Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Rais Ruto amegoma kusaini Muswada wa Fedha na kuurudisha Bungeni. Hili limetokea baada ya maandamano yalikuwa yakiongozwa na Gen Z kufanyika zaidi ya wiki nchini humo. Ikulu imeripoti kwamba Rais Ruto anatarajia kuurudisha Mswada huo Bungeni kabla ya Bunge kuvunjwa baadaye leo.
Rais Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa muda wowote kuanzia sasa.
=====
=====
Pia soma: LIVE - Yanayojiri Maandamano Kenya: Waandamanaji wafika Bungeni, wawili wauawa kwa risasi
Rais Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa muda wowote kuanzia sasa.
=====
Rais William Ruto amesitisha kusaini Mswada wa Fedha, 2024 na muswada huo utarejeshwa bungeni leo tarehe Juni 26, 2024. Amependekeza marekebisho kadhaa kwenye Mswada huo kabla ya wabunge kwenda mapumziko.
Aidha ikiwa Wabunge watafanyia kazi marekebisho hayo, Spika atalazimika kuurudisha kwa rais lakini pia wanaweza kuupitisha tena bila marekebisho. Na upitishwaji wa Muswada huu unapaswa kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge nchini humo.
=====
Pia soma: LIVE - Yanayojiri Maandamano Kenya: Waandamanaji wafika Bungeni, wawili wauawa kwa risasi