Rais Ruto azitaka nchi za Afrika kuacha kutumia sarafu ya dola kwenye biashara zao za kimataifa

Rais Ruto azitaka nchi za Afrika kuacha kutumia sarafu ya dola kwenye biashara zao za kimataifa

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2019
Posts
2,926
Reaction score
15,634
Rais Ruto wa Kenya amezitaka nchi za Africa kuacha kutumia sarafu ya US Dollar đź’µ đź’µ đź’µ kwenye biashara zao za kimataifa.

Ruto anashangaa kwa nini Africa tumekuwa watumwa wa sarafu ya dola ya kimarekani kwenye biashara zetu kiasi kwamba inafikia nchi za Afrika zashindwa kuuziana bidhaa zao mfano kahawa, chai, sukari kwa sababu tu ya ukosefu wa US dollar!

Anasema ni muda sasa wa kuachana na utumwa wa USD na kutumia sarafu zetu wenyewe kwani tayari Afrika tumeshatengeneza mfumo wetu mpya wa malipo..

Hayo yamejiri siku chache baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Urusi kutembelea Kenya ktk ziara maalumu ya kikazi.

MK254 msikilize Rais wako mtukufu Ruto kuanzia dkk 0.40 - 2.00, 3.00 - 5.30

===================

KENYA: RUTO ATOA WITO AFRIKA KUTOTUMIA DOLA KATIKA MIKATABA YA KIBIASHARA
Rais wa #Kenya, #WilliamRuto ametoa ushauri huo kwa viongozi wa Afrika akisema ni muda wa kuanza kuchukua hatua ya kuachana na malipo ya fedha kwa kutumia Dola ya Marekani badala yake kuwepo na mfumo wa malipo wa Pan-African Payments System (PAPSS)

Amesema mfumo wa #PAPSS uruhusu kufanyika malipo kwenda nje kwa kutumia fedha za ndani ya Nchi lakini thamani ya kile kinacholipiwa kinabadilika kulingana na thamani ya fedha ya sehemu husika badala ya wote kulazimika kutumia Dola

Ruto amesema “Tunapata tabu kufanya malipo ya huduma na bidhaa kwa kuwa kila nchi ina fedha zake, hatuna haja ya kuwa na Dola wala kuhamia kutumia fedha nyingine kama ya China, tukitumia PAPSS itasaidia biashara kufanyika kwa urahisi.”

===================================

Kenya calls on Africa to use PAPSS to ditch US dollar in trade deals

Kenya’s President William Ruto has called on African leaders to take first steps towards ditching the US dollar as the world’s reserve currency by adopting a pan-African payments system to facilitate trade within the continent.

Ruto has urged his African counterparts to mobilize central and commercial banks to join the Pan-African Payments and Settlement System (PAPSS) which was launched in January last year. Backed by the African Union and African central banks, the system for intra-African trade was developed by African Export-Import Bank (Afreximbank) and African Continental Free Trade Area (AfCFTA) Secretariat.

“We are all struggling to make payments for goods and services from one country to another because of differences in currencies. And in the middle of all these, we are all subjected to a dollar environment,” Kenya’s president said during a forum on AfCFTA in Nairobi earlier this week. “We do not have to look for dollars; our businessmen will concentrate on moving goods and services, and leave the arduous task of currencies to Afreximbank.”

This comes as many experts have increasingly raised the prospect of whether the BRICS grouping — Brazil, Russia, India, China and South Africa — could break the grip of the globally-bullish greenback.

Africa, and South Africa in particular, could be critical to any efforts to dislodge the US dollar from its place at the foundation of the world’s financial systems.

Behind the intensifying geopolitical rivalry between the United States and China are quieter initiatives that could have much greater impact in the long run: a series of moves by the BRICS bloc of countries to challenge the dominance of the greenback. The BRICS leaders would prefer the upcoming summit in South Africa to be known as a key milestone in their efforts to move away from the Western-dominated world order that has reigned since the end of the WWII – and to embrace a more diverse and representative global economic system, which would move away from a US-dollar dominance.

Source: northafricapost
 
Mbadala ndo hela gani, maana hajafafanua vizuri, Kama ni Tzs Labda tubebe Kwenye magunia kwende soko la dunia
 
Rais Ruto wa Kenya amezitaka nchi za Africa kuacha kutumia sarafu ya US Dollar đź’µ đź’µ đź’µ kwenye biashara zao za kimataifa.

Ruto anashangaa kwa nini Africa tumekuwa watumwa wa sarafu ya dola ya kimarekani kwenye biashara zetu kiasi kwamba inafikia nchi za Afrika zashindwa kuuziana bidhaa zao mfano kahawa, chai, sukari kwa sababu tu ya ukosefu wa US dollar!

Anasema ni muda sasa wa kuachana na utumwa wa USD na kutumia sarafu zetu wenyewe kwani tayari Afrika tumeshatengeneza mfumo wetu mpya wa malipo..

