Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Hapo ndipo mnapoonyesha ujinga mliona .Hapo hakuna dereva,Kazi inataka mtu awe kamaliza form four na cheti cha ufundi magari cha Veta yeye hana anafoji.Gari za serikali ndio maana nyingi tu ulikuwa unazikuta ziko kwenye mawe wakati zinaonekana ni kama mpya sababu mwendeshaji hana ujuzi woiwote wa utunzaji gari wala kujua hata lina tatizo lipi anajua tu kupeleka gari mbele na kurudisha reverse!!! Mpaka linafikia ubovu wa kufa kabisa
Sawa, Mazaa ameamua, WATALIPWA stahiki zao, kama hupendi rudi Burundi!
 
Asiyeridhika ndie aernde mahakamani.Short and clear.Mwenye cheti cha kugushi anayeona alionewa aende mahakamani.Hilo zoezi liliwadaka vyeti feki kwa wingi kuanzia kipindi cha Kikwete na kuhitimishwa kipindi cha Magufuli

wasioridhika wenye vyeti feki waende MAHAKAMANI
Sawa, upo sahihi kabisa, hujaridhika nenda mahakamani, wapo sahihi kuwafukuza maana waligushi vyeti.

Swali ni kwamba serikali itatumia utaratibu upi wa kisheria kuchukua hizi fedha kwenye account za wahusika kwenye mifuko ya jamii?
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Sasa waliopokea vyeti feki je., nadhan kama walitumika vizuri wakatoa huduma inavyostahiki wapewe haki zao kwa sababu hata walioajiriwa kwa sifa uko maofisini wana viburi vya hali ya juu kabisa.,
 
Kisheria kughushi nyaraka ni jinai...wanatakiwa washtakiwe......
Sawa kwenye hilo tupo pamoja.....
serikali imeamua haiwashtaki bali imewafukuza tu aliyeonewa ndo aende mahakamani si ndio?

Na wahalifu wamekubali makosa hawaendi mahakamani kuishtaki serikali wanapambana na hali zao...

Swali ni kwamba zile pesa serikali itafuata utaratibu upi wa kisheria kuzichukua kwenye account za mifuko ya jamii ya wahusika bila hukumu ya mahakama?

Ili kuchukua hizo fedha, mahakama inatakiwa ihukumu wahusika baada ya serikali kuwafungulia mashtaka.

Hiyo hukumu inatakiwa ieleze kuwa serikali ilipwe fidia kwa kutumia stahiki za waajiriwa, na kwa stahiki zisizotosha fidia basi watuhumiwa watumikie kifungo.

Huo ndo utaratibu wa sheria kama unataka ufatwe.

Baada ya hukumu raisi anaweza pia kutangaza msamaha na akawaacha.

Ndo maana nakwambia tatizo si sheria, tatizo ni msamaha kama watapewa. Hutaki wasamehewe kwa sababu unazozijua wewe.
 
Mchakato umeanza wa kumuita nwenye heri... kisha saint..

St Magufuli[emoji16][emoji16]
Rest in peace Jembe mafii yako. Limeiba matrillion na bila aibu hadi rambirambi. Limeondoka na halirudi tenaaaaaaaaaa na life tena huko lilipo.
 
Nakusikitikia sana. Wewe na huu uzi wako ndio laana kwa inchi yetu. Huwezi kuja kutetea majitu yamefoji vyeti wakati kuna ndugu zako wanalalamika kukosa ajira na wamesoma na uwezo wanao.

Wewe ndio ukoma kwa taifa letu na ndie mnafiki sababu unashindwa kutetea haki unatetea ubadhirifu ukiita haki. Wewe na hii namna ya kufiriki yako ndio laana kwa taifa letu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe Kuna laana kubwa zaidi ya kudhulumu jasho la watu , Mungu mwenyewe kaamua kumuadhibu Jiwe na wewe bado unafanya yaleyale angalia mkono wa bwana utakushukia , hata Jiwe alifikiri yupo sahihi kwenye kila kitu kumbe amekosea mambo mengi sana na ameathiri watu wengi sana na familia zao , mpaka Mungu akaamua kuingilia kati muwe mnajifunza .
 
Wewe nawe ni mmojawao. Unatufanya wengine hatukusiliza hotuba ya Rais ? Mama kazungumzia darasa la saba wewe.
Pimbi kweli wewe kwahiyo kila anayetetea Jambo naye Ni mhusika ? Use common sense or rational procedure to think and act .
 
Kwa hiyo muajiriwa anapofanikiwa kumrubuni muajiri basi vyeti vyote vinageuka vinakuwa halali....??
Unaelewa maana ya mwajiri kuwafanyia interview wafanyakazi kabla ya kuwaajiri ? Kama mwajiri anawaajiri huku wanna vyeti feki kazi ya huyo mwajiri ni nini sasa ?
 
Michango iliyokuwa inakatwa ilitoka kwenye mshahara ambao haramu......sio tu hawapaswi kulipwa bali wanapaswa hata kurudisha mishahara yote waliyokuwa wanapokea huku wakijua wao ni matapeli.....UADILIFU UANZIE HAPO KWANZA.....
Una akili za kitoto kweli , kwahiyo wakirudisha hiyo mishahara na nyinyi mtawarudishie nguvu zao na huduma walizozitoa kwa muda wote waliofanya kazi ?
 
Hongera Rais , kwa kuamua kulipa haki zao stahiki Mungu akubaliki sana . Katika hotuba yake leo amesema watumishi wa darasa la na vyeti feki walikuwa wakichangia mifuko ya hifadhi ya jamii hivyo amewataka waajiri wote kuhitimisha utumishi wao kwa kuwalipa stahiki zao.

