Rais wa Kenya, William Samoei Ruto, leo Mei 5, 2026, amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kiuchumi na kuunganisha nguvu katika kupambana na changamoto zinazozikabili nchi zote mbili.
Rais Ruto amesisitiza kuwa Kenya na Tanzania hazigombani, bali zinakabiliwa na changamoto zinazofanana ambazo zinachelewesha ustawi wa wananchi wake:
"Tuko na maadui wengi, ndugu wa Tanzania, ndugu wa Kenya tuko na maadui wengi. Maadui wetu sio Wakenya, maadui wetu sio Watanzania. Maadui wetu ni ukosefu wa kazi na umaskini. Wacha nirudie. Ndugu wa Tanzania, Wakenya wenzangu, maadui wetu sio Watanzania ama Wakenya, maadui wetu ni kukosa ajira, umaskini na kukosa maendeleo"- Amesema Rais wa Kenya, William Samoel Ruto