Rais Ruto asitisha kusaini Muswada wa Sheria ya Fedha 2024, aurejesha Bungeni

Rais Ruto asitisha kusaini Muswada wa Sheria ya Fedha 2024, aurejesha Bungeni

Ikiwa serikali za Kiafrika zitaamua kutumia busara na siyo ubabe uliowekwa kwa kigezo cha sheria hakuna haja ya hizi kelele,na shida hasa inakuja kutokana na nchi inakopa sana na pakutoa hela za kulipa hiyo mikopo hakuna ktk wanaotia saini mikataba hiyo anajua zitakakotoka zaidi ya kutaka kuzitoa kwa wananchi ambao hata hawana idea hizo hela zilizokopwa zilienda wapi zikafanya nini.

Mf;matumizi makubwa ya viongozi yasiyo na kichwa wala miguu,kuna umuhimu gani wa mtumishi anayelipwa salary mwisho wa mwezi kupewa posho kila akikaa kikao kuzungumzia au kupanga jambo fulani ambalo lipo kwenye uwajibikaji wake?(wenyewe hiyo posho wanaiita seat allowance),kubadilishiwa magari tena ya gharama kila mwaka,kiongozi mkuu wa nchi kusafiri na mdege wa kubeba abiria 300+ yeye anakaa humo mlinzi wake sijui katibu na mshauri yaani gharama za kurusha ndege ya abiria 300 inalipwa just kwa watu chini ya ishirini.
 
Aiseee nguvu ya umma si mchezo

Haya mambo nadhani yatazagaa kusini mwa sahara pote ..huo ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa barani Afrika

Watu wamechoshwa na ulafi wa viongozi uchwara wa Afrika
 
Nafikiri Ruto amejua kitakachotokea, ilikuwa ni kutolewa ikulu sababu popote pale pamoja na kumtii amiri jeshi mkuu jeshi linakazi ya kulinda Raia, so jeshi lisingeweza kuua watu sababu ya politician ambaye anamuda mchache madarakani wakati kenya itabaki milele.

Hata hapa bongo mnaosema polisi watawavunja miguu sijui wataua watu, jeshi haliwezi kubali kumtii mtu mmoja na kuumiza watanzania wenzao kisa mwanasiasa ambaye ataondoka madarakani.
 
Huko Kenya Rais Ruto amekubaliana na madai wa Wakenya walio wengi ya kuachana na muswaada mbovu wa fedha, zaidi sana amekubaliana na kuachana na matumizi yasiyo ya lazima na anasa kwa kupunguza bejeti ya kukirimu maofisini, magari, fenicha, safari za nje n.k kwa kuanzaia na Ofisi ya Rais yeneywe. Ameelekeza bajeti iwe ni ya kubana matumizi.
Mbona kule jukwaa letu pendwa la Ukraine umepoa sana siku hizi. Au kwa vile mpendwa wako Zeleinsky anakimbizwa kila siku
 
Ruto kaamua liwalo na liwe baada ya wabunge wengi kupinga pia huo mswada Koona isiwe kesi kama wao hawana Imani na yeye na yeye anawaridishia

Kuwa wakileta za kuleta watusi kwenye uchaguzi
Acha uongo, wabunge was Ruto ambao ndio wengi walioupitisha huo muswada. Na Jana walikimbizwa bungeni wakaingia kwenye basement.
 
Kenya sio Tanzagiza ambapo pesa zote ni za Samiah.
Tanzania haiwezi kuwa Nchi ya kipumbavu kama Kenya ndio maana Wananchi waliwadharau na maandamano yenu fake.

Wapi mgao wa umeme na maisha magumu yaliyonadiwa na Machadema? 🤣🤣
 
Yale Yale Kama CCM. Wana creat tatizo halafu wanali solve.
Angalia kikokotoo Ni tatizo lilikua created na CCM, halafu juzi wamepunguza kiwango Cha tatizo. Mazwazwa wanapiga makofi .
Kwa Kenya ni tofauti. Rais kakubali kutii sauti ya Wananchi. Huku CCM hata wakiamua kikotoo kiwe 20 hakuna wa kufanya chochote.
 
20240626_191634.jpg
20240626_185949.jpg
 
Mind games, why bunge liliupitisha katikati ya machafuko?!

Ruto anawatega wakenya.
Anajitega mwenyewe. Ni kwamba jeshi limekataa kumuunga mkono ndio maana kapiga u turn, kasahau Jana alitangazwa state of emergency. Pia kuzagaa kwa ramani ya Ikulu kumemtisha.
 
Back
Top Bottom