=========

RAIS SAMIA SULUHU: Changamoto nyingine ni suala la watumishi wa darasa la saba waliostaafishwa ajira, kuhusiana na suala la watumishi hawa waliositishwa ajira kama mnavyokumbuka serikali ilitoa msamaha na kuwarejesha kazini watumishi walioajiriwa kabla ya tarehe 20 May 2004 ambao hawakufanya udanganyifu wa vyeti pamoja na watumishi waliojiendeleza na kujipatia sifa stahiki kwa mujibu wa miundombinu ya utumishi wa umma.

Kupitia msamaha huo, nafahamu kuwa watumishi 4,380 walirejeshwa kazini, hata hivyo napenda kutumia fursa hii kurudia maelezo ya serikali kwa waajiri kuhusu kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kuhitimisha ajira za watumishi walioajiriwa kwa elimu ya darasa la saba na wale walioghushi vyeti.

Hapa niwaagize waajiri wote waliokuwa na wafanyakazi wa aina hii, wafanye inavyowezekana kila mwenye haki aweze kupatiwa haki yake. Natambua kwamba, wafanyakazi hawa walikuwa wanakatwa makato inayokwenda kwenye mifuko ya jamii, ile ni haki yao. Walitoa jasho lao wakakatwa wakapeleka kule.

Kwa hiyo niombe sana waajiri, niwaombe sana waajiri, wale wasio na kumbukumbu za wafanyakazi wale waziweke kumbukumbu vizuri na wale ambao na wale ambao hawajalipwa kwa kisingizio kwamba serikali haikutoa muongozo, muongozo sasa ni huu, kila mwenye haki yake alipwe haki yake.

Na hapa naitaka ofisi yangu ya utumishi na utawala bora kusimamia zoezi hili.

View attachment 1770861Rais Samia Suluhu akihutubia siku ya wafanyakazi duniani jijini Mwanza​
Huyu mama yetu hajawa Rais kwa bahati ; hwenda Mungu kaamua kutuliza mioyo iliyopondeka taratibu.Ingawa hakuongeza michuzi kwa wafanyakazi lakini sababu alizotoa zimejaa matumaini
 
Huna Akili hata kidogo,mlipeleka vyeti feki tunaanzia hapo mlipwe haki yenu then tuwapeleke kortini kwa kughushi.
We Pimbi kwahiyo vyeti ndio vilikuwa vinafanya kazi ? Sio kila anayetetea wahanga nae mhusika , mimi Sina roho mbaya ya kihutu kufurahia haki za binadamu kudhulumiwa , Sasa na nyie mlipe nguvu zao na huduma walizozitoa kwa muda wote waliofanya kazi .
 
Hapa kuna kituko kikubwa tu unakuta mfano Asha Mataputapu alisoma chuo cha ualimu

Cheti hicho hicho unakuta kuna walimu 10 wameajiriwa sehemu mbali mbali kwa jina hilo hilo la Asha mataputapu

Ukiwambia lete cheti cha form four original wanakuwa hawana anacho mmoja tu.

Wengine alikuwa akiomba kazi yeye anampa ndugu yake darasa la saba akaombee kazi cheti hicho hicho .Ilipofika uhakiki huyu mwingine akiomba cheti original nduguye kuwa nipe na mimi kikahakikiwe nduguye anaogopa jela au kufukuzwa kazi sababu kitaonekana mara ya pili

Waathirika wakubwa wa kupeana vyeti wengi walitoka mikoa miwili ya watu wanaojifanya wajanja sana nchini
We chawa wa marehemu Jiwe unasemaje ? Vipi jeshini , polisi ,magereza , uhamiaji , usalama wa taifa wamejaa mpaka kumi wanakitumia cheti kimoja na wana vyeo vikubwa kweli double standard ya nini ?
 
Cheti feki alifanya kazi gani? ya kumdhulumu mwenye cheti halali asipte haki yake ya kuajiriwa akae yeye?

Vyeti feki wanatakiwa kurudisha pesa zote toka tarehe ya kwanza waliyoajiriwa ni wahujumu uchumi na wezi wa mali ya umma kwa njia ya udanganyifu serikali inatakiwa itaifishe hadi mali zao ziwe pensheni au chochote
Marehemu baba yako aliyeiba tilioni moja na nusu sio mwizi ? Na zile tillioni saba alizodhulumiwa na Kagame alizompa Tanzanite yeye sio mhujumu uchumi ?
 
Tupo pamoja Yehoyadaya katika hili.Kila hela waliyolipa kutoka kwenye mishahara yao ni mali ya serikali na walichokula kwenye social funds ni mali ya serikali wasilipwe.

Furthermore hela yote waliyolipwa kwa miaka yote interest iwe calculated walipe.Watu wanaiba fedha zetu halafu eti walipwe mafao.Mwishoni tutambiwa warudishwe kazini na muda wote ambayo hawakulipwa walipwe with disturbance allowance!Inaudhi frankly.
Na ndio itakavyokuwa Kama unaumia we umia tu , mbona Jiwe hajarudisha tilioni moja na nusu na tilioni saba alizodhulumiwa na Kagame alizompa Tanzanite ?
 
Vyeti fake ni jinai sasa alipwe ksha apelekwe mahakamani afungwe kwa udanganyifu kisha alipe ma fidia.
Je watakubali hilo?
Uvivu wa waajiri hauwezi kuwapeleka jera waajiriwa
 
Back
Top Bottom