya uchaguzi tulimaliza last year. Ile kazi imebaki sasa si ya viongozi; kazi imebaki ni maendeleo ya wananchi," aliongeza.

"Hakuna mali au biashara ya wananchi itaharibika tena. Serikali ya Kenya itasimama imara kuhakikisha inalinda maisha, mali na biashara ya kila mwananchi."
RUTO Anapotoshwa na Viongozi wa Muungano wa Kenya kwanza Ruto anatakiwa akumbuke ana FAILI ICC
 
Naomba niwakumbushe wana East Africa kwamba Yanga imeingia nusu fainali
 
Amchinje kwa sababu anapoteza aman ya inchi biashara za watu zinaporwa na mali kuhalibiwa. Njia rahisi ya kukomesha hili swala atume tu makachero wamtwange shaba bac
Acheni kujificha kwa raila. Lipeni watu mishahara na mpunguze gharama za Maisha. Yani mnashindwa kumdhibiti ma Kenzie mnahangaika na Raila.
 
Amemshindwa Mackenzie anaye ua watu ndio aje ahangaike na Raila. Ruto mpuuzi Sana.
 
RUTO Anapotoshwa na Viongozi wa Muungano wa Kenya kwanza Ruto anatakiwa akumbuke ana FAILI ICC
Mjinga tu yule. Baadala ahangaike na mishahara na madeni ya nje, anawatumia polisi kiboya. Ngoja tuone mwisho wake huyo tapeli wa UDA.
 
Ruto anaongea tu kufurahisha makundi yaliyopo upande wake, Raila na wanazimio wanapata nguvu kutoka kwa katiba yao ya mwaka 2010, hivyo raia wakiuawa kwenye maandamano Ruto na Serikali yake watawajibika kulipa gharama.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom