benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Jumatano ya Machi 29, mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Pamoia na mambo kadhaa, ripoti ya CAG kwa mwaka fedha wa 2021/22 iliyowasilishwa bungeni leo, inaonyesha UZEMBE MKUBWA KATIKA USIMAMIZI WA MALI ZA UMMA MIONGONI MWA WATENDAJI NA WATUELE WA MHESHIMIWA RAIS
Kwa ufupi tu ripoti ya CAG imeonesha kuwa:
1. Serikali inatumia TZS bilioni 5.68 kwa mwaka kuwalisha wahamiaji haramu 3,110 waliopo magereza kwa kipindi cha mwaka hadi miaka mitano, licha ya kumaliza vifungo.
2. Kwa miaka 22 (2000-2022), Tanzania imetumia TZS bilioni 6.69 kutunza vyura 500 iliowapeleka Marekani ili kuepuka hatari ya kupotea kutokana na utekelezaji mradi wa umeme wa Kihansi. Hata hivyo, idadi yao kwa sasa haijulikani, na mkataba wa kuwepo Marekani umekwisha
3. TTCL ina madeni makubwa ya TZS bilioni 21, lakini uongozi haukuweza kutambua wadaiwa husika. (YAANI HAIJUI INAMDAI NANI)
4. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulipata hasara TZS bilioni 204.65 mwaka 2021/22 kutokana na ongezeko la gharama za mafao ya matibabu na gharama za huduma kwa wanachama ambazo hazikulingana na mapato yaliyoongezeka.

5. Ripoti ya ukaguzi wa Ukaguzi Maalum wa CAG katika fedha za Uviko-19 imebainisha madudu kadhaa, ikiwemo kwamba bidhaa zenye thamani ya zaidi ya Sh50 bilioni zilizolipiwa fedha hazijapokewa.
Taarifa ya CAG na ile ya Takukuru imebaini na kuonyesha upotevu wa mabilioni ya fedha za umma ambazo zingetumika kutekeleza miradi ya maendeleo kuboresha huduma na maisha ya wananchi ambao ndio walipa kodi.
Kwa lugha rahisi, ripoti zote mbili zimeonyesha upigaji wa fedha za umma unaofanyika ama kwa uzembe
HII Inaumiza, na hakika haikubaliki hata kidogo.
Ni Muda sasa umefika kwa mamlaka husika kuanzia vyombo na taasisi za uchunguzi na hata Ofisi ya Rais kuanza kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika kukomesha vitendo vya aina hii.
Rais Samia ameonyesha kukerwa na upotevu huu wa fedha za umma; sasa ni muda wa kuchukua hatua. tumeona uchungu wa Rais Samia, tumeona hasira yake, lakini yote hayo HAYATOSHI. HUU NI MUDA WA RAIS WA NCHI NA AMIRI JESHI MKUU KUCHUKUA HATUA
Umma hautarajii kumwona Rais waliyemkasimu dhamana ya kuongoza Ofisi Kuu ya nchi akiendelea kulalamika huku fedha za umma zikiendelea kutafunwa na wajanja wachache kila mwaka.
Japo CAG hana madaraka ya kuchukua hatua, lakini tayari ametoa mapendekezo, ikiwemo hatua za kuchukua.
Sasa ni zamu ya Rais mwenyewe pamoja na mamlaka husika kuwachukulia hatua stahiki wahusika wote wanaotajwa kwenye ripoti ya CAG kuwa wamehusika kwa njia moja au nyingine kufanya au kusababisha upotevu wa fedha na mali ya umma.
Bila kuchukua hatua, ni dhahiri hali itaendelea kuwa hivyo hivyo katika ripoti zijazo za CAG na ile ya Takukuru.
Rais Samia akatae kushiriki dhambi ya baadhi ya viongozi na watendaji ya kutafuna nchi.