Rais Ruto asitisha kusaini Muswada wa Sheria ya Fedha 2024, aurejesha Bungeni

Rais Ruto asitisha kusaini Muswada wa Sheria ya Fedha 2024, aurejesha Bungeni

Rais Ruto amegoma kusaini Muswada wa Fedha na kuurudisha Bungeni. Hili limetokea baada ya maandamano yalikuwa yakiongozwa na Gen Z kufanyika zaidi ya wiki nchini humo. Ikulu imeripoti kwamba Rais Ruto anatarajia kuurudisha Mswada huo Bungeni kabla ya Bunge kuvunjwa baadaye leo.

Rais Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa muda wowote kuanzia sasa.

Good thinking
 
Hii ndio tasrifa mpya Finance Bill imeondolewa

Rais Ruto amesema Sauti ya Watoto Wadogo ni Sauti ya Mungu, hatasaini finance bill ya 2024

Rais Ruto ameagiza Matumizi yote kuanzia ya Rais hadi Muhudumu wa ofisini yapunguzwe mara Moja

Source: Citizens tv
 
Wakishinda wakenya Nina wasiwasi na wafanyabiashara wa hapa bongo watakaza
Si kwamba maandamano ya Kenya yataleta matokeo chanya na huku kwetu? Ni kama naona Wakenya wametuandamia na sisi.

Sasa hivi viongozi wetu wako vyumbani wanarekebisha mambo. Nadhani msemo wa mwenzako akinyolewa, unafanya kazi sasa hivi.

Nawashauri wao wasione aibu wala kukaza shingo. Wawasikilize wananchi na kuwahudumia ipasavyo. Hapo watajitwalia pointi 3 muhimu.
 
Hawa vijana ambao unemployment ngoja waendelee kuongezeka serikali itavuna inachopanda muda si mrefu..
 
Back
Top Bottom