Hayo yamejiri siku chache baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Urusi kutembelea Kenya ktk ziara maalumu ya kikazi.

MK254 msikilize Rais wako mtukufu Ruto kuanzia dkk 0:40 - 2:00

Shilling yake inayumba sana sana na inazidi kuyumba. Shida sarafu zetu wenyewe zinayumba sana haziaminika zinashuka shuka hovyo.
Hii kamprni ya kupiga chini dollar sijui tafanikiwaaa maana naona ni kama kaupepo kameingia
 
Anajifanya gadafi eeh. Subiri wanyonya DAMU WA kizungu wamrukie. Unataka kuharibu Uchumi WA watu
 
Kutoaminika kwa sarafu zetu ni matokeo ya kuendekeza dollar.
Sidhani kama ndio sababu mkuu. Sarafu ya kenya inaanguka kwa kasi mama nafanya miamala sana safaricom to airtel money tz.
Mwaka jana mwishonj exchange rate yao ilikuwa 1kes - 18.22 tzs, ila jana 1kes - 16.88 tzs
 
Shilling yake inayumba sana sana na inazidi kuyumba. Shida sarafu zetu wenyewe zinayumba sana haziaminika zinashuka shuka hovyo.
Hii kamprni ya kupiga chini dollar sijui tafanikiwaaa maana naona ni kama kaupepo kameingia
Ruto kafafanua vizuri sana kwenye clip hiyo (kuanzia dkk ya 3.0 - 5.30) kuwa huko kutegemea USD ktk biashara zetu kunachangia ktk kushuka thamani za sarafu za nchi zetu...
 
Ruto kafafanua vizuri sana kuanzia dkk ya 3.0 - 5.30 kuwa huko kutegemea USD ktk biashara zetu kunachangia ktk kushuka thamani za sarafu za nchi zetu
Yah nimemsikiliza ila labda tutengeneze single currency ya afrika mashariki kama walivyo na CFA west afrika ili iwe rahisi kutrade kwa sababu ndani yetu kuna nchi zinanunua zaidi kwa nyingine
 
Ghadafi aliona mbali wakammaliza jamaa hawataki kabisa Africans tujitegemee wanajua kitakachowakuta kwenye uchumi wao,tukiungana na kujitambua hawatotuweza najua ipo siku tu
 
Ukiangalia hii ishu ya upungufu wa US dollar kwenye mzunguko duniani utagundua inachangiwa na china ambaye si mmiliki wa dollar ila ndo muuzaji mkuu. Hivyo its possible china anamiliki asilimia kubwa ya dollar kuliko mmarekani mwenyewe.

Ni changamoto kwelikweli kwa sisi watumiaji tusiokua na export za kutosha na kwa mmiliki asiemiliki dollar zake. Akiwaza kuprint more anajikuta kwenye hali ya dollar yake kushuka thamani dhidi ya pound na euro.
 
Nini kitatokea Kwa china kuwa na dollar nyingi,wakati huo huo Mataifa yanaachana na utegemezi wa dollar?[emoji34][emoji34][emoji34]
JamiiForums914827189.jpg
 
Shilling yake inayumba sana sana na inazidi kuyumba. Shida sarafu zetu wenyewe zinayumba sana haziaminika zinashuka shuka hovyo.
Hii kamprni ya kupiga chini dollar sijui tafanikiwaaa maana naona ni kama kaupepo kameingia
Nchi ambazo zinapinga matumizi ya dola ya kimarekani ukiziangalia zote zimechoka zinategenea misaada kutoka marekani ngoja marekani watugeukie wapizipitie upya Sera zao kwa Africa utakuwa mwanza kuanguka serekali nyingi Africa.
 
Yah nimemsikiliza ila labda tutengeneze single currency ya afrika mashariki kama walivyo na CFA west afrika ili iwe rahisi kutrade kwa sababu ndani yetu kuna nchi zinanunua zaidi kwa nyingine
tatizo ni Tanzania ndio inayotuburuta nyuma katika jumuia ya Afrika Mashariki. siko zote hawako tayari kuenda mbele
 
Sidhani kama ndio sababu mkuu. Sarafu ya kenya inaanguka kwa kasi mama nafanya miamala sana safaricom to airtel money tz.
Mwaka jana mwishonj exchange rate yao ilikuwa 1kes - 18.22 tzs, ila jana 1kes - 16.88 tzs
Yaani wewe sijui unaelewa ninachoandika? Kuyumba kwa sarafu zetu na kukosa stability ni kwa sababu ya sisi wenyewe kutozitumia kwenye biashara baina yetu, hivyo demand yake inakuwa ndogo. Tumeamua kuendekeza dollar matokeo yake ndio haya. Tukianza kutumia hela zetu kwenye hizi biashara zetu tukaiacha dollar, hela zetu zitaimarika na zitakuwa stable mkuu
 
Back
Top Bottom