Rais Samia aache kulalamika, achukue hatua mara moja

"Stupid"

Likaishia hapo.
Report ni mali ya CAG umma inatakiwa iende bungeni ijadiliwe na wawakilishi wa wananchi, waje na maazimio kwa serikali na mamlaka za uteuzi ili kuwawajibisha watakaoonekana kuhusika. Kwa hulka na silka ya Rais, si mtu wa kukurupuka na kuropoka ni mtu mtulivu anayependa kufuata utaratibu wa kisheria na kikatiba.

Ndio maana unaona hana watu wa atake asitake tutamuongezea muda wa kutawala hata baada ya muda wake wa kikatiba.
 
TUKIWASILIZA VIZURI NHIF WANAYO MAJIBU MAZURI

Nimeshuhudia vyombo vingi vya habari ikiwemo mitandao ya KIJAMII ikiandika mengi juu ya taarifa ya CAG, moja ya gazeti likasema"NHIF KINARA KATIKA MASHIRIKA YA UMMA KWA HASARA".

Inafikirisha sana ukisikia hivyo na hasa kile kiasi kilichotajwa cha zaidi ya Bilioni 200, unaweza ukaona Shirika lina matatizo au watendaji wake wameshindwa kufanya kazi lakini kumbe ukiwapa sikio wanazo hoja na majibu sahihi kabisa.

Nikafanya kazi ya ziara ya kupitia taarifa mbalimbali za NHIF juu ya namna inavyotoa huduma na namna inavyopambana katika suala zima la udanganyifu.
Nikabaini kuwa hiyo hasara iliyotajwa na CAG inatokana na madai ya watoa huduma kuwa kubwa ikilinganishwa na makusanyo yalitofanywa na Mfuko.

Nikachimbua kwa undani ili nijue sababu, nikarejea mpaka mwaka 2001 wakati Mfuko unaanzishwa nikabaini kuwa huduma zilizotolewa miaka hiyo zilikuwa chache sana ni kama mara kumi ya sasa lakini kiwango cha uchangiaji ni hicho hicho hakijaongezeka kwa wanachama wake.

Tunashuhudua huduma kubwa za kibingwa zikigharamiwa na NHIF ambazo awali hazikuwepo hivyo hapa moja kwa moja unaona kuna tatizo la msingi ambalo linajibu hiyo hasara ambayo leo tunaiona sisi ni kubwa.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, NHIF pamoja na changamoto zake lakini kuna mambo lazima yafanyiwe kazi na sisi wananchi tukubali hata kama kutakuwepo ongezeko la mchango ili waweze kugharamia hizi huduma bila kuingia hasara.

Baada ya udadisi nilioufanya binafsi NHIF nawapa pole na ninawaomba wananchi wenzangu tuwasikilize nao wanazo hoja.

Mkereketwa masuala ya Afya

Mbinga- Ruvuma
 
Mkiambiwa matibabu ni gharama hamsemi halafu mkisikia NHIF imelipa malipo makubwa kwa gharama hizo mnaanza kuishambulia lazima tukubali kuwa NHIF wanajitahidi sana hata hapo walipo pamoja na kwamba michango haijawahi kupanda
 
Raisi alijinasibu kuwa yeye sio mtu wa kufyoka bali ni mtu wa kalama naona hiyo kalamu yake imeisha wino kabisa
 
Rais samia ameshajipambanua katika kupambana na kila aina ya Ubadhirifu katika Serikali anayoiongoza. shida yenu watu wa mnataka kusikia Flani katumbuliwa sjui huyu kafanywa hivi, Hatua zinaendelea kuchukuliwa na tumeshuhudia maeneo yenye changamoto kulingana na Taarifa ya CAG.
 
Kuhusu NHIF inapaswa Tutambue kuwa Hatua kadhaa Zimeshachukuliwa kwanza NHIF imesitisha mkataba na vituo 32 vya matibabu vilivyobainika kuibia Mfuko huo na Waumishi wa Vituo vya matibabu 129 wameliobainika kuibia Mfuko wameripotiwa na Mfuko kwenye Mamlaka zao ili wachukulwe hatua
 
Lakini pia NHIF haifumbii macho watumishi wake wanaojihusisha na udanganyifu kwa Mfuko. Imeshachukua hatua za kinidhamu kwa watumishi 17 ikiwani pamoja na kufukuza kazi baadhi yao na tunajua changamoto zipo ila Mfuko unachukua hatua ila ni wajibu wetu sote kuulinda Mfuko na kuhakikisha unadumu
 
Raisi alijinasibu kuwa yeye sio mtu wa kufyoka bali ni mtu wa kalama naona hiyo kalamu yake imeisha wino kabisa
Tusiwe wepesi wa kukomaza Akili kwa kudhani Hatua Hazichukuliwi, ilihali mmeona TANOIL Imefutwa Wakurugenzi wake kwa wizi NHIF Imefungia Vituo kibao vilivyokua Vinaibia Mfuko na Wafanyakazi wake walihusika na wizi wamesimamaisha kazi, Tatizo lenu humu Mnataka kila kitu afanye Rais hii sio sawa Kabisa 🤣🤣🤣 Bi Mkubwa ana Wasaidizi aliowateua kila Idara hio kazi ya Kuchukua hatua wanaiweza wakiishindwa basi ataingia mwenye kumtimua huyo aliyeahindwa kuchukua hatua
 
Sisi ndio Wabongo!!! 😁😁😁😁😁Tukiambiwa Tulipe Bima tunadai gharama zipo juu ikitokea changamoto za hapa na pale inakua agenda ya Kitaifa. Ipo hivi licha ya changamoto za hapa na pale NHIF wamekua mstari wa mbele sana kuhakikisha hatua stahiki zinachukulia kwa watumishi wake wote wanaojaribu kufanya udanganyifu kwa namna moja ama nyingine, Watumishi zaidi ya 17 wamechukuliwa hatua za kinidhamu na baadhi wamefukuzwa kazi.
 
NHIF Wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya za uhakika, sisi wananchi tumekua mstari wa mbele kufanya udanganyifu katika matumizi ya bima zetu tulizonazo.

Tusiwadondoshee jumba bovu NHIF.
 
 

 

 
Hadi leo watu wamemdindia na yeye kaamua kudinda Ikulu
 
 
Asepe tu, haiwezekani muda wote kulalamika tu, sasa anatengeneza generation gani? Ila tutafika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…